Kuna haja gani ya kuwa na taifa la wasomi?

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,118
Nipo Benjamin William Mkapa nasoma kipindi kile (2002-2005) huwa kuna swali najiuliza:

Hivi hizi Chemistry, Biology, Physics, Mathematics, History, Book-Keeping, Civics, English, Kiswahili na Geography huko Ulaya nao wanasoma hizihizi kweli!?

Mbona wenzetu wakimaliza masomo mpaka chuo wanakuwa watu wenye mawazo,maono na fikra zinazoendana na nafasi zao katika jamii zao na serikali. Mbona wenzetu wakimaliza masomo kama ni mwanasiasa anakuwa mwanasiasa na mleta mabadiliko ya kweli na si ubaguzi?

Kama ni injinia anaijenga nchi yake kwa
majengo marefu,barabara nzuri,viwanda vya magari na kila aina ya ubunifu na uvumbuzi wa kisayansi kwa nchi yake

Kama ni daktari anatibu na kutengeneza
kinga dhidi ya magonjwa,uvumbuzi wa dawa mpya za magonjwa mbalimbali na vifaa tiba

Kama ni mfanyabiashara anakuja kuwa mfanyabiashara mkubwa duniani na kutufikia sisi hizo bidhaa zake na kampuni zake kusambaa na kuja hata kuajiriwa na sisi huku Africa

Mbona huku kwetu ni tofauti kabisaa yani mkimaliza chuo wale mainjinia wanaenda kuwa wachungaji,waganga wa kienyeji na matapeli
Wale madaktari wanaenda kuwa madaktari wa kuwapa watu Panadol,kutoa mimba na migomo ya mishahara
Wale wanasiasa wanaenda kuwa waalimu wa vyuo vikuu na wakuu wa wilaya,wanasaikolojia na ma MC's WA sherehe
Wale waliosoma history na arts schools kule chuo na sekondari wanakuja kuwa bodaboda,motivational speakers,mabraza men na matapeli

Sasa katika kundi hili la graduates mmoja Wapo paap anakuwa raisi wa nchi hivi unafikiri ataamini tafiti za kisayansi,atasikiliza ushauri wa wataalam wa afya,atasikiliza majibu ya tafiti

Hivi Viongozi wetu wa Africa kama hawaamini sayansi,madaktari,na tafiti mbalimbali kuhusiana na magonjwa,mafuriko,hali ya hewa,matetemeko ya Ardhi,uchumi basi hakuna haja ya kuwa na taifa la wasomi wala kuwa na Viongozi wasomi wa PhD,degree wala diploma tutambulishane na kupeana madaraka kwa uwezo wetu wa kupiga maombi,kupiga ramli,kusoma ahlal badil,kupaa na ungo,kuweka misukule labda hili litatusaidia maana ndio wengi wetu tunaamini huko kuliko kupambana na janga Kama la CORONA covid19 kwa njia za kisayansi.

Asanteni nawasilisha
Capture%2B_2020-04-17-17-25-34.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me Nadhani tatizo ni Sisi tuu wenye yaani Nature yetu,Hatup effective kwenye hilo swala Maana huu mfumo wa elimu wenyewe wao Waliutumia kitambo.
.
Sisi ndio wenye matatizo
Africans We have Problems that's all
 
Kwa bahati mbaya wanaoongoza nchi siyo wasomi kwa maana halisi ndio maana corona itafyeka sana.
 
Me Nadhani tatizo ni Sisi tuu wenye yaani Nature yetu,Hatup effective kwenye hilo swala Maana huu mfumo wa elimu wenyewe wao Waliutumia kitambo.
.
Sisi ndio wenye matatizo
Africans We have Problems that's all
Matatizo gani hayo mkuu tujurishane?
 
Me Nadhani tatizo ni Sisi tuu wenye yaani Nature yetu,Hatup effective kwenye hilo swala Maana huu mfumo wa elimu wenyewe wao Waliutumia kitambo.
.
Sisi ndio wenye matatizo
Africans We have Problems that's all
Nakuunga mkono mtalaam yaan history uliyoisoma ww na mjomba wako baada ya miaka 20 ataisoma historia iyo iyo
 
Back
Top Bottom