Kuna haja ya CCM kuendelea kubaki madarakani kama hata suala la lishe bora kwa Watanzania limeshindikana?

Atropine

JF-Expert Member
Oct 15, 2017
758
1,715
Utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto umeonesha katika watoto milioni 9 wenye umri chini ya miaka 5, kati yao milioni 3 wamebainika kuwa na utapiamlo.

Chanzo cha idadi hiyo kubwa ya watoto wenye utapiamlo ni hari ngumu ya maisha na umasikini uliokithiri miongoni mwa Watanzania inayopelekea Wazazi kushindwa kuwapa lishe bora kwa ukuaji bora wa watoto wao.

Miongoni mwa athari za utapiamlo kwa watoto walio chini ya miaka 5 ni:

1. Udumavu wa mwili uliopitiliza:

Hivyo tutegemee kizazi kijacho kitakua kizazi goigoi kuliko hata hiki cha sasa.

2. Athari ktk ukuaji wa ubongo:

Hivyo tutegemee kua na kizazi kisicho na ustadi na uhodari ktk kazi za nyanja anuai .

3. Urahisi wa kupata mgonjwa:

Kutokana na low immunity (kinga ya mwili kua chini).

4. Lower intellectual Quotient (IQ):

Hivyo tutegemee kua na ongezeko kubwa la vilaza, wajinga na wapumbavu ktk kizazi kijacho.

HITIMISHO:

Kwa athari zote hizo ktk jamii na kizazi kijacho, kuna haja ya CCM kuendelea kubaki madarakani?.

Wasalaam JF GT.

ITV%20TANZANIA%20on%20Instagram_%20_Waziri%20wa%20Afya%20Maendel(JPG).jpg
 
... halafu tutegemee taifa kupiga hatua katika nyanja za hesabu na sayansi wakati nusu ya watoto wana utapiamlo unaopelekea udumavu wa akili! Tusahau hilo!
 
Mitano inamtosha ili tulinde maswaibu kwa vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom