Kuna haja uongozi wa chadema kutueleza kura zetu zilikwenda wapi?

Uncle Rukus

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
2,425
0
Ndugu poleni kwa majukumu ya kila siku.
Ningependa kuwasilisha hoja jukwaani kuhusiana na kuelezwa kilichojiri kwenye matokeo ya uchaguzi wa raisi. Na kumbuka Dr slaa alishaandikwa sana kwenye vyombo vya habari kuwa anafanyia uchunguzi baadhi ya taarifa na angetueleza wapiga kura wake kuwa kura zetu zimekwenda wapi au kama alishindwa ki halali alishindwa kwa kura ngapi na alichobaini kwenye matokeo ya mawakala baada ya kukusanya nakala ni kipi?

Kuna haja ya kufanya hivyo maana na amini siko peke yangu ninaye hitaji kujua ukweli wa zile nakala halisi kutoka kwa mawakala zilikuwa na idadi au kiwango gani cha kura tofauti na matokeo tuliyojisi kuwa yamejaa utata yale yaliyotangazwa na NEC.

Mimi binafsi yangu naamini kuwa inchi ina maraisi 2, mmoja yuko ikulu na mwingine yuko uraiani ambaye ni Dr Slaa. Sasa naomba wazidi kutujengea imani sisi wafuasi wao makini ambao tuko kwenye chama makini watueleze ukweli usio na shaka kwa kile walichokibaini kwenye matokeo ya kura ninazo amini huenda zilichakachuliwa.
 

KIMICHIO

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
1,180
1,225
Mkuu siyo kama umepotea jukwaa au ni macho yangu yana vibration niyaweke silence?
 

Uncle Rukus

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
2,425
0
Mkuu siyo kama umepotea jukwaa au ni macho yangu yana vibration niyaweke silence?

Ni kweli mkuu nimepotea jukwaa... hata hivyo nimewasiliana na MODS wanisaidie kuihamishia kwenye jukwaa la siasa naona hadi sasa kimya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom