Kuna haja ya kupunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,332
2,000
Hivi karibuni Rais ametangaza baraza la mawaziri ambalo binafsi mimi naona kwamba ni kubwa sana na litakuwa mzigo kwa sisi walipa kodi wa nchi hii.

Kuna baadhi ya wizara zinapaswa kuunganishwa ili kuwapunguzia mzigo wananchi, maana mawaziri hawa watahudumiwa na kodi za wananchi, mathalani zipo wizara ambazo zinapaswa kuunganishwa na kuunda wizara moja maana kimajukumu zinaendana na kuingiliana.

Mfano:
1. Wizara ya Viwanda na Biashara na ile ya uwekezaji inapaswa kuwa moja maana wawekezaji ndio hao hao wafanyabiashara na wanaokuja kufungua viwanda.

2. Wizara ya Habari na ile ya mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, hapa wizara inapaswa kubaki moja ambayo ni wizara ya Habari na sio vinginevyo.

3. TAMISEMI na Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala bora zinapaswa kuwa wizara moja.

4. Maliasili na Utalii iunganishwe na Madini, maana madini nayo ni maliasili.

5. Nishati na Maji iwe wizara moja

6. Kilimo, Mifugo na Uvuvi iwe wizara moja

7. Ulinzi na Mambo ya Ndani iunganishwe iundwe Wizara ya ulinzi na Usalama wa Raia.

8.Wizara ya sheria na katiba iunganishwe na ile ya muuungano pamoja na bunge.

9.Wizara ya afya, maendeleo ya jamii na watu wenye mahitaji maalumu ambao ni walemavu, vijana, wanawake na watoto kwa mantiki hii tutakuwa tumevunja wizara Sera, bunge, Vijana na ajira.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
38,313
2,000
Sio mawaziri kuwa wengi tu, hata viti maalum havina tija yoyote zaidi ya kula hela za wananchi bila sababu ya msingi, japo ni ulaji wa kisheria.
 
Mwaikibaki

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
1,970
2,000
Hivi katiba ikiwa inaeleza wazi muundo wa serikali hasa wizara si itaondoa issue kama hizi? Maana wizara zingine ukiangalia scope yake hata huelewi rationale ya kua nayo sanasana unaona iko kama idara tu..
 
Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,214
2,000
Duuh huu muhula wa mwisho mkuu kila mtu anatakiwa kula asee...
Mkuu nani kakwambia ndio muhula wa mwisho? ww ungejipanga kivyakowale wenye viherehere walizimwa kina Kangi, Mkamia, kessy.

sasa kina Kigwa, Mavunde Mpina, Makamba, Nnauye wameminywa sasa ujue mbele patamu na pachungu kwa watakaoguswa, njia shwariii
 
Mar 1, 2018
44
95
Mkuu nani kakwambia ndio muhula wa mwisho? ww ungejipanga kivyakowale wenye viherehere walizimwa kina Kangi, Mkamia, kessy
sasa kina Kigwa, Mavunde Mpina, Makamba, Nnauye wameminywa sasa ujue mbele patamu na pachungu kwa watakaoguswa, njia shwariii
Dooh! but meko alisema mwenyewe kuwa ndio mwisho!!
Au ndio tusiwaamini hawa watu?
 
Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
5,858
2,000
Tatozo la kuweka idara nyingi kwenye wizara moja ni kupunguwa kwa ufanisi. Waziri mmoja hawezi kujigawa kwenye majukumu mingi na ukategemea kula kitu kitakwenda sawa. Mara kwenye utali, mara kwenye maliasili, mara kwenye madini, lazima kimoja kitakosa umakini na kuharibika.
 
ofisa

JF-Expert Member
May 15, 2011
2,709
2,000
Sikuona haja ya TAL kukimbia nchi aliahidiwa kazi na Rais.

Kweli mabeberu wamevishika vichwa vya baadhi ya watu.hapakuwa na ishara yoyote ile ya kufanyiwa hujuma wala nini.
Au atarudi akisikia DPP amemfutia kesi zake zoote?

