Kuna haja ya DPP kuwaachia Mashekhe wa Uamsho na ikibidi iwashtaki tena baada ya upelelezi kukamilika

M

Mohamed Abubakar

JF-Expert Member
225
500
Mahakama imechukua hatua za makusudi kwa kutosikiliza kesi ambazo ushahidi wake haujakamilika, na kesi ambazo ushahidi wake umekamilika mahakama zitaendesha mashauri nayo kwa njia ya teleconference.

Hata hivyo kuna watumuhumiwa waliokaa rumande zaidi ya miaka nane ambapo ushahidi wa kesi zao haujakamilika na upelelezi hauendelei.

Watu hao wapo wengi mahabusu wakiwemo viongozi wa dini Uamsho.

Serikali inapaswa kuona huruma japo kidogo, watanzania hawana furaha kwa sheria hizi kandamizi; na ikitokea mashekhe hawa (Mungu apishe Mbali) kusikia kuwa viongozi hawa wamekufa kwa corona au sababu ingine yyt ile?

CCM itazidi kujipotezea haiba kwa jamii. Na ni maiti pekee ndizo zitakazoweza kukipigia kura kwenye changuzi unaofata. Wananchi na waumini tumechoshwa na mateso haya kwa mashekhe

Ni utoe ushauri wa bure...... Na ombi, mkijisia....

Mh JPM alitoa ushauri kwa DPP hivi karibuni na kwa mamlaka aliyonayo atoe misamaha kwa mahabusu na kuwafutia mashitaka. Ushauri huu wa Mh JPM ulikuwa nandhamira njema wa kupunguza mlundikano wa mahabusu magereza.

Basi nimkumbuse DPP kuwa atumie burasa alizojaaliwa na Mungu kuwaachia huru wote ambao jamii (public opinion) inaona watumumiwa hawajatendewa haki kwa kukaa kifungoni kwa kipindi chote hiki iwaachie huru.

If CCM inaamini itaweza kushinda uchaguzi ujao bila kuwategemea waumini wenza wa mashekhe hawa basi ushauri huu wanaweza kuuzarau.

M

mbingunikwetu

JF-Expert Member
6,808
2,000
Usilazimishe kuiingiza dini kwenye kesi hii. Hawa wako rumande kama watuhumiwa na si kama mashehe!! Ushehe wao hauhusiki Bali tuhuma serious za ugaidi ndizo zinazowahusu! Kwa hiyo sema watuhumiwa wa ugaidi waachiwe!!

Bila shaka tutakubaliana kuwa yote inayoyafanya serikali ni kwa nia njema. Unalala na kuamka ukiwa salama bila hofu kwa sababu serikali inatimiza majukumu yake. Ni vizuri tuksipa serikali nafasi ya kuendelea na kesi hii mpaka itakapojiridhisha kuwa zipi ni ngano na pumba ni zipi.

Bila shaka haujasahau shughuli ilivyokuwa kibiti na Rufiji! Tuhuma za ugaidi si za kuchukulia kivyepasi!! Tujizuie kuingilia mahakama katika jambo lolote hasa kwa tuhuma nzito kama ugaidi.

Vinginevyo na wewe uchukuliwe ukasaidie kukamilisha kesi kwa haraka kama unaamini una ushahidi utakaowezesha kuharakisha shauri hili.
 
Msingida

Msingida

JF-Expert Member
5,757
2,000
Ccm haitegemei ushindi kupitia sanduku ka kura pekee,hivyo ombi lako wanaweza "kuzarau"
 
  • Thanks
Reactions: R.K
Bome-e

Bome-e

JF-Expert Member
12,649
2,000
Usilazimishe kuiingiza dini kwenye kesi hii. Hawa wako rumande kama watuhumiwa na si kama mashehe!! Ushehe wao hauhusiki Bali tuhuma serious za ugaidi ndizo zinazowahusu! Kwa hiyo sema watuhumiwa wa ugaidi waachiwe!!
Bila shaka tutakubaliana kuwa yote inayoyafanya serikali ni kwa nia njema. Unalala na kuamka ukiwa salama bila hofu kwa sababu serikali inatimiza majukumu yake. Ni vizuri tuksipa serikali nafasi ya kuendelea na kesi hii mpaka itakapojiridhisha kuwa zipi ni ngano na pumba ni zipi. Bila shaka haujasahau shughuli ilivyokuwa kibiti na Rufiji! Tuhuma za ugaidi si za kuchukulia kivyepasi!! Tujizuie kuingilia mahakama katika jambo lolote hasa kwa tuhuma nzito kama ugaidi. Vinginevyo na wewe uchukuliwe ukasaidie kukamilisha kesi kwa haraka kama unaamini una ushahidi utakaowezesha kuharakisha shauri hili.
Ulikuwa na miaka mingapi tokea umeanza kusikia kesi ya hao mashekhe wa uamsho?
 
kirengased

kirengased

JF-Expert Member
3,659
2,000
Gaidi sio mtu wakuchukulia poa awe sheikh ama padre... tizama boko haram wanavyosumbua west Afrika ndani ya siku tano wameua watu (wanajeshi) laki na u-sheikh!! Watu milioni mbili wamekimbia makazi yao!!

Bora wakae huko watoke wamezeeka, wamarekani sio wajinga kutoa matrilioni kwa Cuba kuipata Guantanamo kukwepa wapigania haki uchwara ndani ya USA.
 
Karne

Karne

JF-Expert Member
3,926
2,000
Huu ni ushauri tu au "mkwara" Sheikh?

Hao mashekh hata wakinyongwa kabisa hakuna athari yoyote kwenye sanduku la kura bara labda visiwani.

Haohao waumini wenza ndo waliwakamata huko kwao na kutuletea huku wakiamini wanakwepa lawama,ni wanafiki tu wale.

Wawarudishe huko nchini kwao wakayamalize,si kuna mahakama kule.
 
Ni maneno yenye chembe za kiburi. Ni dalili za kulewa madaraka kwa wenye madaraka na wewe ukitumika kama mshenga. No aibu sana kuwa RAIA mwenzangu huwafikii wenye shida. Jaribu kujiweka upande wa wanaodai haki uone maumivu utakayoyapata. Ktk mazingira hawa wananchi yyt kwenye chembechembe za wema lazima ahisi kuna ounevu kama ville si udini unaowasumbua wale tuliowaamini na tukawaweka madarakani.

Ni maajabu tz kuwepo na sheria lkn ili ushitakiwe lzm uwe wa dini Fulani, na utakamatwa pasipo kuwa Na ushahidi.

Kesi kama hizi zilikuwa enzi makaburi dhidi ya watu weusi SA.

Na kina uncle tom kama nyie mlikuwa mkishabikia makaburu.

Ni aibu kwa taifa kama tz kuwa Na sheria za kibaguzi kama hizi. Na inakipunguzia chama kilichopo madarakani authority ya kuendelea kutawala.

We tuombe uhai tutashuhudilia wenyewe kwa mungu hawi upande wa wanaofanya dhuluma....
 
M

Mohamed Abubakar

JF-Expert Member
225
500
Gaidi sio mtu wakuchukulia poa awe sheikh ama padre... tizama boko haram wanavyosumbua west Afrika ndani ya siku tano wameua watu (wanajeshi) laki na u-sheikh!! Watu milioni mbili wamekimbia makazi yao!!
Bora wakae huko watoke wamezeeka, wamarekani sio wajinga kutoa matrilioni kwa Cuba kuipata Guantanamo kukwepa wapigania haki uchwara ndani ya USA.
Hakuna padre atakaekamatwa kwa sheria kama hizi nchini. haxiwahusu, ingawa ktk nchi zilizopitia machafuko mapadre walipatikana na hatia ya kutenda uovu, na wala siio mashekhe. Eg Rwanda.

Kwa nusu karne CCM imekuwa ikiwabagua na kuwakandamiza wanamchi wake, na kuwatesa, ikawatungia sheria kandamizi zilizowahusu wao pekee (ugaidi). Sasa hivi inawageukia Chadema na wanaharakati kuwapa kesi za kipekee (utakatakatishaji),

Sijui itashindaje kura ikiwa inatengeza uadui kwa RAIA wake wenyewe.

Ee mungu nipe uhai, yangu macho,
 
M

Mohamed Abubakar

JF-Expert Member
225
500
Huu ni ushauri tu au "mkwara" Sheikh?

Hao mashekh hata wakinyongwa kabisa hakuna athari yoyote kwenye sanduku la kura bara labda visiwani.

Haohao waumini wenza ndo waliwakamata huko kwao na kutuletea huku wakiamini wanakwepa lawama,ni wanafiki tu wale.

Wawarudishe huko nchini kwao wakayamalize,si kuna mahakama kule.
I swear, mashekhe nyuma yao kuwa maelfu ya wafuasi. Na kiburi si maungwana
 
kirengased

kirengased

JF-Expert Member
3,659
2,000
Mohamed Abubakar,
Viongozi wa dini Rwanda kibao walifungwa wengine waliachiwa baada ya kuombana msamaha na maridhiano.

Luna taarifa za vijana kadhaa kupelekwa somalia kujifunza ugaidi na mpaka masheikh hao kushikiliwa sio bure kunajambo haliposawa sasa kama hatujui walichofanya sirini tusiteteetetee hovyo mbona viongozi wa bakwata (walio karibu na prezoo) hawatetei?

Yawezekana kunamambo wameambiwa ila hawatakiwi kuyaweka hadharani. Dunia inamambo mazito hii ila hatujuani tuu,serikali inaona/inafahamu mengi tujifunze kuiamini na kutoilaumu kwa kilajambo
 
U

UHURU JR

JF-Expert Member
8,633
2,000
Hao wangekuwa viongozi wa kisiasa hasa upinzani Jf ingekuwa balaa ila kwa kuwa si viongozi wa kisiasa basi watu hawajali.
 
Robidinyo

Robidinyo

JF-Expert Member
1,929
2,000
Kwa Africa hii Utawatii vipi hawa Viongozi bila hizi Sheria kandamizi.
 
Karne

Karne

JF-Expert Member
3,926
2,000
I swear, mashekhe nyuma yao kuwa maelfu ya wafuasi. Na kiburi si maungwana
Hao wafuasi si wapo nyuma yao since 2012?

Haki itendeke ila hawana influence to that extent kwenye ballot box!

"Justice delayed is justice denied"
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

Platinum Member
35,671
2,000
If CCM inaamini itaweza kushinda uchaguzi ujao bila kuwategemea waumini wenza wa mashekhe hawa basi ushauri huu wanaweza kuuzarau.
Mkuu Maalim Mohammed Abubakar,
Naunga mkono hoja, tena isiwe kwa masheikh wa uamsho tuu bali mahabusu wote ambao uchunguzi wa kesi zao haujakamilika, na kuanzia sasa, polisi wasikamate watu kabla ya kukamilisha upepelezi. Mahakama isipokee kesi ambazo DPP hajakamilisha uchunguzi.

Ila pia ukiomba kitu wewe omba tuu usiweke conditionalities, kama CCM imeweza kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kishindo cha asilimia 99.9% huku hao masheikh wanaozea mahabusu, what differences will it make kwa uchaguzi Mkuu?.

P
 
M

Mohamed Abubakar

JF-Expert Member
225
500
Mohamed Abubakar,
Viongozi wa dini Rwanda kibao walifungwa wengine waliachiwa baada ya kuombana msamaha na maridhiano. Luna taarifa za vijana kadhaa kupelekwa somalia kujifunza ugaidi na mpaka masheikh hao kushikiliwa sio bure kunajambo haliposawa sasa kama hatujui walichofanya sirini tusiteteetetee hovyo mbona viongozi wa bakwata (walio karibu na prezoo) hawatetei? yawezekana kunamambo wameambiwa ila hawatakiwi kuyaweka hadharani. Dunia inamambo mazito hii ila hatujuani tuu,serikali inaona/inafahamu mengi tujifunze kuiamini na kutoilaumu kwa kilajambo
( Justice delayed is justice denied)
Jeshi la Polisi linamkamata mtu na kumuweka ndani na baada ya kelele nyingi kutoka kwa jamii, mtuhumiwa huandaliwa mashtaka. Jamhuri inamtuhumu na kumshtaki kwa makosa mbalimbali mazito yasiyodhaminika. Awamu ya NNE ilitumia makosa ya ugaidi kwa watesi wao. Naamini Mzee kikwete anaumizwa na maamuzi yake. Awamu hii inawabana wanaoneka ni maadui wa CCM kwa sheria ya (utakatishaji).

Sasa Baada ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani kesi hutajwa lakini kesi huahirishwa na mtuhumiwa anaambiwa hawezi kujibu lo lote kwa kuwa 'upelelezi unakuwa bado haujakamilika'! Kila inapofikia tarehe ya kesi kutajwa, waendesha mashtaka wa Serikali huiambia Mahakama kuwa kesi bado haijakamilika na Hakimu au Jaji hulazimika kuiahirisha tena kesi hadi tarehe nyingine.

Huo ndio unakuwa mwanzo wa mateso na kukomolewa kwa mtuhumiwa. Biashara zake na kazi zake huathiriwa vibaya sambamba na familia yake achilia mbali afya yake kuathiriwa akiwa mahabusu! Inaonekana katika nchi yetu, sisi sote tunakosa ujasiri wa kuhoji ukiritimba huu wa Sheria zetu unaochochewa na watendaji wenye husuda na roho mbaya wanaotumia mwanya wa vipengere kandamizi vya Sheria zetu na hivyo kuwatesa na kuwakomoa wale wasiopatana nao ndani na nje ya mfumo wa Serikali. Haki ye yote iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyokataliwa (justice delayed is justice denied).

Hivyo, kuchelewesha kusikiliza kesi za waliotuhumiwa huku wakiachwa kusota mahabusu ni sawa na kuwacheleweshea na kuwanyima haki yao. Kwa nini umkamate mtu na kumtuhumu na kisha kumshtaki lakini unamuweka mahabusu miezi na hata miaka kwa kisingizio cha upelelezi kutokukamilika katika zama hizi? Hivi ni kiongozi gani au mamlaka gani inayoweza kufidia hasara za mtuhumiwa aliyecheleweshewa haki hadi kuathirika na kupata magonjwa hadi kifo?

Mambo haya yanaumiza sana moyo wangu kwani kwa njia hii watu wengine husigina haki za wengine. Mambo haya hayatakiwi kufanyika katika nchi inayosadikika kuwa na idadi kubwa ya waumini wa dini zinazofundisha kuhusu haki na upendo ikiwemo ninyi Kikristo. Unless mtuambia mtaingia peponi kwa kuwadhulumu watu wa dini nyingine.

Hasira ya Mungu iko dhahiri kwa mtu mmoja mmoja, jamii au taifa lo lote ambalo watawala na viongozi wake husigina haki za wengine.
 
M

Mohamed Abubakar

JF-Expert Member
225
500
Mkuu Maalim Mohammed Abubakar,
Naunga mkono hoja, tena isiwe kwa masheikh wa uamsho tuu bali mahabusu wote ambao uchunguzi wa kesi zao haujakamilika, na kuanzia sasa, polisi wasikamate watu kabla ya kukamilisha upepelezi. Mahakama isipokee kesi ambazo DPP hajakamilisha uchunguzi.

Ila pia ukiomba kitu wewe omba tuu usiweke conditionalities, kama CCM imeweza kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kishindo cha asilimia 99.9% huku hao masheikh wanaozea mahabusu, what differences will it make kwa uchaguzi Mkuu?.

