Kuna haja ya kuwepo masomo ya ulazima yenye kuakisi mazingira yetu huko mashuleni

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
492
1,000
Imezoeleka shule za sekondari kuwa Kuna utitiri wa vitabu vya fasihi kwa wastani havipungui 12 nje ya vitabu vya masomo mengine ya kawaidaz ambavyo kimsingi mchango wake ni mdogo Sana kwenye maisha ya mwanafunzi baada ya kuhitimu masomo yake.

Sasa kwanini yasiwepo masomo maalumu kama vile ufundi au ujasiliamali na kujitegemea ambayo yatafundishwa kuanzia shule ya msingi Hadi sekondari na iwe lazima kila mwanafunzi kuyasoma na kufaulu na ikitokea ukafaulu masomo mengine halafu kwenye Hayo ukafeli Basi kuwe na penalt.

Hii itasaidia hata kijana akifeli kuendelea na level nyingine ya elimu Basi muda ule aliokaa SHULENI atoke na kitu/fani itakayomfanya aweze kuitumia iwe kwenye ufundi au biashara.

Imekuwa ikiumiza Sana kuona kijana kasoma Hadi kidato cha nne akifeli anakuwa kafeli kotekote kwani Hana analolijua zaidi ya kusoma na kuandika tu, lakini akipelekwa veta akasoma kozi ya miezi mitatu au sita ghafla anakuwa fundi mzuri Sana. Sasa endapo hayo masomo aliyoyasoma kwa muda mchache yasiwe sehemu ya mosomo huko shule ya msingi na sekondari ili watoto wayasome kwa muda mrefu na wakihitimu wawe mafundi kwelikweli na Kama ni biashara wafanye biashara kweli kweli.

Kiufupi masomo yetu ya akisi moja kwa moja mazingira yetu isiwe inatumika nguvu kubwa kumkaririsha mtoto mambo yasiyo na uhalisia lakini hayatakuwa na msaada kwake hata baada ya kumaliza shule.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom