DOFFA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2016
- 425
- 233
Chama walimu inakata asilimia fulani kwenye mishahara ya walimu kwa
MADHUMUNI ya:
(a) Kuendeleza na kulinda hadhi ya kazi ya Ualimu pamoja na kusimamia viwango vya juu vya maadili, ufahamu, maarifa na ujuzi.
(b) Kusimamia, kuendeleza na kulinda maslahi ya Walimu na Watendaji, katika Taasisi za Elimu na kuhakikisha kuwa kuna vivutio vya kutosha na mazingira mazuri ya kuwafanya waipende na kuizingatia kazi yao.
(c) Kuhimiza elimu na ujuzi wa Watendaji wanaohudumia Shule, Vyuo na sehemu zote zinazoshughulikia elimu.
(d) Kuwa kitovu cha maandiko ya kuwaendeleza Walimu, Wanachama na Wananchi katika elimu na mafunzo ya kazi ya Ualimu.
(e) Kuwahimiza Walimu kufanya kazi yao vizuri na kuwasisitiza waoneshe mfano bora wa kazi, uadilifu, tabia na mwenendo.
(f) Kuwakutanisha Walimu mara kwa mara ili waweze kujadili maendeleo na matatizo katika taaluma zao na kutafuta mbinu za kuyatatua, kufahamiana na kubadilishana mawazo ili kujenga utamaduni wa kujiendeleza.
(g) Kuhimiza na kuhakikisha kuwa Walimu na Watendaji wanapata huduma zote wanazostahili kiuchumi, kiafya na kijamii.
(h) Kujadili na kushauriana na Waajiri juu ya haki, maslahi na hali nyingine zinazohusiana na mazingira ya ajira ya Ualimu.
(i) Kuishauri serikali juu ya mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya elimu nchini.
(j) Kuhakikisha kuwa waajiri wanaohusika wanatambua uwepo wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na kuwaelimisha Walimu kuwa wana uhuru wa kujiunga na Chama hicho na uhuru wa kufanya mgomo pale inapobidi.
7
(k) Kusuluhisha migogoro na kutatua malalamiko mahali pa kazi kati ya Waajiri na Walimu au miongoni mwa Walimu wenyewe.
(l) Kutunga na kusimamia Sera itakayolinda hadhi ya Walimu wanawake kwa kutambua hali na maumbile yao na kuhakikisha kuwa afya zao zinalindwa bila ubaguzi wa ajira, likizo ya uzazi na huduma nyingine anazostahili Mwalimu yeyote.
(m) Kutunga na kusimamia Sera itakayolinda hadhi ya Walimu wenye ulemavu kwa kutambua hali, maumbile na mazingira yao ya kazi .
(n) Kuhakikisha kuwa katika sehemu zote za kazi Walimu hawapati bughudha ya kijinsi na kuweka utaratibu utakaodhibiti wale watakaokiuka.
(o) Kuhakikisha kuwa waajiri na Walimu wanazingatia na kutekeleza sheria na kanuni za nchi zinazohusu kazi, pamoja na mikataba iliyopo kati ya waajiri hao na Walimu au Chama cha Walimu ili mradi sheria hizo zinazingatia HAKI.
(p) Kuwaelimisha wanachama juu ya masuala yote yanayohusiana na ajira zao ikiwa ni pamoja na kuwapa ushauri wa kisheria unapohitajika.
(q) Kuhakikisha kwamba hakuna ubaguzi wa rangi, kabila, dini,
jinsi, ulemavu au hali miongoni mwa wanachama.
(r) Kuwa na uhuru wa kushirikiana na kushauriana na vyama vingine vya wafanyakazi nchini na nje ya nchi.
(s) Kuwekeza katika vitega uchumi vitakavyoboresha ustawi wa wanachama ingawa si Chama cha Kibiashara.
(t) Kutengeneza na kutetea Sera itakayolinda hadhi ya Walimu wenye ulemavu na kuhakikisha kuwa afya zao na vikwazo vinavyoathiri utendaji wao vinaondolewa na kupata huduma nyingine wanazostahili Walimu wenye ulemavu.