Kuna Haja Gani Ya Mtu Kudanganya Umri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna Haja Gani Ya Mtu Kudanganya Umri?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Apr 13, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,169
  Trophy Points: 280
  lwe ni shuleni,
  kazini,
  kwenye mahusiano na shughuli mbalimbali,
  je kuna haja gani ya kudanganya umri?
  Hivi aibu yako utaiweka wapi umri wako halisi ukibainika?
   
 2. senator

  senator JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Zaman watu walikuwa si kama wanadanganya Umri bali ilikuwa hakuna record siku gani mtu amezaliwa, haswa kwa watu wa vijijini, siku hizi watu kwenye kazi wanarudisha nyuma ili kuongeza muda wa kuwa kazini lakin sidhan kama inawork mana maisha yenyewe haya...Ukifika 55 upo choka mbaya hata memory inapotea kwa kichwa.Kimsingi hakuna wanaodanya umri wanakuwa wamekosa uaminifu iwe kwenye mahusiano au kazini...
   
 3. Z

  Zebaki Member

  #3
  Apr 13, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna haja wala hakuleti faida, ni uwoga tu wa kuonekana mzee ;)
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Wanaogopa kulinganishwa matendo yao na umri wao. Me nashangaa watu wanadanganya umri ili waonekane watoto na uki mwambia mtu we ni mtoto anakasirika. Sasa nashindwa kuelewa wanaamka au wanalala?
   
 5. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  .........Mie huwa nawashangaa sana watu wanaodanganya umri, watu wengi utakuta wanapenda kujiweka katika umri mdogo. Hii ipo sana Tanzania au tuseme bara la Africa watu hawapendi kusema ukweli wa umri wao. Utakuta mtu sura imemkomaa kweli kweli lakini umri anaoutaja hadi mtu unabaki kushangaa..........uzee jamani upo tu na lazima tu tuzeeke hivyo tuwe huru kutaja umri wetu........kuna mwanamuziki aliimba nikikumbuka uzee silali.
   
 6. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kazi ipo mie naanza na kutaja umri wangu 35!!
  tuendelee!!!!
   
 7. senator

  senator JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Ujana maji ya moto....Fainali uzeeni...ila watu wengine wanapenda kuonekana wakubwa wakati umri mdogo...afu kuna baadhi ya makabila (wakina ni thithithi)unaweza kumzania mdogo kumbe chumvi zakutosha amekula
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,169
  Trophy Points: 280
  Kuna rafiki yangu alikuwa na mchumba na kwao alishampeleka kumtambulisha.
  Cha kuchekesha ni kwamba binti alitangaza ana miaka ishirini na sita,
  bahati mbaya binti akafariki kwenye ajali.
  Wakati wa kusoma wasifu wa marehemu ndio jamaa akaja gundua kuwa binti alikuwa amezaliwa mwaka 1973.
  Jamaa alilia sana, sasa baada ya kumpooza akatutobole siri kuwa alikuwa amedanganywa umri na marehemu mchumba wake.
   
 9. T

  Tall JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  UONGO KATIKA UMRI:
  1.Kuna uongo wa shuleni,kwavile miaka sita huwezi anza darasa la kwanza inabidi useme unamiaka saba.
  2.Maenzi,kama niae mtaka ni mkubwa au mtoto kuliko mimi inbidi ni adjust umri angalau ufananefanane
  3.Kuaminika,kuna watu,umri wao na wao wenyewe tofauti kabisa,akitaja umri halisi watu wote hawaamini wanabaki kucheka,sasa anaona bora ataje huohuo.
  4.Heshima,kuna wenye mawazo kuwa watu wazima wanaheshimika zaidi kwa hiyo nao hujiadjust huko huko ukubwani.
  5.AJIRA, NAFASI za kazi zinataka wenye umri usiozidi 40,na wewe una 41 hapo piga ua mwaka mmoja lazima upigwe kitanzi
  6.kutojua, kuna watu tumezaliwa hukooo madongo kwinama mambo ya mwaka,tarehe unatakanikudanganye tu
  7.Kustaafu,kuna umri maalum wa kustaafu,ukiajiriwa ukitaja miaka mingi zaidi maana yake ustaafu mapema.
  UTAGUNDUA KUWA UMRI UDANGANYIFU WA UMRI UNAFANYIKA ILI MTU AFAIDIKE AU APATE AKITAKACHO

