Kuna haja gani ya kuwa na mahakama zisizoweza kuwapa wananchi haki zao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna haja gani ya kuwa na mahakama zisizoweza kuwapa wananchi haki zao?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Magezi, Jun 18, 2010.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nimesoma hukumu ya jana juu ya mgombea binafsi mpaka nimepatwa na homa. Nimesikitishwa na kauli kwamba mahakama za Tanzania hazina mamlaka ya kuwapa wananchi haki zao zilizo minywa na katiba ya kikoloni mpaka bunge, labda zinaweza kushauri tu.

  Najiuliza swali, kama kweli mahakama hazina uwezo wa kuwapa haki wananchi ambazo zinakiukwa na katiba, je wizara ya sheria inakazi gani?? Mwanansheria mkuu wa serikali anafanya kazi gani ili kuwasaidia wananchi??

  Nachelea kusema ndiyo maana vita vya weneywe kwa wenyewe afrika havita kwisha kwa sababu ya ukoloni wa sisi wenyewe watu weusi.
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nina wasiwasi huenda CJ ana kadi ya kijani yenye nembo ya jembe na nyundo mfukoni.
  Yaani hawa waheshimiwa saaaana majaji wanashindwa kuelewa kwamba siasa ni maisha, ni maisha ya watu ambayo kila mmoja anatakiwa kuishi bila kuwekewa vikwazo ama vizingiti visivyokuwa na maana. Kusema kwamba suala la mgombea binafsi ni la kisiasa likaamuliwe bungeni huku wakijua kabisa kwamba mara zote bunge la ccm na serikali yake hawataki kusikia suala la mgombea binafsi ni upotoshaji mkubwa wa haki za kiraia na kidemokrasia, na mbaya zaidi mahakama imechangia kabisa kudidimiza haki za watanzania.
  Hukumu hii imeitia aibu mahakama kwa ujumla wake na kupoteza hata ile imani ndogo tuliyokuwa nayo kwamba mahakama za tanzania zinawatendea haki watanzania.Hukumu hii imeonyesha ni kiasi gani mahakama zetu zinafanya maamuzi kwa kushinikizwa na CCM na serikali yake.
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inaweza kuwa hizi tetesi kuwa Mahakama imeshinikizwa na serikali zikawa za kweli
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jun 18, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nimesikitishwa sana na kauli zifuatazo za Mahakama ya Rufani:

  1. At no time in the history of this country we have had sour relationship between Executive and the Judiciary!
  Hapa tunapewa somo kwamba wakubwa LAZIMA waheshimiane, Sheria zimewekwa pembeni, wakubwa waliowekana madarakani LAZIMA wapeane HESHIMA!

  2. Courts are NOT the Custodians of the will of the People. That is the property of the elected Members of Parliament!
  Nilikuwa sijui kama Mahakama hazifuati matakwa ya wananchi na ni kazi za wabunge pekee! Jana ndio nimefumbuka macho ndugu zangu kupitia kesi hii! Swali la kujiuliza, hizi Sheria zimetungwa kwa ajili ya mawe au miti? Napata shida sana!

  3. Tanzania Courts exercise calculated restraint to AVOID MEDDLING in counstituencies of other two pillars of state!
  Hii kauli utafikiri haitoki kwa Mwanasheria, ni afadhali kama ingetolewa na vijana wavuta bangi vijiweni! Kwani hapa suala lilikuwa ni kuepusha malumbano au kulinda haki za wananchi za kugombea? Naona maruwe ruwe kwenye hili. Jopo la Majaji saba (7) walipoteza fedha zetu bure kutuletea kauli za KISIASA!

  4. The issue of independent candidates IS POLITICAL AND NOT LEGAL!
  Hapa Jopo la Majaji saba (7) ndio limetoa kituko cha mwaka! Kama suala la mgombea binafsi SI LA KISHERIA kwa nini walilipokea Mahakamani? Mbona katika ukurasa wa 19 Mahakama ya Rufani imedai kwamba Mahakama Kuu ya Tanzania ilikuwa na mamlaka (Jurisdiction) ya kusikiliza shauri hili? Sasa Mahakama Kuu ilikuwaje na Mamlaka ya kusikiliza suala la kisiasa? Hapa nimepata homa kabisa kuhusu Hukumu ya ajabu ya Mahakama ya Rufani!
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145


  That would mean the constitution of the United Republic of Tanzania which provides for the citizens' rights and duties is a political document as well!.
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mahakimu wote na Majaji wa tz ni makada wa CCM, hakuna tofauti kati yao na makamba au chiligati. Kuwapelekea kesi ya kikatiba isiyo na maslahi kwa CCM ni kukimbizana na upepo.
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Mbona zile za uchaguzi huwa wanaamua!
   
