Kuna haja ya kubadili muundo, mfumo na utendaji kazi wa vyombo vya ulinzi Tanzania

MeinKempf

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
11,094
7,218
Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali yanayohusiana na kuleta madhara , iwe kwa mtu , kikundi au taasisi kwa mfumo wa milipuko, kutekwa au kumwagiwa vitu kama tindikali na kadhalika.

Serikali yetu imekuwa na kauli za KUSHITUKIZA NA KUBAHATISHA, ambazo zinambatana na majibu ya DHAHANIA.

Mimi kwa mtizamo wangu naona kuna umuhimu wakubadili mfumo , muundo, utendaji kazi, sheria na kanuni za vyombo vyetu vya ulinzi ili tuweze pata maana sahihi ya ulinzi,ninapendekeza kuwa liundwe BARAZA LA USALAMA LA TAIFA litalokuwa na kazi ya kumshauri mkulu wa kaya namna ya kuendesha mfumo wa ulinzi.

Pia nasikitika kumuona waziri wa ulinzi ( vuai nahodha) aki relax kwenye mechi uwanja wa Taifa huku Taifa lina majanga ( kwanini asingeenda waziri/ naibu wa michezo au habari au wavijan kwenye mtanange huo au ndo ulinzi shirikishi??). Pamoja na makamu wa kaya kwenda unguja kushiriki bonanza la kukwea minazi na kutembelea kisima cha ajabu huku unguja, wakati huo huo kiranja mkuu wa sirikari mjengoni akiwa anazindua kitabu cha manyanya na mkulu wa kaya akiwa anapiga tizi na madogo wa sunderland. je hapo kuwajibika kiitifaki kukowapi kwa viongozi wetu au ndo kusema ilikwa weekend , au dno kusema itifaki inakuwepo kwenye maadhimisho ya kitaifa tu??na je hiyo ndo kusema kwamba j3 ndo siku rasmi ya kazi tu?

Tz idumu daima .
 
mkuu, wakati mlipoambiwa mtoe mawazo yenu kwenye tume ya mabadiliko ya katiba mlinyuti, sasa mnaanza kuweweseka. hata hivyo warioba amesaidia sana na tutoe ushirikiano stahiki ili katiba mpya ipatikane haraka
 
hapa ni tume huru ya kimahakama tu, baraza la usalama litakuwa chini ya rais wa c.c.m ambaye anajua fika matukio yote haya.
 
wamekwenda xaxa kwa sababu mpaka tukio linatokea wao (wabunge wa M4C) walikuwa mjengo idodomya kwa jili ya kikao cha bunge, hivyo waetokea huko na kwenda moja kwa moja kwenye eneo la tukio arusha , ila kwa nafasi za hao wengine niliowataja hapo juu ni aibu kubwa xana kwao kwani ilibidi waoneshe uwajibikaji wa haraka pia na kujali.
 
Back
Top Bottom