Inanambo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 4,037
- 2,839
Leo nimemsikia mkuu wa polisi kanda maalum ya DSM akiwataka kwenye nyumba kuweka picha ya mpangaji kwenye mikataba. Hii itasaidia utambuzi kwenye uhalifu. Kwa maoni yangu napenda kumwambia mkuu huyu kuwa wahalifu DSM si wapangaji tu.
Kuna tabia iliyojengeka hapa mjini ya majirani kutofahamiana pamoja na wajumbe wao wa nyumba kumi hawajui nani anaishi mtaani kwake, na wakaazi pia hawamjui mjumbe. Watu wanaamka saa kumi alfajiri wanarudi makazi saa 4 usiku hoi. Ni vema ule utaratibu wa kuripoti kwa wajumbe ukarudi.
Pia wakaazi wajulikane wao ni nani, wanafanya shughuli gani, wamepanga au wanamiliki nyumba mtaani, kaya ina watu wangapi, watoto n.k. Sense ya Community irudi. Hii itasaidia shughuli za usafi, kuwajua wazururaji;panya road wacheza pool table, wanafunzi, house girls na house boys.
Tena watu wafahamike kwa majina yao matatu na si kwa majina ya watoto au waume. Haya maisha ya kuingia ndani na kutoka getini ukiwa ndani ya Gari tena tinted inapelekea wakaazi wa eneo fulani kutofahamika. Naona system ya registration mitaani itasaidia kuondoa uhalifu na watoto wa mbwa.
Nakaribisha maoni yenu tumsaidie kamanda wetu wa uusalama kanda maalum ya DSM.