 8. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Cry, the beloved country!
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Elimu ndo tiba ya uhuni wa serikali hii
  tusichoke kuwaelimisha watanzania wenzetu wajue hapa tulipo ni wapi
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Jun 18, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Yaani hiyo statement imenichosha sana!
   
 11. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa heshima na taadhima naomba niuunge mkono mchango wa BUCHANAN hapo juu.

  Ni kweli kabisa this was expected and what the Judges did was copying and pasting what Prof Kabudi as an amicus curiae told the court.Hatuna wale majaji bold minded aina ya akina Mustapha,Lugakingira,Mwalusanya na akina Biron wa 1970's.

  The CAT has subjected itself to the executive and judiciary not knowing that its an independent institution in making its decisions.This concept of avoiding a confrontation with the executive is outmoded.

  How comes the constitution says one thing and the other???This is a clear miscarriage of justice.Serikali itakuwa imeweka mkono wake na wanaogopa yale mambo ya akina Sarwatt yaliyotokea 1960's.
   
 12. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  For everything I have endeavored to s tate and
  notwithstanding the exclusionary elements to that effect in
  arts 39, 67 and 77 of the Constitution as well as s 39 of the
  Local Authorities (Elections) Act 1979, I declare and
  direct that it shal l be lawful for independent
  candidates, along with candidates sponsored by
  political parties, to contest presidential,
  3
  parliamentary and local council elections. This will not
  apply to the council elections due in a few days.

