Kuna haja ya kuwa mwanachama wa chama cha wafanyakazi?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Vyama vya wafanyakazi vina kazi ya kutetea maslahi ya wafanyakazi na kuongeza tija kazini.
Ukiwa mwanachama hai wa chama cha wafanyakazi mahali pa kazi utalazimika kukatwa 2% ya mshahara wako kila mwezi kwenda makao makuu ya chama husika. Asilimia 2-5 ya makato hayo yanabaki tawini kwa matumizi ya viongozi wa tawi kazini.

Kwa hali ilivyo sasa Tanzania kuna haja mfanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi?
 
Hicho chama zamani kilikuwa kinajua madhumuni ya kuwepo pale kazini. Leo, nadhani kipo ili kukidhi matakwa ya wengine wala sio wafanyakazi.
Siku m/kiti akiuliza swali lolote, awe kesha aga kwao kwani waweza usirudi
 
Mishahara haiongezwi kwa nguvu wala uwepo wa TUCTA bali nguvu za wanasiasa kuomba kura za wafanyakazi wa wakati wa uchaguzi. Mfano, mishahara itapanda Mei Mosi 2020.
 
Vyama vya wafanyakazi vina kazi ya kutetea maslahi ya wafanyakazi na kuongeza tija kazini.
Ukiwa mwanachama hai wa chama cha wafanyakazi mahali pa kazi utalazimika kukatwa 2% ya mshahara wako kila mwezi kwenda makao makuu ya chama husika. Asilimia 2-5 ya makato hayo yanabaki tawini kwa matumizi ya viongozi wa tawi kazini.

Kwa hali ilivyo sasa Tanzania kuna haja mfanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi?
viongozi wa vyama vya wafanyakazi kwenye halmashaur nyingi ni watu wa masija! wengi wa watu hawa hawajui hata kwanini ni viongozi wanasubir mikutano ya mwaka ili wakale posho.
 
Back
Top Bottom