Kuna haja ya kuvifuta vyote viwili, CHADEMA na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna haja ya kuvifuta vyote viwili, CHADEMA na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sangarara, Jun 19, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Upepo wa Kisiasa unaashiria kwamba huko tunakokwenda hali inaweza ikawa tete kiasi cha kukosekana mtu wala taasisi yoyote ya kuirudisha kwenye hali ya kawaida.

  Ushindani wa vyama hivi viwili naona kama umeingia kwenye stage ingine kabisa, kiasi kwamba hata wakati wa kujadili mambo ya msingi kabisa ya Kitaifa mambo yanabadirika na kuegemea kwenye hoja za kisiasa zaidi zenye nia ya ama kubomoa chama kingine au kujijenga.

  Mfano ni mchakato wa Katiba ambao kuanzia Bungeni, ghafla ulichukua taswira ya ushindani wa kisiasa, na sasa wakati watanzania tunategemea wabunge wetu wajadiliane na hatimaye mwisho wa siku wakubaliane kwenye mambo ambayo yana maslahi kwa watanzania, ghafla pia mjadala umeamia kwenye ushindani wa hoja za kisiasa ambazo hivi sasa matusi na moja ya kiungo chake muhimu sana.

  Nikikumbuka mauhaji yaliyojitokeza kwenye uchaguzi mdogo wa ulambo na arumeru mashariki, na namna Rais Kikwete a.k.a Mdhaifu anavyoendelea kushindwa kukabiliana na chagamoto za Muungano kutokea kisiwani Unguja akibuy time kwa sababu za kisiasa, naishiwa kabisa uwezo wa kuona uendelevu wa amani na utulivu katika taifa letu ndani ya kipindi kifupi kijacho.

  Mimi kwa nia njema kabisa, naonelea kwamba, ili tuweze kuwa na Bunge lenye kusimamia Maslahi ya Watanzania na kuwarudisha watanzania katika hali ya kuendesha siasa za kuvumiliana kuna haja ya hivi vyama viwili vifutwe sababu naamini kwamba nguvu ya mabadiriko yanayohitajika iko mioyoni mwa watanzania ama sivyo muda si mrefu tutajikuta tunachepuka kutoka kwenye hoja ya kupigania ustawi wa jamii yetu na kuanza kupigania vyama.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,412
  Trophy Points: 280
  Hakuna kuvumiliana pale ambapo Utajiri wa nchi unawanufaisha wachache ndani ya Serkali fisadi na Wageni wanaojifanya ni wawekezaji kumbe ni wezi tu. Magamba imeshajifia inasubiri kuzikwa tu. CDM haitalala mapaka kieleweke.
   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hoja dhaifu kama alivyo mwenyekiti wako dhaifu,
   
 4. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,010
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Inaelekea kuwa watu wengi bado hawajaelewa maana na faida za vyama vya upinzani katika demokrasia. Kuna haja ya kutilia mkazo somo la siasa au uraia katika ngazi zote za elimu, hasa elimu ya watu wazima.
   
 5. M

  Mwanandani Senior Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hoja yaki puuzi kama sekali ya Ccm ilivo ya kipuuzi.
   
 6. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Faida zinaeleweka, lakini wasi wasi wangu ni kwamba namna ya kuendesha mfumo huu wa kisiasa bila kuathiri amani na utulivu wetu na zaidi kuhakikisha kwamba tunanufaika nao ni weledi ambao hatunao kiasi cha kutosha.

  Kuwa na orodha ya faida za mfumo wa vyama vingi ambazo mwisho wa siku tunaziona zikipepeluka kama njiwa haisaidii kitu, kwa mfano angalia mchakato wa kujadili bajeti unaoendelea bungeni, vyama vyote viwili vimechukua extreme positions.

  Wabunge wa CHADEMA wanasema Bajeti ya Mgimwa iondolewe bungeni, maana yake hawaoni point hata moja
  Wabunge wa CCM wanasema Bajeti ya Zitto ni Rabish.

  where will they meet, na hakuna dalili za utayari wa kukubaliana kufikia makubaliano japo kwa kubuy points kutoka pande zote, mwisho wa siku kura zitapigwa budget utapitishwa na wananchi tutabaki kushangaa kwamba ni nini hasa kilikuwa kinaendelea pale.

