Kuna haja ya kuanzisha kampeni ya kususia miamala?

Kuna mengi ya kususia, pamoja na miamala, kuna kununua chochote kinachouzwa kwenye bus terminals ambako tumeambiwa lazima tununue chakula cha mama lishe, tutumie matoroli ya mizigo, tupande bajaji, pikipiki na daladala
 
Wadau mnaonaje tukaanza kampeni ya kususia kufanya miamala kwasababu ya gharama kupanda??
Ili iweje? Lengo ni nini, kwa faida ya nani?! Nchi ni yetu, maendeleo ni yetu, Tanzania itajengwa na wa Tanzania wenyewe. Ushauri acha kuhubiri mipango hasi na uchochezi kuwa mzalendo changia maendeleo ya Nchi. Je kufanya miamala kwa Dunia ya leo ni hiali , anasa au "necessity?".
 
Haina shida Mussa Azan a.k.a Zungu
 
Huwezi kususia kwani kwa zama hizi teknolojia ndio Mpango mzima, kamwe huwezi kuikwepa lazima ukutane nayo popote pale uendako. ni kama vile maji, usipo yanywa utayaoga tu, au kufulia, au kuchambia kamwe huwezi kukwepa lazima tutatumia teknolojia, hata babu yangu wa kijijini anatumia simu kutuma au kupokea pesa.

Usishindane na teknolojia utapasuka kabla hujaiva.
 
Nahisi hii nikampeni ya serikali kurudisha ujambazi kwa nguvu wanajua kabisa makato ya miamala yakiwa makubwa mtu ataona nibora atembee nakeshi mfukoni kohafia sasa hapo unategemea ninikitatokea.
 
Wadau mnaonaje tukaanza kampeni ya kususia kufanya miamala kwasababu ya gharama kupanda?
Acheni mama aupige mwingi mtazoea tu, aendelee kulazimisha tulipe kodi kujazia pale ambapo walipa kodi wakubwa wamekwepa maana anawarembulia macho.
 
Hapo tayari umesha changia mwanao au mtoto wa ndugu yako akapate elimu bora, pia umesaidia ndugu yako popote alipo apate huduma bora hospitalini.

Usijutie makato hayo, utafurahia huduma za afya, elimu na barabara.

Mjenga nchi ni mwananchi, tujenge nchi yetu.
 
Ili iweje? Lengo ni nini, kwa faida ya nani?! Nchi ni yetu, maendeleo ni yetu, Tanzania itajengwa na wa Tanzania wenyewe. Ushauri acha kuhubiri mipango hasi na uchochezi kuwa mzalendo changia maendeleo ya Nchi. Je kufanya miamala kwa Dunia ya leo ni hiali , anasa au "necessity?".
Imagine umebahatika kuugua UTI umempiga mziga mtu 20000 ununue azuma, genge la wanyang'anyi linachuku 1350 kwenye kutuma tu kwenye kutoa unapigwa ngeta 2810 muamala wa 20,000 kughalimu 4000+ ni dhuluma kubwa mno hapo lazima tutofautishe uzalendo na upimbi,
 
hii sasa ndio kampeni mpya ya chadema baada ya kuona katiba mpya imekuwa ndoto za mchana.
ila chadema inazidi kujichafua zaidi kisiasa kwa kuhamasisha mambo ambayo ni kinyume na uzalendo, hakuna anaye shawishika na uhuni huu .
 
Back
Top Bottom