Uchaguzi 2020 Kuna haja ya kutoipigia kura CCM ili kuwafundisha kuwa hatutaki ubaguzi wa Vyama kwa Viongozi

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,153
Hii nchi toka imepata Uhuru hakujawahi kuwepo na ubaguzi wa maendeleo kisa tu upande ule unakaa ukoo Fulani, au upande ule kuna kabila Fulani au kuna upinzani.

Enzi za Nyerere aliwai pata mbunge wa upinzani pekee akiitwa Sarwatt lakini hata siku moja hakusikika mwl Nyerere akiwananga wananchi wa kule kisa wamemchagua mpinzani.

Hela inayoleta maendeleo inatokana na kodi ya wananchi wote hivyo kubagua baadhi ya sehemu ni kinyume kabisa na ustawi wa nchi. Hivyo basi kwa umoja wetu Tanzania nzima kuna haja ya kutoichagua kabisa CCM ili hata wakiiba kura ya uraisi wakose mahali pa kupeleka hayo maendeleo maana wao si wanaangalia sehemu zao tu wakati kodi tunalipa wote.

Imekua kasumba kila anapopita hata kama wameweka mgombea mbaya ambae hakubaliki wanalazimisha achaguliwe kwa kutishia eti watawanyima maendeleo, kwani Dodoma kwenye Hospital ya vichaa Mirembe si ndo Mkoa mzima una wabunge wa CCM je ina maana umeshajitosheleza kwa maendeleo.

Shimeshime huu ni wakati kwa umoja wetu kukataa ubaguzi wa aina yoyote ule katika taifa letu kwa kuonesha kwa vitendo.
 
Je, ulitegemea Lissu atasema pigia kura Magufuli ? tujaribu kuweka uzi ambao utatutofautishisha Jamii Forum na Face book
Serikali hufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo kupitia mapato yake. Ukiachana na mapato ya nje (mikopo, misaada, etc), mapato ya ndani hutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi maeneo mbalimbali bila kujali mbunge au diwani wa eneo hilo anatoka Chama gani.

Bunda Kuna wafanyakazi wanakatwa PAYE, Kuna wafanyabiashara wanalipa Kodi, etc. Sio sahihi kuacha kupeleka Maendeleo kisa tu hawakuchagua mbunge wa CCM.

Huyu jamaa yetu ndio muumini mkubwa wa Msemo wa "Maendeleo Hayana Vyama". Ni wazi maneno haya huanzia tu kwenye mdomo na kuelekea nje, hayako kabisa moyoni.

Watu wa aina yako ndio sababu members wengi humu sio Great Thinker anymore.
 
Back
Top Bottom