  Kwamba vyama vya upinzani vinaisimamia serikali, we unaona dalili yoyote ya CCM kukubaliana na hili?
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Walioko Chadema wataendelea Vizuri kuwa wananchi; Walio CCM Mmmm hatari hawata weza, Wamezoea Madaraka

  Wamezoea Ubwanyenye, Ubabe, Mfano Lau Masha kaondolewa Uwaziri lakini UCCM bado unamlinda, haendi kazini kila

  Siku kazi yake anaifanyia Bar; CCM imempa kila kitu hana Shida... Sasa utaniambia Riz1 atarukaruka Mjini bila CCM? Hao

  Vidada Vyote Wabunge wa CCM watakula wapi? Hiyo ni hatari kwa CCM utaleta JANGA LA TAIFA
   
 8. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,010
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Uzuri wa demokrasia ni kuwa wakati ukitimia wananchi ndio watakuwa na mamlaka na uwezo wa kuamua. Bila ya kuwa na vyama vya upinzani itakuwa vigumu kwa wananchi kufanya hivyo.
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  SANGARARA,

  kama ni maneno yaliyotoka rohoni wakati avatar yako ina picha ya Dk. Slaa ni wazo jema.

  Utakubali kupoteza huyo kipenzi chako na chama chake.??????
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Sijasema tuwazue viongozi wa vyama vya siasa kufanya shughuli za kisiasa, hiyo ni haki yao ya msingi kabisa, lakini vyama hivi viwili vifutwe kama DR SLAA ataenda CUF au vipi hayo ni mambo mengine, cha msingi tutapata fursa ya kukaa na kuanza kufikiria mambo ya kitaifa kuanzia point moja na sio kama ilivyo sasa.
   
 11. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo wewe unaona kwamba wakati pekee wananchi wanastahili kushiriki actively kwenye mchakato wa kimaamuzi kwenye mfumo wa vyama vingi ni wakati wa kupiga kura tu?

  Umeniongezea sababu ya kuamini kwenye ulazima wa kufuta hivi vyama.
   
 12. s

  sawabho JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Jifunze kwanza maana ya vyama vya siasas na umuhimu wa vyama vya upinzani. Bila migongano kama hiyo, hakuna maendeleo, maana hakuna wa kumkosoa mwenzake, wote ni NDIO MZEE.
   
 13. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Sasa Kinachoendelea Bungeni ni Migongano au Mifarakano? hawakubalini kwa kitu chochote kile alafu wewe unasema wanagongana? kweli?
   
 14. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  mkuu lini uchaguzi ulifanyika urambo.? Alafu hoja yako ni dhaifu sana na inaelekea siku hizi umeshakuwa gamba ww.
   
 15. s

  sawabho JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Ni kweli yanayoendelee Bungeni yanaweza kuwa sio mazuri kwa jamii kwa sababu Jamii hiyo imelelewa katika hali ya kutopinga kitu cho chote hata kama kinaleta madhara kwao, watakwambia wanamwachia Mungu. Swala la kungalia hapa ni kwamba kwa nini kuna hiyo mifarakano ? Ni nini chanzo chake, je ni maslahi ya Umma, chama au mtu binafsi. Ukiona Mbunge anayetetea maslahi yake binafsi, chama au kikundi fulani ujue huyo ndiye chanzo cha mifarakano kwa faida ya wachache. Lakini kama anatetea maslahi ya Umma, ujue ana haki ya kuanzisha huo mfarakano. Lakini nikukumbushe kitu kimoja, Umma wa Watzania unaenda unabadilika, miaka ya nyuma hakuna mtu angeweza kumsema vibaya Kiongozi wa nchi, viongozi wa nchi waliheshimiwa au kuogopwa sana, akitembelea sehemu maduka yanafungwa !!!! Ina maana kuna kitu kimeenda vibaya miaka ya hivi karibuni. Hakuna nidhamu ya uoga, watu wamekuwa wakweli na kuhoji mambo ya nchi, sasa inabidi viongozi wawe tayari kutoa uafafanuzi bila kutumia nguvu, matumizi ya nguvu yanajenga uadui miongoni mwa Serikali na Wananchi wake. watu wametawanyika sana, unaweza kuwa unaishi Bukoba, lakini matumizi ya nguvu yakifanyika Tanga, yanakuadhiri maana kuna ndugu yako huko au kwingineko.
   
