Kuna haja ya CCM kutuomba radhi watanzania?

four eyes

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
894
1,000
Jamani Habari?natumai wazima kabisa.

Pamoja na kutokuwa mwanachama ama mshabiki WA Chama chochote cha kisiasa hapa nchini nimejikuta najiuliza haka kaswali kutokana na mambo kadhaa yanayojitokeza nchini.

Toka mheshimiwa Rais aingie madarakani amekuwa akitoa lawama nyingi kulaumu utendaji WA idara mbalimbali na hasa WA kipindi cha nyuma.

Katika lawama hizi amekuwa akiaisitiza uwepo WA uongozi mbovu na usimamizi mbovu,kama haitoshi juzi kaibua suala jipya LA mikataba ya madini huku akiendeleza lawama mpaka kwa viongozi WA ngazi za wizara huku akikwepa kabisa lawama hzo kuzielekeza kwa Marais waliopita.

Lakni sote tunajua Chama ambacho kipo madarakani Muda mrefu ni CCM na viongozi ambao wamekuwa wakiharibu nchi ni kutoka ktk Chama hicho,kama haitoshi kilikuwa na jukumu LA kuwasimamia viongozi wanaotoka ktk Chama hicho na serikali kwa ujumla ktk utendaji wao ili kudhibiti ufisadi.

Je kwkuwa tumegundua Sasa kwamba viongozi toka Chama hiki tawala ndio wametufikisha hapa kwenye dhiki hizi Kuna haja Sasa Chama hiki kuwa na uungwana WA kutuomba radhi wananchi 1 kwa kutosimamia viongozi WA serikali yake vizuri 2 kwa ufisadi uliofanywa na viongozi waliotoka ktk Chama hiki?

Karibuni wadau.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom