Shukurani
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 251
- 11
Jana katika kikao cha bunge, wachangia hoja waliopata nafasi waliwapongeza Lowasa, Karamagi na Msabahaa kwa uamuzi wao wa kujiuzuru. Kwa upande wangu sikuona sababu ya kuwapongeza watu ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao na kulitia taifa hasara kubwa. Kiujumula Lowassa alitakiwa ajiuzuru toka miezi sita iliyopita baada ya serikali kuonyesha udhaifu mkubwa sana kwa kuingia mkataba na kampuni hewa,hii ni fedheha kubwa sana. Ndani ya baraza la mawaziri kulikuwa na PhD ngapi? na masters ngapi? zisiweze kujua mambo haya, sitaki kuamini unahitaji elimu kubwa kugundua utapeli wa watu. Ni uzembe uzeembe, sihitaji kumpongeza fisadi yeyote kwa kujiuzuru. nitampongezaje mtu anayeniumiza kwa kunipandishia bei za umeme kila kukicha, ni wendazimu huu. nitalazimika kuwataka wale wote waliowapongeza mafisadi hawa wafute kauli zao ama wajiuzuru,