Bashir Yakub
Member
- May 27, 2013
- 84
- 1,561
ANASA ZIMERUDI?
Bashir Yakub.
Ukumbi wa Mlimani City ukitengwa kwa watu 900 gharama ni Tshs 36,000,000/= bila chakula na vinywaji.
Gharama ya dawati moja zuri ni Tshs 80,000/=. Kwa Tshs. 36,000,000/= tunapata dawati 450,000.
Kwa dawati linalokaliwa na wanafunzi wawili jumla ya wanafunzi 225,000 wanakuwa wamepata sehemu nzuri ya kukaa na kupata maarifa.
Unaweza kutafuta mfano mwingine kwa fedha hiyo M.36.
Ikulu ya Magogoni upo ukumbi mkubwa hauna kazi leo. Kadhalika Ikulu ya Chamwino, Dodoma ambako nako wapo wazee, upo ukumbi mkubwa, mpya, na mzuri.
Kabla sijasahau ukumbi wa Serikali wa Mwalim Nyerere Mtaa wa Shaban Robert uliojengwa kwa USD 15 Milioni wenye uwezo wa kukalisha watu zaidi ya 1000, ndani ya ekari 6.2.
Achana na Karimjee na kumbi nyingine nyingi zilizo kila pahala kwenye Maghorofa ya Wizara zilizohamia Dodoma.
Bajeti yetu ya 2020/2021 Trilioni 12.8 ambayo ni asilimia 37 tu ya bajeti yote ndo ilienda kwenye miradi ya maendeleo. Asilimia 63 ya fedha iliyobaki ni MATUMIZI.
Kuna haja ya kuulizana tena kwanini fedha nyingi huingia kwenye matumizi kuliko miradi ya maendeleo.
Kupanga ni kuchagua.