Kuna haja ya kupima UKIMWI kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna haja ya kupima UKIMWI kweli?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FisadiNyangumi, Jun 4, 2009.

 1. F

  FisadiNyangumi Member

  #1
  Jun 4, 2009
  Joined: May 4, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Suala la kupima UKIMWI linasemwa sana.

  Tunaambiwa Tanzania bila UKIMWI inawezekana, kwa kupima.

  Inakuwa kama kujua afya yako ni jambo la maana sana.


  Ukiangalia athari za kujua afya yako kulinganisha na faida, utaona jinsi ambavyo tendo hilo la kupima halina msaada mkubwa kama inavyosikika.


  Kuishi maisha ya kutokuwa na hakika na uwapo wa wadudu hao mwilini, hakuwezi kukuathiri kama pale unapokuwa unajua ubomoaji wa seli unaendelea mwilini. Ni rahisi kuanza kuugua kabla ya wakati, kitu ambacho
  kisingekuwapo kama ungesingejua.
  Faida iko wapi?

  Kujua kwamba tayari unaumwa, kunakushawishi kujinyanyapaa mwenyewe, na kuanza kuhisi kufakufa, jambo ambalo haliwezi kuelezeka kama faida.

  Ni kama unapokunywa maji yasiyochemshwa bila taarifa.
  Huumwi tumbo.

  Suala la kupima kimsingi halina maana zaidi ya kukusanya takwimu za wagonjwa nchini.

  Maoni ya Daktari mwanafunzi, Muhimbili. Asante sana!
   
 2. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2009
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Anyway hayo ni maoni yako. Ila Acha kudanganya watu! Ukimwi ni kitu kingine..
   
 3. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  Mkuu;

  Kwanza, Una nafasi nzuri ya kuboresha mwenendo wa maisha yako paele unapojua una Ukimwi au hauna.

  Swala la kupima huendana na Ushauri Nasaha ambao ni muhimu sana. Tatzo la Stigma, Msongo wa mawzo nk katika ukimwi ni la kisaikolojia zaidi kuliko kiafya. Kupima ni muhimu.

  Tafakari. Chukua hatua.
   
 4. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [quote
  Maoni ya Daktari mwanafunzi, Muhimbili. Asante sana![/quote]

  Kama haya ni mawazo ya daktari mtarajiwa, hii vita dhidi ya ukimwi haitaisha kwa mwendo huu. Uko kitengo cha dawa za miti shamba au?
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  1. Uki jua afya yako uta badili mfumo wa maisha yako kutokana na hali yako. Mfano kula vya kula vinavyo takiwa na kupumzika zaidi. Kubadili mfumo wa maisha uta kusaidia sana kurefusha maisha.

  2. Uta walinda wengine. Ukijua ume athirika hauta fanya ngono zembe na kuambukiza watu makusudi(kama una utu).

  3. Una weza kuanza kutumia dawa. Japo kuna wanao sema dawa zina madhara yake ila in the wrong run ni bora kutumia dawa kuliko kuto kutumia.

  4. Usicho kijua ni kama usiku wa giza. Ni bora kujua ukweli uchukue hatua madhubuti za kuku saidia.

   
 6. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,631
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Wakati mwingine kupima Ukimwi ni lazima.
  Mifano:
  -Umepata rafiki wa kike na mnataka muanze kula nyama kwa nyama
  -Unataka kwenda masomoni nje ya nje
  -unataka kufunga harusi

  Hata hivyo inatakiwa kupewa ushauri nasaha na kuandaliwa kisaikolojia katika hilo
   
 7. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  usiombe kupima ukimwi raha ila kusubiri majibu noma,huwa napima ukimwi nikiwa mjamzito only for my baby;otherwise sipimi ng'o!maana hata ukipima kama unao unao tu
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ndiyo hata ukipima kama unao unao lakini nia ya kupima si ilimradi tu. Mtu una pima ili ujue afya yako na uji tunze kutokana na maisha yako. Mtu yoyote mwenye ugonjwa fulani haswa wenye long term effects kama Ukimwi, Kisukari, ugonjwa wa moya nk huwa ni vizuri zaidi mtu ajue hali yako so as to adjust accordingly. It is a proven fact that the sooner you know you have HIV & start taking the right measures, the longer you can live. Kama mimi na my girl tuna pima every three months in fact I'm scheduled for one this month.
   
 9. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kwakweli haina haja.

  Nishapima mara ya kwanza 1996 majibu yakarudi -ve, nikapima tena 1998 majibu vile vile yakawa -ve, nikapima tena mwaka 2000 majibu yakarudi -ve, ...2007 nikacheki tena -hola! majuzi juzi nimecheki tena -hola!... sasa kuendelea kucheki kwa mara ya sita si itakuwa namtafuta Subhana wa Taala muhali, ee wajemeni?
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tatizo Ukimwi kama ugonjwa mwingine una weza ukaupata muda wowote hata upime mara ngapi na kwa miaka mingapi. Keep it up mzee bira upime mara kwa mara because you never know when you will be exposed. Au kama una mtu wako mna aminiana sana una weza kuachana na hiyo processya kupima.
   
 11. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  lol kama unatabia ya kufyonza damu za watu wengine kama wenye asili ya jina lako wee endelea kupima tu wala usichoke lol
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  This post made my day. Nime cheka mpaka basi.
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Jun 5, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  sijui kama umeshawahi kuona watoto waliozaliwa na ukimwi! utajiuliza kwa nini walizaliwa?? wazazi wao pengine walikuwa na mawazo kama wewe!

  [​IMG]
  [​IMG]


  angalia yatima hawa wazazi wao hwakujua wala kujitayarisha
  [​IMG]

  [​IMG]

  waafrika tumezoea sana maisha ya kujionyesha na kushindana, achilia mbali maisha ya kutoface-responsibility, thats why una
  wasiwasi ukijulikana ndio hivyo tena

  Pili mkuu UKIMWI SIO UGONJWA, NI UPUNGUFU WA KINGA MWILINI WATU WENYE UKIMWI WANAKUFA KWA MAGONJWA MENGINE MENGI AMBAYO MENGI YANATIBIKA!

  umefanya vyema kuuliza naamini utashiba, kama una wasi wasi basi ukipima na kukuta -OK inakupa motisha na faraja ya kubadili tabia , ukikuta unao mkuu sio ndio hali halisi??

  wenzako wanawaza kukinga wewe ndio haujikingi(mfano) unawaza usipime! umevuka hatua zote za usalama umesimama katikati ya reli unasema treni itasimama ikikuona, wakati usalama ni kuwa nje ya reli!

  KAMA UMEPIMA NA KUKUTA UNAO, IS GOOD TIME SIO KUFIGHT KWA AJILI YA AFYA YAKO TU, BALI YA WEWE NA WATOTO UTAKAOWAACHA, OFCOURSE HAUTAKUFA GHAFLA, UKIJITAYARISHA itakupa furaha sana.
   
Loading...