Kuna haja ya kujua historia (background) ya mpenzi wako mpya?

yantuzu

Senior Member
Dec 10, 2011
115
16
Nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu kuhusu swala hili... kila mtu ana historia yake katika mapenzi.

Historia ninayoiongelea hapa ni ile ya mpenzi wako alishawahi kuwa na wapenzi wangapi kabla hajawa na wewe.

Kuna watunawajua historia zao si nzuri sana yaani unakuta mtu alishawahi kuwa na wapenzi kama 30 wa kiume /kike (mara nyingi wanaume wanakuwa na historia mbovu).

Sasa, kama mtu wa namna hii akipata mpenzi mpya kuna haja ya yeye kumweleza mpenzi wake kuhusu historia yake na asipomweleza akijua baadaye itakuweje?

Soma pia: Naomba Ushauri: Nimejikuta nimeoa mke aliyepitiwa na wengi
 
ili kiwe nini/we furahi penzi kwa nafasi yako,na umia katika hilo prnzi kwa nafasi yako!hao wengine sio wewe na wala hawana nafasi yoyyote katika kuboresha mahusiano uliyanayo na huyo mpenzi!
 
Ukimchunguza BATA hutomla asilini. Yanini kujihangaisha na yaliyopita? La mbolea hapo ni kuwashukuru hao waliopita kwa kutomchukua jumla jumla hadi na wewe ukabahatika kujivinjari nae!!! Mimi Mwanaume akiniuliza How many Guys have u dated before me? Baaaaaaaaas!!!!! Afterall the number is never true! Mtu akikwambia  amedate na 4 fanya 4*2=8 ujue hiyo ni 8 hapoo! Whats the point ya kuulizia kitu wakati unajua utapewa jibu FEKEROOOOOOO!
 
Hata wangekuwa mia..
Wewe unapompata mpenzi wako hesabu kuwa ni mpya..
Achana na habari za alikuwa na wangapi!..Haisadii sana kujua ya zamani!
 
ijue story yake kweli kwa kwenda angaza mengine ni kukitia mchanga kitumbua kipya.
 
Kama unahisi itakusaidia kitu katika mahusiano yenu,basi ni vyema kufahamu historia yake..ila kama unahisi itakusababishia maumivu wala usiulize hiyo background yake.
 
Kuna hawa mabinti ukikutana naye anataka umwelezee kila kitu kuhusu historia yako, sasa ugumu unakuwa kusema ukweli...maana ukimwambia ukweli lazima akutose hasa ukimtajia idadi, ukimdanganya baadaye akijua inakuwa balaa tena, naona inachanganya sana.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Kujua historia yake ni muhimu ili ujue uko na mtu wa aina gani, wengine wameshashindika hawafai mtini wala shimoni!
 
si kila mtu anataka historia....

Ila unapoelezoea unataja wawili wa mwishoni wengine unapotezea
 
Wasichana ndio wanapenda sana hizi ishu za kutaka kujua historia ya mvulana!!
 
Mtu aliyeshindikana mara nyingi hawezi kukwambia ukweli, dawa ni kuachana na historia kama wadau wanavyosema!!
 
Kwangu mie ALWAYS "Yaliyopita si ndwele" naona dhambi kumhesabia madudu yake ya nyuma, sometimes alikuwa HURT, hivyo kumdodosa saana anaweza akakuona na wewe ni wale wale.
 
Back
Top Bottom