P
Karma mkuu, karma
 
Chrismoris

Chrismoris

JF-Expert Member
13,201
2,000
Mahakama imechukua hatua za makusudi kwa kutosikiliza kesi ambazo ushahidi wake haujakamilika, na kesi ambazo ushahidi wake umekamilika mahakama zitaendesha mashauri nayo kwa njia ya teleconference.

Hata hivyo kuna watumuhumiwa waliokaa rumande zaidi ya miaka nane ambapo ushahidi wa kesi zao haujakamilika na upelelezi hauendelei.

Watu hao wapo wengi mahabusu wakiwemo viongozi wa dini Uamsho.

Serikali inapaswa kuona huruma japo kidogo, watanzania hawana furaha kwa sheria hizi kandamizi; na ikitokea mashekhe hawa (Mungu apishe Mbali) kusikia kuwa viongozi hawa wamekufa kwa corona au sababu ingine yyt ile?

CCM itazidi kujipotezea haiba kwa jamii. Na ni maiti pekee ndizo zitakazoweza kukipigia kura kwenye changuzi unaofata. Wananchi na waumini tumechoshwa na mateso haya kwa mashekhe

Ni utoe ushauri wa bure...... Na ombi, mkijisia....

Mh JPM alitoa ushauri kwa DPP hivi karibuni na kwa mamlaka aliyonayo atoe misamaha kwa mahabusu na kuwafutia mashitaka. Ushauri huu wa Mh JPM ulikuwa nandhamira njema wa kupunguza mlundikano wa mahabusu magereza.

Basi nimkumbuse DPP kuwa atumie burasa alizojaaliwa na Mungu kuwaachia huru wote ambao jamii (public opinion) inaona watumumiwa hawajatendewa haki kwa kukaa kifungoni kwa kipindi chote hiki iwaachie huru.

If CCM inaamini itaweza kushinda uchaguzi ujao bila kuwategemea waumini wenza wa mashekhe hawa basi ushauri huu wanaweza kuuzarau.
Kila taifa lina Guatanamo yake
 
chagu wa malunde

chagu wa malunde

JF-Expert Member
2,936

Nafikiri alichoongelea leo JK ni kuhusiana na kesi ambazo ki uhalisia upelelezi wake hauchukui muda mrefu. Au kwa kuangalia tu premafacie utakuta mtu ana kesi ya kujibu. Lakini kwa ishu nzito kama murder au ugaidi.

Ni ngumu sana. Maana wakati mwingine upelelezi lazima ufanyike watuhumiwa wakiwa rumande. Pia sometimes kwa usalama wa mtuhumiwa tu huwa inalazimika mtuhumiwa awe rumande. Nafikiri hii sio ishu ya kuangalia upande mmoja . Inategemea na mazingira ya kesi sio ishu ya kuangalia shilingi upande mmoja.
 
M

Mohamed Abubakar

JF-Expert Member
225
500
Nafikiri alichoongelea leo JK ni kuhusiana na kesi ambazo ki uhalisia upelelezi wake hauchukui muda mrefu. Au kwa kuangalia tu premafacie utakuta mtu ana kesi ya kujibu. Lakini kwa ishu nzito kama murder au ugaidi. Ni ngumu sana. Maana wakati mwingine upelelezi lazima ufanyike watuhumiwa wakiwa rumande. Pia sometimes kwa usalama wa mtuhumiwa tu huwa inalazimika mtuhumiwa awe rumande. Nafikiri hii sio ishu ya kuangalia upande mmoja . Inategemea na mazingira ya kesi sio ishu ya kuangalia shilingi upande mmoja.
Sawa, lkn uchunguzi wa miaka 8; jamii lazima ipate ukakasi.

Justice delayed is justice denied
 
Forum statistics

Threads
1,424,956

Messages
35,077,075

Members
538,169
Top Bottom