Kuna haja ya kurudisha Tanzania Housing Bank (THB) na kuichukua CRDB iwe ya Serikali kwa 100%

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,853
141,776
CRDB ilikuwa Bank ya serikali lakini ikabinafsishwa GM akiwa huyo Kimei au John Rubambe sikumbuki vizuri

Tulikuwa pia na Benki ya Nyumba THB, Benki ya Posta TPB, Benki ya Rasilimali TIB, Benki ya Biashara NBC na Benki Kuu BoT

Mwigullu Nchemba hebu turejeshee THB tafadhali

Na wewe Bashe acha kulia lia CRDB ni Benki ya serikali na kirefu chake ni Cooperative and Rural Development Bank sass inataka kuanzisha Benki nyingine ya nini?

Mungu anawaona mjue
 
Ilikirudi serikalini inakufa kifo cha mende. Taasisi nyingi za serikali ziko hoi.

Nida wakishakupa namba ndiyo basi tena kitambulisho hupewi. Pale kumejaa vidada unaenda kama havikuoni viko busy vinapiga story tu kuhusu mabwana na waume zao.

Yani sijui aliyeturoga nani. Nadhani mfumo unaowalinda watumishi wa umma uanchangia wao kuwa wavuvi kazini.
 
Mkuu, Cooperative and Rural Development Bank ilikufa, CRDB Bank (1996) Ltd ambayo ilijibadili na kuwa CRDB Bank PlC alipandia na kudesa vizuri CRDB ya zamani ilikuwa ni bank ya ushirika na maendeleo vijijini.

Hii CRDB ya sasa ni commercial bank na haina element zozote za ilikuwa CRDB ya enzi ya Nyerere.

Hapa tuanze upya kwa kurejesha bank ya Nyumba ikiwamo kuwarudishia assets zao za majengo na wapewe mtaji ili kujenga nyumba na wazo za Bashe lisipigwe nyundo bali liboreshwe.
 
Mara CRDB ilibinaifishwa halafu tena mara ni bank ya serikali, sasa tukuelewe vipi?

Anyway, siungi mkono hii bank kuchukuliwa na serikali mana itakuwa ya hovyo kama baadhi ya mashirika mengine ya kiserikali.
 
Ubinafsishaji uko wa aina mbalimbali bwashee

Hata Simba SC imebinafsishwa
 
Mkuu, Cooperative and Rural Development Bank ilikufa, CRDB Bank (1996) Ltd ambayo ilijibadili na kuwa CRDB Bank PlC alipandia na kudesa vizuri CRDB ya zamani ilikuwa ni bank ya ushirika na maendeleo vijijini.

Hii CRDB ya sasa ni commercial bank na haina element zozote za ilikuwa CRDB ya enzi ya Nyerere.

Hapa tuanze upya kwa kurejesha bank ya Nyumba ikiwamo kuwarudishia assets zao za majengo na wapewe mtaji ili kujenga nyumba na wazo za Bashe lisipigwe nyundo bali liboreshwe.
Kama Ilikufa mbona serikali ina Hisa zake pale CRDB

Wengi waliamini kama wewe lakini Mzalendo namba 2 hayati Magufuli akatufumbua macho
 
Ilikirudi serikalini inakufa kifo cha mende. Taasisi nyingi za serikali ziko hoi.

Nida wakishakupa namba ndiyo basi tena kitambulisho hupewi. Pale kumejaa vidada unaenda kama havikuoni viko busy vinapiga story tu kuhusu mabwana na waume zao.

Yani sijui aliyeturoga nani. Nadhani mfumo unaowalinda watumishi wa umma uanchangia wao kuwa wavuvi kazini.
Watanzania hapa ndipo tunapofeli, ajira ziwe za mkataba, usipofanya vizuri, kibarua kinaota nyasi! serikali inahofu gani angali sasa wapo wahitimu wengi?
 
Ilikirudi serikalini inakufa kifo cha mende. Taasisi nyingi za serikali ziko hoi.

Nida wakishakupa namba ndiyo basi tena kitambulisho hupewi. Pale kumejaa vidada unaenda kama havikuoni viko busy vinapiga story tu kuhusu mabwana na waume zao.

Yani sijui aliyeturoga nani. Nadhani mfumo unaowalinda watumishi wa umma uanchangia wao kuwa wavuvi kazini.
Watanzania tunapenda Tarabu mno kuliko kazi, mchina wakati anajenga Tazara, alikuwa na msemo wake"wala wala minga kazi hamne" aliona hilo. Kwenye majukwaa ni hodari mno, njoo utekelezaji ni minus zero.
 
Mfumo ya ujamaa, kwamba kinachopatikana tugawane anayejituma na mvivu wote wapewe sawa ili pasiwe na gap la kiuchumi.
 
Watanzania tunapenda Tarabu mno kuliko kazi, mchina wakati anajenga Tazara, alikuwa na msemo wake"wala wala minga kazi hamne" aliona hilo. Kwenye majukwaa ni hodari mno, njoo utekelezaji ni minus zero.
Sasa kama wakuu wa nchi ni taarabu kwenda mbele na sisi ni kina nani basi tusionje kilichomo ndani yakhe. Akija mpindua meza na kuweka kazi kazi majungu kama yote.
 
Kama Ilikufa mbona serikali ina Hisa zake pale CRDB

Wengi waliamini kama wewe lakini Mzalendo namba 2 hayati Magufuli akatufumbua macho

soma hapo juu.'

Nimekulia Mwanza nikiiona Cooperative & Rural Development bank inakufa hivihivi. Kama hisa zake zilichulikuwa, inaweza kuwa kuna namna zilihamishiwa CRDB 1996 Ltd na wakahama kwenye core buz ya bank ya ushirika na sasa wanafanya biashara kama bank zingine.

Kumbuka hata NBC (National Bank of Commerce ambae ni baba/mama wa NMB) ilikuwa bank ya umma, ila kilichofanyika Nyerere akiwepo alishangaa na mpaka leo imebakia historia.
 
Mkuu, Cooperative and Rural Development Bank ilikufa, CRDB Bank (1996) Ltd ambayo ilijibadili na kuwa CRDB Bank PlC alipandia na kudesa vizuri CRDB ya zamani ilikuwa ni bank ya ushirika na maendeleo vijijini.

Hii CRDB ya sasa ni commercial bank na haina element zozote za ilikuwa CRDB ya enzi ya Nyerere.

Hapa tuanze upya kwa kurejesha bank ya Nyumba ikiwamo kuwarudishia assets zao za majengo na wapewe mtaji ili kujenga nyumba na wazo za Bashe lisipigwe nyundo bali liboreshwe.

Uko sahihi kabisa. Kubakiza “CRDB” katika jina ni PR strategy na huenda neno hilo sio tena abbreviations za “cooperative n rural development bank” tena nimuundo wala kiutendaji!!

Kuna tabia ya wivu ndani ya watu wengi. Wanataka kuichukua kwa kuwa inafanya vizuri. Sawa na uswahilini mtu kaona kuku mgeni wa jirani na anakua ni wa kuchinjwa soon, anachukua gongo na kumtupia yule kuku kutaka kumuua ati kwa kunya nyumbani kwa mtu au kula mahindi yaloanikwa.

Tukitaka benki ya nyumba - tuanzishe benki mpya ya nyumba. Basi!!
 
Mfumo wa Bank zote zilizobinafsishwa zilibaki na majina yao ya zamani ingawa shughuli zinazofanywa na bank hizo kwa hivi sasa hazifanani na majina yao
Na hilo utaliona kwa CRDB, NMB, NBC na nyingine Sababu kubwa ni kulinda jina (to maintain Goodwill)
Ni vzuri kufahamu kuwa wakati haya Mabank yanauzwa/yanabinafsishwa wakati wanapiga mahesabu ya mali zinazouzwa na Majina nayo yalikuwa yanauzwa
 
Back
Top Bottom