Kuna haja ya kuitisha upya Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA tupate Mwenyekiti KIJANA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna haja ya kuitisha upya Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA tupate Mwenyekiti KIJANA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fuehrer, Jul 8, 2011.

 1. F

  Fuehrer Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama mtakumbuka Uchaguzi Mkuu wa cdm uliopita ulikuwa na mazengwe na kupelekea Chama kupoteza wanachama na viongozi mashuhuri. Binafsi sikupendezwa na hilo na hizi tetesi za manung'uniko miongoni mwa Wanachama zitapeleka cdm pabaya. Kuna watu wameaza kujenga imani eti Mwenyekiti wa cdm lazima awe mchagga.

  Mimi sioni kama Freeman Aikaeli ana mvuti (Charisma)wa kuwa kiongozi, na anarudisha nyuma jitihada za cdm kukamata dola.

  Bora uitishwe uchaguzi tupate kiongiozi makini.

  Kuna akina Zitto, Mnyika; tunang'ang'ania Mbowe wa nini? au zile fedha za urithi?
   
 2. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli, kwa utaratibu uliopo

  cdm = uchagga
  kama utakumbuka viti maalum, mbeya hawakupata, vingi wamepeana
  Zitto alilazimishwa kutoa jina lake kwa design alizolazimishwa Malecela ccm; au ndio wale wale ccm na cdm?
  vijana walifukuzwa
  Mbowe sio tu kuwa hana charisma, na eloquency yake ni contestable.

  MBOWE ANAIMALIZA cdm, aondoke
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Pilipili usiyokula inakuwasha namuna gani?- Jean Bosco Mwenda.
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mchange mla Rushwa hafai Chadema
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280

  Na sasa Prof Safari.
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Kingunge Ngombale Mwiru
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Chama kinachoenda hovyo ni chama changu ccm,na suggest tumpe kijana nape ili tuvutie vijana zaidi.
   
 8. M

  Marytina JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti kwa sababu ubabe na hulka zake zimeisaidia sana CDM
  zitto,mnyika wasubiri wakati wao utakuja.

  MBOWE NI KISIKI NAMBA 2 KWA CCM,yeye amewezesha CDM kutorubuniwa na mamluki wapenda pesa walio ndani ya chama
  mbowe endelea hivyohivyo.
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Jes,fai,ms mwaka 2015 atagombea mlutheri kupitia ccm sijui mtarudi cuf au mtamuunga mkono?tumeshindwa kuingoa bakwata sasa tunaifitini cdm!huoni cdm wamepinga mangapi kwa manufaa ya watz?eg suala sukari,epa pesa zimerudi kiasi na mengine mengi!MBOWE kafanya maendeleo makubwa sana ktk cdm na dhana ya vyama vya upinzani kwa jumla tanzania
   
 10. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  CDM ipo hapa ilipo kwa sababu ya uongozi wa sasa chini ya mkiti Mbowe, kama kuna mistake wanayoweza kuifanya CDM ni kumpa tu mtu yoyote uongozi wa hiki chama ilimradi demokrasia itimizwe. wapinzani wao wanaangalia wapi pa kupenyezea mamruki ili kuua chadema. Nadhani ndicho kinachoonekana hata kwa mleta thread hii.

  TUNAMWAMINI MBOWE KWA SABABU HAWEZI KUPOKEE PESA NA KUKISALITI CHAMA NA HII NDIYO MBINU YA MWISHO YA WAPINZANI HAWANA NYINGINE YA KUIMALIZA CHADEMA.

  Chama ni kama kampuni ni lazima wawepo watu wenye uchungu na wenye kusimamia vision ya chama ili kibaki focused.

  kama mtu ataonekana dictator kwa baadhi tu ya wananchama ili hali asilimia kubwa wanaunga mkono uongozi wake na matunda yake yanaonekana basi hayo yatakuwa ni majungu tu kama kawaida na wala watu wale hawafai kuwepo pale ni bora wakaondoka kuliko kuharibu chama.

  Watanzania sasa wanataka chama cha upinzani ambacho kitakuwa na msimamo usioyumba katika harakati hizi za kujikomboa. Kama chadema hawataliangalia hili na kubaki wakibadili badili uongozi ili tu kukidhi matakwa ya wachache hawataweza kuwaongoza watanzania kushinda vita iliyoko mbele yao. Kwa maoni ya wengi hapa uongozi wa chadema so far so good hakunahaja yakuanza mapambano ya ndani kwa ndani tena. Ni lazima kuwe na umoja ndani ya chadema kwanza ili kuweza kupmabana na adui yao waa nje.

  Nadhani siyo mbaya kama kuna mtu hayuko happy na uongozi wa sasa basi anaweza kupisha kwa manufaa ya waliowengi.
   
 11. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Huwezi kufundisha Chama makini nini Chakufanya huku wewe mwenyewe akili yako imejaa Tongo tongo.
   
