Kuna haja kwa kampuni ya TIGO kubadili jina hili la matusi?

Nadhani haya yote yalitokana na tangazo lao...Tigo, mtandao unaokupa zaidi, kubadili jina hakuna maana labda kama wao wataona wanapoteza wateja kwa kuogopa kusema ...mie napenda Tigo..wakimaanisha mtandao wa tigo . Sio kazi yetu.
 
TIGO mtaani kwa sasa ni neno tata kwani linafarakanisha watu kutokana na jina hilo kutumiwa kwa matusi,hili linaishusha hadhi na watu waoheshimiana huogopa kuwa na mtandao huo kuogopa kutaja neno hilo.Je ili kulinda heshima ya kampuni si vema kubadili jina hilo kuachana na matusi?Hivi ni nini chanzo cha neno hilo kutumika kama matusi?Wanajamvi changieni.

You better change your mind na si jina la mtandao.
 
mkuu kweli kabisa.....siku hizi JF hamna great thinking.....thread za kipuuzi puuzi kila siku.....alafu kumezuka siku hizi kila kitu udini..kuna watu sijui wametumwa kila kitu wenyewe wanasema ni udini....najua nia yao.....
....msione watu mnaowaulizia wamepotea... ni wapo lakini wanasoma upupu wenu na kusikitika....

....tubadilike thread za upupu hazifai.....kuna thread ambazo mpaka mtu unajiuliza hii ni JF?

Mkuu,
Ahsante sana kwa angalizo hili muhimu. Nadhani iko haja Mods na uongozi wa JF ufanye tathmini mahsusi kabisa itakayoangalia uwezekano wa kupunguza kasi hii ya 'threads upupu'. The way I see, mwendo huu ninaufananisha na uvamizi wa viwavi-jeshi katika shamba, tusipokuwa wangalifu ubora wa JF utaporomoka kwa kasi kama si kwa kishindo.
 
kusema kweli kwa sasa hata ukiwa kwenye Daladala ukipigiwa simu anaambiwa kuwa weka line ya Tigo,ukisema kwamba tigo yako umeacha nyumbani utasikia abiria wote wanaangua kicheko.mi sijui tufanyaje kuhusu hili.
 
our thinking capacity is very low ndo maana tunabadilisha maana za maneno,tubadili mitazamo na fikra zetu katika kuwaza ili tusipotoshe maana ya maneno,mimi sioni shida ya jina tigo hao wanaopata shida na hili jina nadhani its better wakajichunguza uwezo wao wa kufikiri.
 
Kama tulikuwa tunaweza kutumia fikra zetu kwenye kusoma vitabu kutafakari namna ya kuchagua au kuwa kiongozi bora na mwenye maadili nafikiri our mind could have no room for thinking of destroying people's business....infact sisi hata matumizi ya simu bado yanatutatiza mtu anaweka 2000 anaongea ujinga na matusi kwani hio hela siingekusaidia kwa mambo mengine?? hasa wanafunzi wa elimu ya juu(vyuoni). Kukiwa na mada redioni tunaanza naitwa Nguli niko na kyachakiche tunamngoja itei tei la kite watakuja Ndugu.....lakini mada inataka tuchangie uchafuzi wa mazingira wapi tunakwenda???
 
This thread shows how much people are not serious and concentrating on issues. It disappoints to see the way our thinking resources are applied.
Do we still need someone to blame?
Wewe unafikiri ni mzaha lakini watu wanadundana mtaani kwa neno TIGO.Hata wewe ukiwa mtaani mwambie mtu nipe TIGO yako uone muziki wake.
 
Wanajamii inabidi muwe makini na fikra zisioleta maendeleo TIGO Inabaki hivyo hivyo,kabla watu walitafsiri KISAMVU,MBAAZI,KUNDE NA HATA BAMIA kwa maana mbalimbali kimatusi lakini leo zipo wapi hizo tafsiri zao. TUBADILIKENI tupeana vile ambavyo vitatuneemesha sasa na vizazi vyetu vya baadae tuache fikrana mawazo mabovu.
 
mkuu,
ahsante sana kwa angalizo hili muhimu. Nadhani iko haja mods na uongozi wa jf ufanye tathmini mahsusi kabisa itakayoangalia uwezekano wa kupunguza kasi hii ya 'threads upupu'. The way i see, mwendo huu ninaufananisha na uvamizi wa viwavi-jeshi katika shamba, tusipokuwa wangalifu ubora wa jf utaporomoka kwa kasi kama si kwa kishindo.

mategemeo yangu ni kuwa tutajenga fikra za kuokoa taifa letu kupitia jf. Lakini kwa "prejudised threads" hatutafika.
Uongozi wa jf wawe makini, tusipoteze "vision" na "mission" ya jf.
 
....Wanajamii inabidi muwe makini na fikra zisioleta maendeleo TIGO Inabaki hivyo hivyo,kabla watu walitafsiri KISAMVU,MBAAZI,KUNDE NA HATA BAMIA kwa maana mbalimbali......
Kisamvu walikuwa wanamaanisha nini ati?
 
Inabidi wabadilishe staili tu kama vile Mzee Kenyatta alivyofanya kule Mombasa.

Mzee Kenyatta akitoa hotuba yake mjini Mombasa, watu wakawa wanamshangilia na kusema mzee sisi tupo nyuma yako.

Kenyatta akawajibu " Nyinyi watu ya Mombasa mnafanya nini nyuma yangu, sema twende bega kwa bega. Hapana kaa nyuma angu".
hahaaa mkuu you make my day..nimecheka sana...bega kwa bega sio kukaa nyuma yanguuu wanikumbusha mambo la LAMU mie
 
Tena jana kuna sehemu nimepita watu walikuwa wanazozana kuhusu mmoja kumwambia mwenzake mbona unaipenda TIGO sana wewe.Kweli ukosefu wa maadili sasa inapotosha lugha ya kiswahili.
 
Nakumbuka kwanza ilikuwa mobitel, watu wakaita wasichana wadogo wadogo vimobiteli. Then Ikaitwa BUZZ, wababa wapenda vimwana wakaitwa mabuzi. Inaitwa tigo, tayari ishapewa tafsiri nyingine. Nawahakikishia hata ikipewa jina jingine bado watapewa tafsiri mpya. Cha msingi si kubadili jina ila kubadili FIKRA!! Namsapoti Mchungaji Mwema, tubadili fikra, si jina!! Mchungaji Mwema, chunga kondoo wako vizuri.
Kwanini kampuni hii tu ndio inabatizwa majina mabaya? Why not Tritel au Celtel na sasa Zain? Is it something to do with business competition?
 
tigo neno la kispanish inamaanisha "everywhere".sasa kama unataka ibadirishwe kwa vile wanatumia vibaya neno hilo kama matusi basi itabidi tubadirishe neno "jicho" pia manake watu wanalitumie vibaya pia.
 
Haya kama siyo tu basi nipe TIGO! Nawe ukifika vijiweni sema hivyo uone muziki wake.
 
Back
Top Bottom