Kuna Haja ya Kumbadilisha DPP kwa ushaidi zaifu unaotia serikari hasara?

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Ukifatillia kwa makini utakuta kwamba wanasheria wengi wa kujitegemea wanashinda kesi nyingi sana zidi ya serikali na kuitia hasara mara mbili, pengine ukiangalia kiundani unaona ushahidi unajitosheleza kumtia mtu hatiani lakini , baadaye kunajitokeza mazingira tata, aidha wanasheria wote wa serikali ni matapeli wanakula rushwa na wanasheria wa kujitegemea au, wanasheria wa serikali bado wachanga sana katika sheria. Angalia kesi ya hivi karibuni ya Afande Zombe alivyoishinda kirahis mbali na ushahidi wa kweli wa kimazingira. Angalia kesi za mafisadi kama Liyumba kuaribu mamilioni na kufungwa miaka kiduchu. Inawezeka DPP wetu anakula cha juu na Majaji wetu wanaaribu ushahidi kwa kushirikiana na wanasheria wa Kujitegemea kufanya kesi iwe na mapungufu mengi ili mteja ashinde au apunguziwe adhabu. Kwa hali hii hatuna nchi maana mtu anaona aibe alafu wanasheria watalekebisha mambo. Zamani watu wa sheria walikuwa watu wa kawaida sana kwa kipato chao, kipato kilikuwa sawa na wahadhili wa vyuo , lakini sasa hivi hawashikiki baada ya hizi kesi za Ufisadi, Madawa ya Kulevya, Ubakaji na Wizi wa Mabenk. Nahsauri DPP ateuliwe kutoka kwenye jopo la mawakili watiifu wanaokubalika na wenye uwezo wa kujenga hoja na kukubalika.
 
Back
Top Bottom