Kuna haja ya Africa kuendelea kujitawala yenyewe???

chief1

JF-Expert Member
May 4, 2015
1,247
2,000
Babu zetu wamepigania uhuru na wakafanikiwa kumtoa mzungu katika bara letu pedwa la Africa, wakajitahidi kutusogeza kimaendeleo kulingana na uwezo wao uliotukuka, watu kama kina Kwame Nkrumah, Nelson Mandela, Julius Nyerere, Patrice Lumumba na wengine wengi, lakini ningepata nafasi ya kukutana na mmoja wao ningemuuliza swali moja tu,swali hilo ni
"Je wakati mnadai uhuru wa Africa mliwaandaa vizuri waafrica kiakili, kifkra,kimwili na ki elimu kujitawala wenyewe "?

Kwa mtazamo wangu kwa jinsi hali ilivyo kwa sasa hapa Africa naona kama hatukujiandaa vizuri kujitawala wenyewe, kuna kitu tulikikosa na bado tunakikosa,hivyo bado hatuwezi kujitawala wenyewe, na hicho kitu tulichokikosa ni "upendo "

Wazungu hawakutufundisha upendo,labda walikuwa wabinafsi au waliuharibu upendo wetu, au walituacha maana tuling'ang'ania uhuru kabla ya wakati, afadhali SA hawakuondoka mapema, angalia jinsi palivyo!

Haishangazi kuona yanayotokea Africa, yote ni kwa sababu hatukujiandaa,
Simshangai Kabila, simshangai Nkrunzinza, simshangai museveni, simshangai Yahya Jameh, siwashangai waafrica wote ,hatukuwekeza kwenye upendo tangu mwanzo, hutukujiandaa..

Swali ni je, kuna haja ya waafrica kuendelea kujitawala wenyewe?
Ilhali hawakujiandaa?
 
mshunami

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
3,988
2,000
Kwahiyo unapendekeza kuwa kama sio Waafrika kuitawala Afrika, nani aitawale? Wazungu au Wachina?
 
NgugiAchebe

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,028
2,000
Babu zetu wamepigania uhuru na wakafanikiwa kumtoa mzungu katika bara letu pedwa la Africa, wakajitahidi kutusogeza kimaendeleo kulingana na uwezo wao uliotukuka, watu kama kina Kwame Nkrumah, Nelson Mandela, Julius Nyerere, Patrice Lumumba na wengine wengi, lakini ningepata nafasi ya kukutana na mmoja wao ningemuuliza swali moja tu,swali hilo ni
"Je wakati mnadai uhuru wa Africa mliwaandaa vizuri waafrica kiakili, kifkra,kimwili na ki elimu kujitawala wenyewe "?

Kwa mtazamo wangu kwa jinsi hali ilivyo kwa sasa hapa Africa naona kama hatukujiandaa vizuri kujitawala wenyewe, kuna kitu tulikikosa na bado tunakikosa,hivyo bado hatuwezi kujitawala wenyewe, na hicho kitu tulichokikosa ni "upendo "

Wazungu hawakutufundisha upendo,labda walikuwa wabinafsi au waliuharibu upendo wetu, au walituacha maana tuling'ang'ania uhuru kabla ya wakati, afadhali SA hawakuondoka mapema, angalia jinsi palivyo!

Haishangazi kuona yanayotokea Africa, yote ni kwa sababu hatukujiandaa,
Simshangai Kabila, simshangai Nkrunzinza, simshangai museveni, simshangai Yahya Jameh, siwashangai waafrica wote ,hatukuwekeza kwenye upendo tangu mwanzo, hutukujiandaa..

Swali ni je, kuna haja ya waafrica kuendelea kujitawala wenyewe?
Ilhali hawakujiandaa?
Hivi kunahaja ya ww kuendelea kuiongoza, familia yako wakati huna akili
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
13,987
2,000
ndio kuna haja ya kuendelea kwasababu afrika ni ardhi ya waafrika
 
lebabu11

JF-Expert Member
Mar 27, 2010
2,005
2,000
Hakuna kitu muhimu kwa binadamu kama uhuru. Waafrika ni lazima waendeleze mapambano ya uhuru wa kiuchumi na kiutamaduni.
Hata hivyo, mafanikio katika mapambano hayo yatapatikana tu pale ambapo watachagua viongozi wenye fikra huru na wasio malimbukeni.
Tatizo kubwa sasa hivi ni wasimamizi wa sera wenye fikra duni za kujiuza kwa bei ya magadi kwa jina la kutafuta wawekezaji.
 
amygdala

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,080
2,000
nafikiri wazungu walikua wanjua kabisa kuwa bado hatuna uwezo wa kujitawalalakin waliamua kutuachia nchi zetu ili waendelee kututawala kwa style nyngne....cc waafrica weusi tuna matatizo sana wenzetu waarabu hata kama mtu ni mroho wa madaraka lakin unaona kabisa ana juhudi za kujenga nchi yake tuliyaona hayo kwa gadafi lakin pia angalia AL sisi pamoja na kuwa alimpindua rais mursi lakini unamuona al sisi anavyofight kuimarisha uchumi wa misri sasa vitu kama hivi ndo ambavyo sisi sub saharan tunavikosa..sometym watu wanaweza wasimind mtu kubaki madarakan mda mrefu kama kweli unafanya mambo yanaonekana yana msalahi na taifa linakimbia kusonga mbele
 
chief1

JF-Expert Member
May 4, 2015
1,247
2,000
Hakuna kitu muhimu kwa binadamu kama uhuru. Waafrika ni lazima waendeleze mapambano ya uhuru wa kiuchumi na kiutamaduni.
Hata hivyo, mafanikio katika mapambano hayo yatapatikana tu pale ambapo watachagua viongozi wenye fikra huru na wasio malimbukeni.
Tatizo kubwa sasa hivi ni wasimamizi wa sera wenye fikra duni za kujiuza kwa bei ya magadi kwa jina la kutafuta wawekezaji.
Elimu, Elimu, Elimu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom