harakat
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 2,887
- 1,350
Kwanza kabisa nimshukuru sana Mh Jaffo kwa kujitahidi kulizungumzia suala la bima ya Afya na kutaka kila mtanzania apate hii ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo hasa pale wathusika wanapokua hawana cash on hand.
Bima ya Afya imekua mkombozi sana kwa watu wengi wanaoitumia hasa wafanyakazi wa serikali na familia zao kama inavyoruhusiwa kwenye utaratibu wa bima hizo.
Imekua ni nguma sana kwa hizi bima kutolewa kwenye baadhi ya hospitali na hata ukikuta zinatolewa huwa wanatanguliza wale wanaolipia Cash kwanza kana kwamba wanaotibiwa kwa bima wao hawalipi fedha bali wanatibiwa bure kumbe wanaotibiwa kwa bima wao walishalipa fedha hizo kwa makato yaani ni sawa na Pre-paid service.
Kuna haja ya dhati kabisa ya serikali kuhakikisha kwamba wanaweka utaratibu mzuri na mahospitali ili watumiaji wa bima wawe wanapatiwa huduma nzuri inayokidhi mahitaji ya mteja.
Pia hizi huduma zimewekwa kwenye madaraja tofauti ila sioni kifo cha mwanadamu kikiwa na daraja lolote wote huwa wanakufa tu kwa kwa kupoteza uhai.
Huduma wanazopewa watu wanaotumia Bima ya Afya sehemu nying imekua ya kusuasua na ambayo inatia mashaka hasa wale wanaotumia daraja la mwisho.
Ninadhani ni muda muafaka sasa kwa serikali kuingilia kati kwa kuweka utaratibu mzuri zaidi wa kuhakikisha kwamba huduma hizi zinztolewa katika kiwangi kinachotakiwa.
Nawasilisha