Kuna haja ya kuishaki serikali kutokana na mgomo wa madaktari uliopelekea vifo vingi?

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
Ndugu watanzania wenzangu na wakazi wote waoishi ndani ya Tanzania(KISIWA CHA AMANI)
Napenda kutoa dukuduku langu kama ifuatavyo.
Wote tunajua kwamba wiki chache nyuma ulitokea mgomo mkubwa wa madaktari nchi nzima,mgomo ambao ulitokana na serikali kupuuza matakwa ya "WANAFANI" hao kwa jeuri na kiburi,naikumbuka moja ya hotuba ya vitisho ya"MTOTO WA MKULIMA"kwamba daktari yeyote atakaye kaidi amri ya serikali ya kusitisha mgomo atakuwa amejifukuzisha kazi.Matokeo yake ni kwamba baada ya muda mfupi mkuu huyu alikula matapishi yake mwenyewe kwa kuwapigia magoti wataalamu hao.
Kama hiyo aitoshi mkuu wa nchi "aka"BABA FULANI"aliteta nao
ameahidi kwamba mgomo umekwisha na hautotokea tena.Sasa swali langu ni jee serikali au madaktari wanawajibika vipi kutokana na maafa makubwa yaliyotokana na mgomo huo???
Jee kuna haja ya kuishitaki serikali kutokana na maafa haya makubwa ya vifo vya wa tz au tuwashitaki madaktari kwa kuvunja na kwenda kinyume na kiapo???
Toeni mchango wa mawazo ili tuweze kuionyesha serikali kwamba tumechoka na manyanyaso.Wao Wamemwaga mboga sasa na sisi tumwage ugali.
 
Tutaanzia wapi?kama una info zozote namna ya kuanza mashitaka weka hapa.Maana kuna haja tena sana ya kuishitaki serikali kwa upuuzi walioufanya!
 
Sijui kama itawezekana maana mahakama nayo sijui kama itakuwa huru kiasi cha kuiwajibisha serikali. Labda tusubiri wanasheria wakija watatueleza.
 
Sijui kama itawezekana maana mahakama nayo sijui kama itakuwa huru kiasi cha kuiwajibisha serikali. Labda tusubiri wanasheria wakija watatueleza.
Poa mkuu!
Ngoja tuwasubili wanasheria waje hapa watufungulie milango.
 
Utaanzia wapi kuishitaki wakati mahakama yao iliamuru waganga waliogoma warudi kazini?

Sehemu pekee ya kuishitaki serikali ni kwenye court of public opinion na hata huko sidhani kama utafika mbali maana hisia yangu ni kwamba hata public opinion imegawanyika.
 
Mkuu mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
kwani who iz responsible na hivyo vifo???
Kwa upande wangu ni madokta, coz uhuru wako unapoishia, na wa mwenzako ndo unapoanzia!!!
So unapodai haki zako, usivunje za mwenzako (right 2 lyf)
 
Back
Top Bottom