Kuna haja ya kupunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri

Hivi karibuni Rais ametangaza baraza la mawaziri ambalo binafsi mimi naona kwamba ni kubwa sana na litakuwa mzigo kwa sisi walipa kodi wa nchi hii.

Kuna baadhi ya wizara zinapaswa kuunganishwa ili kuwapunguzia mzigo wananchi, maana mawaziri hawa watahudumiwa na kodi za wananchi, mathalani zipo wizara ambazo zinapaswa kuunganishwa na kuunda wizara moja maana kimajukumu zinaendana na kuingiliana.

Mfano

1. Wizara ya Viwanda na Biashara na ile ya uwekezaji inapaswa kuwa moja maana wawekezaji ndio hao hao wafanyabiashara na wanaokuja kufungua viwanda.

2. Wizara ya Habari na ile ya mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, hapa wizara inapaswa kubaki moja ambayo ni wizara ya Habari na sio vinginevyo.

3. TAMISEMI na Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala bora zinapaswa kuwa wizara moja.

4. Maliasili na Utalii iunganishwe na Madini, maana madini nayo ni maliasili.

5.Nishati na Maji iwe wizara moja

6. Kilimo, Mifugo na Uvuvi iwe wizara moja

7. Ulinzi na Mambo ya Ndani iunganishwe iundwe Wizara ya ulinzi na Usalama wa Raia.

8.
Ndivyo alivyokuwa ameshauriwa Lissu na Amsterdam? Ahahahahahahah!
 
Likipunguzwa tutalipana vipi fadhila?. Mi nafikiri liongezwe na nafasi mbalimbali serikalini ziongezwe, mf; mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, wawe na wasaidizi, wabunge wote wa kuchaguliwa wawe na wabunge wawili wa viti maalumu, hili kila mtu alikipigani chama kikapata ushindi wa kishindo apate nafasi.
 
Hivi karibuni Rais ametangaza baraza la mawaziri ambalo binafsi mimi naona kwamba ni kubwa sana na litakuwa mzigo kwa sisi walipa kodi wa nchi hii.

Kuna baadhi ya wizara zinapaswa kuunganishwa ili kuwapunguzia mzigo wananchi, maana mawaziri hawa watahudumiwa na kodi za wananchi, mathalani zipo wizara ambazo zinapaswa kuunganishwa na kuunda wizara moja maana kimajukumu zinaendana na kuingiliana.

Mfano

1. Wizara ya Viwanda na Biashara na ile ya uwekezaji inapaswa kuwa moja maana wawekezaji ndio hao hao wafanyabiashara na wanaokuja kufungua viwanda.

2. Wizara ya Habari na ile ya mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, hapa wizara inapaswa kubaki moja ambayo ni wizara ya Habari na sio vinginevyo.

3. TAMISEMI na Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala bora zinapaswa kuwa wizara moja.

4. Maliasili na Utalii iunganishwe na Madini, maana madini nayo ni maliasili.

5.Nishati na Maji iwe wizara moja

6. Kilimo, Mifugo na Uvuvi iwe wizara moja

7. Ulinzi na Mambo ya Ndani iunganishwe iundwe Wizara ya ulinzi na Usalama wa Raia.

8.
Mkuu mbona unalisema lilwhi kufanyika na uzoefu unaonyesha kuwa wazo lako halitekelezeki
 
Back
Top Bottom