 16. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Mkuu,ni lazima ukumbuke kuwa hata ccm na cdm vikifutwa,bado vitaibuka vyma vingine.Ninachoona mimi ni Ccm imeshindwa kujibu hoja nzito zinaz6 ibuliwa na cdm na matokeo yake ni kutumia matusi nk.
  Hata hivyo,ushindani huu wa kisiasa una matokeo chanya!
  Kumbuka katiba mpya,vita dhidi ya ufisadi hazikuwa ajenda za ccm bali wameiga cdm.
   
 17. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Mkuu, unaweza ukaderive point yako kutokea kwenye mfano wa familia ambayo wote wawili, baba na mama wanataka agenda zao binafsi ndio ziwe muongozo wa kuendesha familia? Be sincere please.
   
 18. S

  SAGANKA JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 9, 2012
  Messages: 313
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Unavyoongea unaonekana kuwa mbumbumbu wa siasa,au la basi umetumwa na mbatia.Lakini pia kwa mbali una ka-element ka kike kike,yaani ka uoga.Vyama vinafanya siasa,tangu mwaka 1995,tumekuwa na uchaguzi wa vyama vingi. Nyinyiemu mmekuwa mkishinda hadi mliposhindwa 2010 na kung'ang'ania.Lakini pia mmekuwa mkiwatisha wananchi mliowanyima elimu kwa muda mrefu sasa kuwa wakichagua upinzani wamechagua vita. Swali langu la msingi ni hivi,kwamba Cdm wakipewa ridhaa ya kuiongoza nchi wataanzisha vita ya nini?.Logically ni kwamba ccm ndio wako tayari kuanzisha vita kama watatolewa madarakani,na kama hawana nia hiyo basi wamewanyima wananchi elimu ili kila mara wawaendelee na hizo hoja legelege.Naomba nikwambie mwanzisha mada kuwa,huwezi kudanganya watu wote muda wote. Muda wa uongo wa ccm umefika mwisho,na siku ya kufa nyani,nyani mwenyewe huteleza na sio miti.Ccm wanateleza,cdm na wananchi tupo imara kipindi hiki.
   
 19. s

  sawabho JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa Baba na Mama ndio wenye familia hiyo, ni ruksa agenda zao za siri kuendesha familia yao, lakini haziwezi kutumika kuendesha familia nyingine kama vile ambavyo agenda za CHADEMA haziwezi kuendesha CCM na kinyume chake. Aidha, kama unaelewa ni kwa makusudi gani vyama vya upinzani vilianzishwa, huwezi kupendekeza kuwa vifutwe. Kumbuka vyama hivi vilianzishwa ili kukikosoa chama tawala chochote kiwacho na kutoa changamoto ili kiweze kuongoza vizuri kwa sababu kitakuwa na hofu kuwa kama kikifanya vibaya kitanyang'anywa madaraka. Kwa hiyo waliasisi mfumo wa vyama vingi walifahamu kuwa kutakuwepo na mitafaruku katika mfumo huu, na hiyo mitafaruku ndiyo chachu ya kujirekebisha na kuleta maendeleo. ZINGATIA WAJIBU WA VYAMA VYA UPINZANI.
   
 20. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Unakumbuka lakini kwamba, mfumo wa kuendesha nchi kwa miongozo ya vyama vya siasa ni mfumo mgeni sana hapa kwetu, of course ulianza baada ya kupata uhuru. unataka kusema kwamba jamii zote zilizokuwapo huko nyuma zilijiendesha vipi? akili zako zimefikia mwisho wa kufikiria kwa ufahamu kwamba mfumo wa vyama vingi unaleta changamoto kwa chama tawala sio? unajua kwamba record nzuri ya uongozi wa taifa hili tunayompa baba wa Taifa inatokana na kuongoza Taifa hili chini ya mfumo wa Chama Kimoja? think out of the box.
   
Loading...