 12. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wewe ni mwanachama wa cdm? kama ndio nafikiri unaijua historia yake japo kidogo ilikotoka ilipo sasa na mchango wa Mbowe kuifikisha hapo, nakushangaa na mawazo yako ya kimagamba kutaka kujipendekeza kwamba unapendekeza nani awe mkt wa cdm eti kwasababu ya ujana tu, nenda magamba wambie mzee msekwa aachie u mkamu mkt kwa vijana au nyie hamna vijana?
   
 13. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,322
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280

  Wewe dogo umeamka vibaya leo, naamini umeamua kuwa na siku mbaya. You don't have a strong point to support your post.
   
 14. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Crap
  Mwambie alikutuma hana akili. Mbowe anawasumbua sana. Walikuwa wapi mwaka 2000. Wasubiri tu Mbowe atamaliza muda wake. Waache uchu wa Madaraka, Waambie wamwangalie EL anavyoteseka kwa kuyataka madaraka.

  Mara wengine wanataka Uraisi, Mara wanataka uenyekiti wa CDM, mbona Memosi ni mwenyekiti, au Mtikila ni mwenyekiti hao wote hamwaoni ila Mbowe Tu.

  Mbowe amekitoa CDM kwenye hali mbaya sana mpaka kwenye ushindi wa kuwa chama kikubwa. Nitamheshimu sana, sio hawa vijana wanaotaka madaraka kwa ajili ya sifa. Na hawapati hata kamwe.

  Sifa ya kiongozi ni kufanya kazi kwa bidii na kuwa na uwezo wa kuwa firm kwenye maamuzi, asiyenunulika wala kutamani kununuliwa. Mbowe ni tunu na lulu ya CDM. Ndio kiongozi ambaye CCM wameshindwa kumlaghai na kumnunua. Wametumia mbinu zote kumdhalilisha na kutumia mashambuli ya ndani na nje ila wameshindwa. Hao wanao lilia kuwa wenyeviti wa CDM hawana nia njema kwani tayari wameshindwa test ya uvumilivu.
   
 15. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,322
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  Umeanzisha mada na kutoraka mapema, bora umeamua kufanya hivyo, maana ilishaanza kunyesha mvua za makombora!!!!!!!! usichokonoe siku nyingine kama huna ubavu wa kujibu hoja.
   
 16. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mbowe Kamanda wa Anga ni kiongozi makini na pia ni mbunifu kwani amevumbua Uniform ya Chama"COMBAT",ameleta msemo sahihi wa Chama "PEOPLES POWER",alivumbua Utumiaji wa usafiri wa Chopper kwenye Campaign na pia hata designing ya Public Address System Mafuso.
   
 17. F

  FUSO JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,867
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Mi naona tu deal kwanza na pending issues --- hii ya kuwavua magamba mapacha watatu tukiimaliza then tuje ile ya RADA na chenji yetu toka ughaibuni na lile la KAGODA na washiriki wake tuwaje. Baada ya hapo the tumalizie na hili la KATIBA mpya.

  Watanzania mbona tunapenda kulimbikiza mambo magumu then mnakimbilia mepesi mepesi? ni ugonjwa gani huu tulionao?
   
 18. Mkenazi

  Mkenazi Senior Member

  #18
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  MBOWE anafaa sana kwa kuthibiti mbinu ya CCM ya kuwarubuni viongozi wa upinzani kuhujumu chama. Ni mtu anayejua nini kifanyike ili chama kisonge mbele. Mrema aliipaisha NCCR halafu akiaiuwa, TLP nayo yeye ni mbunge pekee. Lakini chadema kinapaa sababu ya uongozi makini wa chadema chini ya F. Mbowe. Kutoka wabunge watano 2005-2010 to wabunge 48 2010-2015.

  Mtoa hoja labda kama anona ubaya wa Mbowe ni kuipandisha chati Chadema aseme - Kwa mwana CCM ni sahii kwani kawapunguzia Ruzuku kwa mwanamageuzi wa ukweli hawezisema baya kwa Mbowe labda awe na ajenda yake binafsi.

  Mtoa hoja inawezekana umeota usiku wa kuamkia leo nchi inaongozwa na chadema sasa unahaha.
   
 19. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #19
  Jul 8, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280

  waambie viongozi wako wajenge zahanati waache mashangingi.
   

  Attached Files:

 20. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Inaelekea hujatambua kwamba chama chochote cha siasa kinaongozwa na katiba ambayo ndio inayoelekeza ni lini mkutano mkuu unaitishwa kuchagua viongozi. Iwapo matokeo ya uchaguzi uliopita kwa sababu yeyote hayakukufurahisha si busara kutoa wito ambao unapingana na katiba na kwa sababu dhaifu kama ulizotoa. Ni ushauri tu iwapo kweli wewe ni mwanachama mkereketwa
   
Loading...