Kuna haja uongozi wa chadema kutueleza kura zetu zilikwenda wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna haja uongozi wa chadema kutueleza kura zetu zilikwenda wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uncle Rukus, Dec 6, 2010.

 1. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndugu poleni kwa majukumu ya kila siku.
  Ningependa kuwasilisha hoja jukwaani kuhusiana na kuelezwa kilichojiri kwenye matokeo ya uchaguzi wa raisi. Na kumbuka Dr slaa alishaandikwa sana kwenye vyombo vya habari kuwa anafanyia uchunguzi baadhi ya taarifa na angetueleza wapiga kura wake kuwa kura zetu zimekwenda wapi au kama alishindwa ki halali alishindwa kwa kura ngapi na alichobaini kwenye matokeo ya mawakala baada ya kukusanya nakala ni kipi?

  Kuna haja ya kufanya hivyo maana na amini siko peke yangu ninaye hitaji kujua ukweli wa zile nakala halisi kutoka kwa mawakala zilikuwa na idadi au kiwango gani cha kura tofauti na matokeo tuliyojisi kuwa yamejaa utata yale yaliyotangazwa na NEC.

  Mimi binafsi yangu naamini kuwa inchi ina maraisi 2, mmoja yuko ikulu na mwingine yuko uraiani ambaye ni Dr Slaa. Sasa naomba wazidi kutujengea imani sisi wafuasi wao makini ambao tuko kwenye chama makini watueleze ukweli usio na shaka kwa kile walichokibaini kwenye matokeo ya kura ninazo amini huenda zilichakachuliwa.
   
Loading...