Hivi karibuni Rais ametangaza baraza la mawaziri ambalo binafsi mimi naona kwamba ni kubwa sana na litakuwa mzigo kwa sisi walipa kodi wa nchi hii.
Kuna baadhi ya wizara zinapaswa kuunganishwa ili kuwapunguzia mzigo wananchi, maana mawaziri hawa watahudumiwa na kodi za wananchi, mathalani zipo wizara ambazo zinapaswa kuunganishwa na kuunda wizara moja maana kimajukumu zinaendana na kuingiliana.
Mfano:
1. Wizara ya Viwanda na Biashara na ile ya uwekezaji inapaswa kuwa moja maana wawekezaji ndio hao hao wafanyabiashara na wanaokuja kufungua viwanda.
2. Wizara ya Habari na ile ya mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, hapa wizara inapaswa kubaki moja ambayo ni wizara ya Habari na sio vinginevyo.
3. TAMISEMI na Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala bora zinapaswa kuwa wizara moja.
4. Maliasili na Utalii iunganishwe na Madini, maana madini nayo ni maliasili.
5. Nishati na Maji iwe wizara moja
6. Kilimo, Mifugo na Uvuvi iwe wizara moja
7. Ulinzi na Mambo ya Ndani iunganishwe iundwe Wizara ya ulinzi na Usalama wa Raia.
8.Wizara ya sheria na katiba iunganishwe na ile ya muuungano pamoja na bunge.
9.Wizara ya afya, maendeleo ya jamii na watu wenye mahitaji maalumu ambao ni walemavu, vijana, wanawake na watoto kwa mantiki hii tutakuwa tumevunja wizara Sera, bunge, Vijana na ajira.