Kuna haja kwa kampuni ya TIGO kubadili jina hili la matusi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna haja kwa kampuni ya TIGO kubadili jina hili la matusi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mmaroroi, Jul 8, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  TIGO mtaani kwa sasa ni neno tata kwani linafarakanisha watu kutokana na jina hilo kutumiwa kwa matusi,hili linaishusha hadhi na watu waoheshimiana huogopa kuwa na mtandao huo kuogopa kutaja neno hilo.Je ili kulinda heshima ya kampuni si vema kubadili jina hilo kuachana na matusi?Hivi ni nini chanzo cha neno hilo kutumika kama matusi?Wanajamvi changieni.
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mkuu ni kweli ila nafikiri tatizo haiko kwa kampuni ya tigo kwa sababu wakati wanalianzisha lilikuwa safi ila tu binadamu na rotten minds zetu. Am sure hata wakija na lingine watu wakiamua wanaweza kulifananisha na kitu kingine. Kuwaambia wabadili ni kuwaonea tu

  mtazamo wangu
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tigo limekaa vibaya. Hata wakitafsiri voda vibaya haliwezi kuleta tafsiri mbovu. Tigo wabadili jina tu
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Tutabadilisha hadi tutachoka, hakuna haja yoyote.
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Tuseme wabadili jina, na hilo nalo likichukuliwa na washashi wakamaanisha kitu kibaya itakuwaje? Itabidi wabadili tena?

  Hapa tatizo ni kuwa huwezi kuzuia lugha isiyo rasmi, laiti kama mtu angekuwa anaandika au kutumia neno Tigo vibaya katika mazingira rasmi Tigo wangeweza kuwa na kesi ya kuhusu hatimiliki na alama ya biashara.
   
 6. Poetik Justice

  Poetik Justice Member

  #6
  Jul 8, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwani TiGo ni matusi? I always express myself na TiGo
   
 7. M

  Mchungaji mwema New Member

  #7
  Jul 8, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna haja ya kubadilisha fikra zetu!!
   
 8. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Inabidi wabadilishe staili tu kama vile Mzee Kenyatta alivyofanya kule Mombasa.

  Mzee Kenyatta akitoa hotuba yake mjini Mombasa, watu wakawa wanamshangilia na kusema mzee sisi tupo nyuma yako.

  Kenyatta akawajibu " Nyinyi watu ya Mombasa mnafanya nini nyuma yangu, sema twende bega kwa bega. Hapana kaa nyuma angu".
   
 9. K

  Kamuna JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 297
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kwa nini neno TIGO limepewa tafsri ya matusi?someone help me-ilkuwaje hata neno TIGO likapewa maana hiyo na siyo neno VODA au neno lolote?
   
 10. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  This thread shows how much people are not serious and concentrating on issues. It disappoints to see the way our thinking resources are applied.
  Do we still need someone to blame?
   
 11. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Very low! Tatizo watu wanafikiri Tigo ipo Tanzania pekee!!
   
 12. mbuvu

  mbuvu Member

  #12
  Jul 9, 2009
  Joined: Jul 3, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hakuna sababu ya kubadulisha jina ila watu wasipotoshe maana ya tigo.
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,014
  Likes Received: 23,934
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka kwanza ilikuwa mobitel, watu wakaita wasichana wadogo wadogo vimobiteli. Then Ikaitwa BUZZ, wababa wapenda vimwana wakaitwa mabuzi. Inaitwa tigo, tayari ishapewa tafsiri nyingine. Nawahakikishia hata ikipewa jina jingine bado watapewa tafsiri mpya. Cha msingi si kubadili jina ila kubadili FIKRA!! Namsapoti Mchungaji Mwema, tubadili fikra, si jina!! Mchungaji Mwema, chunga kondoo wako vizuri.
   
 14. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  kUNA WENGINE WANAITWA VODA FASTA NA SII WAUZA VOCHA
   
 15. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  mkuu kweli kabisa.....siku hizi JF hamna great thinking.....thread za kipuuzi puuzi kila siku.....alafu kumezuka siku hizi kila kitu udini..kuna watu sijui wametumwa kila kitu wenyewe wanasema ni udini....najua nia yao.....
  ....msione watu mnaowaulizia wamepotea... ni wapo lakini wanasoma upupu wenu na kusikitika....

  ....tubadilike thread za upupu hazifai.....kuna thread ambazo mpaka mtu unajiuliza hii ni JF?
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  tigo awali walikuja na kaulimbiu yao isemayo togi-mtandao ulioenea zaidi pwani. na si unajua pwani kumejaa mambo ya kuruka ukuta?
   
 17. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #17
  Jul 9, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wanajamii naomba niwape chanzo cha jina la tiGo kutafasiwa vibaya.

  kwenye tangazo lao linapomalizika ile O inafanya kama kubana jicho na hicho ndio chanzo kwa hiyo napendekeza TiGo wangeondoa hiyo O kwenye jina lao na kuitwa tiG.

  Vile vile kama na nyie mnakaa katika mazingira ya tafsiri pia voda ile V ni tatizo.
   
 18. G

  Godwin Mpagasi Member

  #18
  Jul 9, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndiyo faida yakubadili majina mara kwa mara,ni sawa na kujichubua ngozi matokeo yake nikupata kansa
   
 19. M

  Mopao Joseph Member

  #19
  Jul 9, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  vitu kama hivi vinatumika sehemu nyingi (world wide) either ushindani wa kibiashara au kimtaa zaidi
   
 20. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #20
  Jul 9, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,800
  Likes Received: 2,481
  Trophy Points: 280
  kwani hilo neno la tigo ni kiswahili au lugha gani mpaka lilete tafisiri mbaya.
  kikubwa ni utashi mdogo wa watanzania kutafsiri maneno kwa maana isiyo eleweka.

  Neno Tigo lipo kwenye kamusi gani au sisi ndio tunaliendekeza mpaka liwe neno baya?

  Hakuna haja ya kampuni hiyo kubadili jina lake.
   
Loading...