  LAKINI UONGO WA AINA YOYOTE ILE HAUFAI NA WAONGO WOTE UFALME WA MBINGUNI WATAUSIKIA REDIONI TU(HAWATAUONA)
  LABDA UONGO HUO UWE UNA NIA YA KUOKOA UHAI WA MTU.
   
 10. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ni inferiority complexes ndio zinawasumbua watu na HOFU zimewajaa watu mpaka wanashindwa kuweka wazi umri wao halisi.
  Tunaogopa ku-face challenges mbalimbali za kimaisha.
   
 11. T

  Tall JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Na mimi ngoja niwasiliane na wakubwa kule kijijini,baadae nitawajulisha UMRI wangu........ au wana JF mnadhani nina umri gani?
  Halafu wewe Maria kama picha ya avatar yako ni ya kwako wewe na ni ya hivi karibuni,huo sio umri wako.
  POSTS na thread zako zinanielekeza kuwa you are a little bit less than 35/ upo chini ya 35. USINIULIZE.
   
 12. T

  Tall JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  inawezekana kabisa mheshimiwa,lakini kumbuka swala la tall,kazaliwa porini sana huenda kule umasaini,enzi zileeee,tena sio hospitali,nitajuaje mwaka?
   
 13. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  wengine wana maumbo makubwa,wakisema umri wakweli watu wanawacheka na kudai wanapunguza umri waonekane wadogo.
  Alafu waTanzania tuna pima umri kwa muonekano na maendeleo au uwezo wa mtu,nina jamaa yangu yko kwenye her late 20s anajiweza sio masihara lakini akisema umri wake kwa watu wanasema anapunguza umri kwani hawezi kuwa na maendelea aliyo nayo kwa umri wake,basi anakubari tu aonekane 37
   
 14. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kama mtu hajui umri wake au alizaliwa lini basi huyo hayupo kwenye kundi la wanaodanganya bali la wasio jua.
  Na wasio jua umri wao siku hizi ni wachache sana,sie wote tuliozaliwa 70s ni wachache sana hawana idea na tarehe za kuzaliwa kwao.
   
 15. Jacbest

  Jacbest Member

  #15
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni hulka ya mtu tu. Wengi hawataki kuonekana wazee ili wasikose starehe za ujanani. Hawajui kuwa ''Old is Gold''. Dawa yao ni kumwabudu Mungu tu.
   
 16. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,169
  Trophy Points: 280
  Biblia ya wapi imeandika hivi?
  Naomba msaada wako pulizi.
   
 17. T

  Tall JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  ahaaaaaa,hapohapo kabla hujaenda mbali,soma kisa cha ibrahim na mkewe sara, ili kuokoa maisha yake,
  ibrahimu alidanganya kuwa sara si mkewe..............................PIA fikiria majambazi wameingia ndani ya nyumba yako na wana siraha. mwenzio kasevu yupo uvunguni,
  Wale jamaa wana kuuliza YUKO WAPI? ili kwenda mbinguni uta sema '' yu yu yupo uvunguni''? hapo italazimu uongope uokoe maisha.utasema karukia dirishani kakimbia.
   
 18. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,712
  Likes Received: 8,258
  Trophy Points: 280
  Duh I hope kukaa kimya si kudanganya!
  Maana mimi hupendelea watu kunipa umri wanaojisikia..na mimi wala sisemi!
   
 19. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,712
  Likes Received: 8,258
  Trophy Points: 280
  Sanda, huyo nduguyo yupo single bado? maana na mimi niko kwenye early thirties!
   
 20. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,952
  Likes Received: 23,831
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono. mi nafukuzia 44 ila haya mapombe watu wakinionaga wanasema nina above 55.
   
Loading...