Nikiwa kama mtanzania sijaona sababu ya yeye kukimbia nchi.sisi tunajivunia kushiriki kuijenga nchi yetu. aje tu teuzi zipo nyingi Sana cha msingi tu aridhike na atakachopata.
 
Valuhwanoswela

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
1,057
2,000
Hivi karibuni Rais ametangaza baraza la mawaziri ambalo binafsi mimi naona kwamba ni kubwa sana na litakuwa mzigo kwa sisi walipa kodi wa nchi hii...
Mimi nafikiri Mawaziri mizigo ndo wanafanya Wizara zinazounda Serikali ziwe mizigo kwa wananchi walipa kodi kama ilivyo kwa Spika dhaifu amefanya Bunge linalotoa Mawaziri liwe dhaifu na kuwa mzigo kwa walipa kodi. Kuunganisha Wizara ni kuunganisha mizigo midogomidogo kuwa mizigo mikubwa mizito zaidi kwa walipa kodi!
 
Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,636
2,000
Hivi karibuni Rais ametangaza baraza la mawaziri ambalo binafsi mimi naona kwamba ni kubwa sana na litakuwa mzigo kwa sisi walipa kodi wa nchi hii.

Kuna baadhi ya wizara zinapaswa kuunganishwa ili kuwapunguzia mzigo wananchi, maana mawaziri hawa watahudumiwa na kodi za wananchi, mathalani zipo wizara ambazo zinapaswa kuunganishwa na kuunda wizara moja maana kimajukumu zinaendana na kuingiliana.

Mfano

1. Wizara ya Viwanda na Biashara na ile ya uwekezaji inapaswa kuwa moja maana wawekezaji ndio hao hao wafanyabiashara na wanaokuja kufungua viwanda.

2. Wizara ya Habari na ile ya mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, hapa wizara inapaswa kubaki moja ambayo ni wizara ya Habari na sio vinginevyo.

3. TAMISEMI na Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala bora zinapaswa kuwa wizara moja.

4. Maliasili na Utalii iunganishwe na Madini, maana madini nayo ni maliasili.

5.Nishati na Maji iwe wizara moja

6. Kilimo, Mifugo na Uvuvi iwe wizara moja

7. Ulinzi na Mambo ya Ndani iunganishwe iundwe Wizara ya ulinzi na Usalama wa Raia.

8.
Mimi ushauli wangu ni kama ifuatavyo:

Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira ivunjwe

Kipande cha mazingira kikaunganishwe na wizara ya maliasili na utalii, then wizara mpya ijulikane kama ifuatavyo; Wizara ya Maliasili, Utalii & hifadhi ya mazingira.
Kwa maana utalii na hifadhi ya mazingira kuna kuoana

Na kipande cha muungano kikaunganishwe na wizara ya katiba na sheria, then wizara mpya ijulikane kama ifuatavyo; Wizara ya Katiba, Sheria & Muungano.
Kwa maana muungano upo kikatiba katiba/ama kisheria sheria
 
Laury

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
986
1,000

Binafsi naona kama Rais kajirundikia mzigo wa Ofisi nyingi kitu ambacho inaweza kuwa ngumu kwa wasaidizi wake hasa Waziri Mkuu au Makamu wa Raisi kuwa na nguvu ya moja kwa moja kwenye hizi ofisi pale mambo yanapokuwa hayaendi sawa..

Me naona hizi wizara zingegawanywa baadhi kuwa kwenye ofisi ya Makamu wa Rais na Nyingine chini ya waziri Mkuu, kwa ajili ya usaidizi wenye tija kwa Rais
 
Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,308
2,000
Aisee mpaka naona aibu mimi;

Hiki ni nini??

Sidhani kama ulifikiri sawasawa kabla ya kupost.

Wenzako wamezitenga hizo wizara baada ya miaka kadhaa ya kuongoza serikali.

Sidhani kama unaijui TAMISEMI namna lilivyo dude kubwa. Halafu bado umuongezee mtu mzigo mwigine tena??

Kusema Habari na Mawasiliano ni kitu kimoja, sijui huu uongo umeutoa wapi.

Kiufupi umeandika mambo ambayo hayaleti maana kabisa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom