Kuna haja ya serikali kuingilia kati kwenye uchaguzi ujao wa TFF

kishumbaz

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
904
1,243
Kwa jinsi wapenda mpira tunavyoumizwa, kuna haja ya serikali kuingilia kati katika uchaguzi ujao.

Tunajua jana TFF waliwaangushia jumba bovu serikali, kotokana na conflict of interest zao, sababu mazingira ya lile tamko lao lilionyesha dhahiri kama waliwatengenezea Bomu serikali liwalipukie wenyewe.

Sasa wapenzi wa mpira tumechoka na huu ujinga ujinga, tunaomba serikali uchaguzi ujao, watuwekee watu wenye weledi na uchungu na mpira wetu na wenye explosure kimataifa, mfano kama yule mmiliki wa Mbao aliyekuwa kocha kwenye vilabu vya England na akawa mkurugenzi wa michezo, akina Kali Ongala, Kina Mzee Oscar Koloso nk.
 
Watu wa mpira na wenye explosure ni wengi mkuu, ila Karia kajiwekea securities kubwa ya kushinda uchaguzi ujao.
 
Hata Dr. Tiboloa anaweza kuwa Rais bora wa TFF kuliko hawa ambao wanateua bodi hata kupanga ratiba za ligi hawawezi na wanalipwa pesa na wadhamin ila kulipa timu changamoto mfano Lipuli, waamuzi hawalipwi yaan ni bora liende.
 
Wana Yanga mnateseka sana hata na vitu ambavyo havijasababishwa na Karia.

Au muombeni tena Jamal Malinzi agombee tena hicho cheo hapo TFF. Maana chini ya uongozi wake miaka yote Yanga ndio ilikuwa Bingwa.

Yanga mnaongozwa na viongozi wa Club wasiojielewa na kukosa Busara basi kilakitu mnaona mnaonewa na Karia.
 
Hata waliopo wapo pale kwa sababu ya serikali kuweka mkono tatizo serikali inaweka watu kwa kigezo cha royality na connection kwa serikali bila kujali uwezo katika fani husika na hii inafanyika kwenye taasisi zote unazozijua wewe kama CWT, BAMITA, BASATA n.k.

Ndo maana watu wanaoujua mpira wanagombea nafasi mbalimbali cha kushangaza wanapata kura zisizotosha na wanafanyiwa fitina kama unavyoona vyama pinzani kwenye uchaguzi mkuu kisa hawaaminiki kuwa royal kwa serikali.

Refer uchaguzi wa TFF uliowaweka hawa viongozi waliopo wapinzani wao wote walifanyiwa fitina kama akina Shaffih Dauda,alikamatwa Mwanza akitafuta kura na kupewa kesi,akina Malinzi akapewa kesi ya uhujumu uchumi na serikali. So mambo yako hivyo.
 
Watu wa mpira na wenye explosure ni wengi mkuu, ila Karia kajiwekea securities kubwa ya kushinda uchaguzi ujao.
Ni kweli kama ameshatengeneza chaini kuanzia wilayani akaweka wajumbe wake basi anakuwa ameshamaliza mchezo.
 
Wana Yanga mnateseka sana hata na vitu ambavyo havijasababishwa na Karia.

Au muombeni tena Jamal Malinzi agombee tena hicho cheo hapo TFF. Maana chini ya uongozi wake miaka yote Yanga ndio ilikuwa Bingwa.

Yanga mnaongozwa na viongozi wa Club wasiojielewa na kukosa Busara basi kilakitu mnaona mnaonewa na Karia.
Huu unaz ndiyo uliotufikisha hapa...tunataka kiongozi mwenye uchungu na soka la nchi hii na siyo kiongozi mpigaji!
 
Hata waliopo wapo pale kwa sababu ya serikali kuweka mkono tatizo serikali inaweka watu kwa kigezo cha royality na connection kwa serikali bila kujali uwezo katika fani husika na hii inafanyika kwenye taasisi zote unazozijua wewe kama CWT, BAMITA, BASATA n.k...
Haya mambo ya kuingiza siasa kwenye utendaji yanaadhiri sana hata maendeleo ya nchi! Ukimchomeka mtu wa namna hii kwenye institution muhim kama hizi lazima aharibu, na kingine ni ile Ego kuwa mimi ni mwanasiasa na nmewekwa hapa na watu wakubwa hakuna wa kunitoa, anafanya mambo hovyohovyo, anatengeneza system yake ya upigaji humu, na taasisi inakuwa hati miliki ya kakikundi ka watu fulan badala ya kuhudumia wananchi.
 
kweli kabisa mkuu
 
Hata Dr. Tiboloa anaweza kuwa Rais bora wa TFF kuliko hawa ambao wanateua bodi hata kupanga ratiba za ligi hawawezi na wanalipwa pesa na wadhamin ila kulipa timu changamoto mfano Lipuli, waamuzi hawalipwi yaan ni bora liende.
Tibohora hana uwezo wowote zaidi ya kubebwa na vyeti
 
Chama cha mpira Tanzania ni cha ovyo sana. Nchi nyingine ukisikia Rais wa chama cha mpira nj mtu mwenye akili zake na anakua na ngubu sana.

Cha ajabu hata sikumbuki jina la Rais wa TFF.
Kwa jinsi wapenda mpira tunavyoumizwa, kuna haja ya serikali kuingilia kati katika uchaguzi ujao.

Tunajua jana TFF waliwaangushia jumba bovu serikali, kotokana na conflict of interest zao, sababu mazingira ya lile tamko lao lilionyesha dhahiri kama waliwatengenezea Bomu serikali liwalipukie wenyewe.

Sasa wapenzi wa mpira tumechoka na huu ujinga ujinga, tunaomba serikali uchaguzi ujao, watuwekee watu wenye weledi na uchungu na mpira wetu na wenye explosure kimataifa, mfano kama yule mmiliki wa Mbao aliyekuwa kocha kwenye vilabu vya England na akawa mkurugenzi wa michezo, akina Kali Ongala, Kina Mzee Oscar Koloso nk.
 
Natamani Li Wallace Karia lishindwe kwenye huu uchaguzi unaokuja. Limekaa kilafi lafi tu! 😋Siamini kama limeshawahi hata kucheza mpira kwenye ngazi yoyote ile. Limejawa tu na haiba ya upigaji, uccm na usimba!😥
 
siku tukipata viongozi wa tff wasioweka unazi kwenye soka letu mpira wetu utafika mbali.
Katika uongozi wa Karia, Timu ya Taifa imefika AFCON, Vilabu vya Tanzania mara mbili vinatoa wawakilishi wanne. Sijajua hatua kama hii imewahi kutokea lini katika awamu zote za uongozi wa TFF na FAT. Acheni mpira uchezwe uwanjani ambapo kila mtu anaona timu nzuri na mbovu
 
Back
Top Bottom