  Sehemu ya hukumu ya Jaji Lugakingira kuhusiana na mgombea binafsi mwaka 1993.
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,700
  Trophy Points: 280
  Hukumu ya jana kwa mara nyingine tena imethibitisha kwamba mahakama zetu haziko huru inapokuja kwenye maamuzi yanayohusu Serikali na watu wenye vyeo vikubwa na pesa nchini. Huyu Jaji ramadhani aliwa kutamka kwamba mahakama zetu zimejaa rushwa ya hali ya juu. Mahakama zetu zinafanya kazi ili kulinda maslahi ya watu wachache badala ya wale walio wengi.
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Jun 18, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sure!
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Hakuna mgombea binafsi  [​IMG] Yasema mahakama haina mamlaka kugusa Katiba
  [​IMG] Wengi wapokea hukumu hiyo kwa mshangao  [​IMG]
  Jaji Mkuu Augustino Ramadhani, akiongoza Majaji wengine sita wa Mahakama ya Rufaa wakati akitoa hukumu kuhusu mgombea binafsi kufuatia serikali kukata rufaa katika mahakama hiyo.  Mahakama ya Rufani imesema haina mamlaka ya kuruhusu mgombea binafsi katika uchaguzi wa kisiasa, bali chombo chenye mamlaka hayo ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambalo ni chombo pekee cha kutunga sheria.
  Uamuzi huo uliotolewa jana umetengua uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania kuruhusu mgombea binafsi. Hukumu hiyo ilitolewa kufuatia rufani ya Serikali dhidi ya Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ambaye alikuwa mjibu rufani, aliyefungua kesi Mahakama Kuu akitaka kuruhusiwa mgombea binafsi na mahakama hiyo kumkubalia.
  Uamuzi wa Mhakama ya Rufani ilisomwa jana baada ya kusikilizwa na jopo la majaji saba liloketi chini ya Jaji Mkuu Augustino Ramadhan, Jaji Eusebia Munuo, Januari Msofe, Nathania Kimaro, Dk. Stephen Bwana, Mbarouk Salim na Benard Ruanda, Februari 8, mwaka huu.
  Kabla ya kusoma hukumu, Jaji Ramadhan alisema uamuzi huo unatokana na mchango uliotolewa na majaji wote saba na kwamba kwa bahati mbaya Jaji Salim hakuwepo kutokana na kuwa mkoani Tabora kikazi.
  Jaji Ramadhan alisema baada ya kupitia madai ya pande zote mbili, mrufaa serikali na Mtikila, jopo hilo limeona kwamba suala hilo linatakiwa kushughulikiwa na Bunge ambalo ni chombo kinachotunga sheria na kwamba lina mamlaka ya kufanya mabadiliko.
  Mbali na mahakama hiyo kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, imeamuru pande zote mbili kujilipia gharama za kesi hiyo. Rufaa hiyo namba 45 ya mwaka jana, inaeleza kwamba serikali iliwasilisha rufaa hiyo mahakamani hapo ikipinga hukumu ya iliyotolewa na waliokuwa majaji wa Mahakama Kuu, Jaji Mstaafu Amir Manento, Salum Massati, sasa Jaji wa Mahakama ya Rufani na Thomas Mihayo (Mstaafu), ambao walikubaliana na ombi na Mtikila na kuruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi.
  Awali, katika usikilizwaji wa rufaa hiyo, serikali iliendelea kung’ang’ania msimamo wa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu unaoruhusu kuwapo mgombea binafsi katika chaguzi za kisiasa, Jamhuri iliwakilishwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju.
  Akitoa hoja zake wakili Masaju, alidai kuwa mahakama ilikosea kufikia uamuzi wa kuruhusu kuwapo kwa mgombea binafsi, kwa madai kwamba haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi inayohusu Katiba ya nchi na kwamba mahakama imepewa mamlaka kisheria kusikiliza tu kesi zinazohusu sheria nyingine au vitendo vyovyote vinavyokiuka Katiba na si Katiba.
  Masaju aliendelea kudai kuwa mahakama haina mamlaka ya kutengua Katiba ya nchi kama ilivyofanya katika uamuzi wake na kwamba, ilikosea kuamua shauri hilo kwa kuzingatia sheria za kimataifa za haki za binadamu, wakati Katiba ya mwaka 1977 ina kifungu kinachoipa mahakama mamlaka ya kuamua.
  Masaju aliliomba jopo la majaji hao kutengua uamuzi huo wa Mahakama Kuu kwa madai kwamba, haukujengwa kwa misingi inayokubalika kisheria.
  Akijibu hoja hizo, wakili wa mrufaniwa, Richard Rweyongeza alidai hoja zilizotolewa na upande wa mrufani, hazina msingi, kwani malalamiko ya kutumia sheria za kimataifa za haki za binadamu, yameelekezwa kwa mahakama bila sababu yoyote.
  Baadaye Mahakama ya Rufani iliwaalika marafiki wa Mahakama, ambao ni Maprofesa Kalamagamba Kabudi na Jwani Mwaikusa, ambao ni wahadhiri wa sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mkurugenzi wa Mashtaka wa Zanzibar, Othman Masoud na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Rajab Kiravu.
  Wakati wa kutoa hoja zao Aprili 8, mwaka huu walitofautiana kuhusiana na mhimili wenye mamlaka ya kubadili katiba.
  Profesa Kabudi na Masoud walisema kuwa Mahakama haina uwezo huo bali Bunge wakati Profesa Mwaikusa alisema kwa mujibu wa mgawanyo wa madaraka miongoni mwa mihimili ya dola, Mahakama ina uwezo wa kuamua kuhusu katiba.
  Kwa upande wake, Kiravu alilieleza kuwa uamuzi wowote utakaotolewa na Mahakama ya Rufaa kukubaliana na ule uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania kuruhusu mgombea binafsi, utaathiri uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
  Mara ya kwanza, serikali ilikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu, katika Mahakama hiyo ya Rufaa mwaka 2007, kwa madai kuwa mahakama hiyo ya chini ilikosea kisheria kutafsiri Ibara ya 21(1) (c), 39 (1) (c) (b) na 69 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo, rufaa hiyo ilitupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa baada ya kukubaliana na ombi la wakili wa Mtikila, Rweyongeza kwamba rufaa hiyo haina msingi na kwamba imejaa dosari za kisheria.
  Awali, katika hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa Mei, mwaka 2006, ililiruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi, kwa sababu Katiba ya nchi inatoa haki hiyo.
  Mapema Mwaka 1993, Mtikila alishinda kesi kama hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, lakini licha ya uamuzi huo wa mahakama, Bunge lilishindwa kutunga sheria ya kuruhusu mgombea binafsi hivyo alifungua kesi hiyo ya kikatiba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo alishindwa tena. Akiongea na waandishi habari baada ya hukumu hiyo, Mtikila alisema hajakubaliana na hukumu iliyotolewa na jopo hilo na kwamba mahakama haijatenda haki kwa wananchi.

  Waishangaa hukumu
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, alisema kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania na historia ya haki za binadamu duniani mahakama yenye mamlaka ya juu imejitia kitanzi yenyewe.
  Alisema huo ndio mwisho wa uhuru wa mahakama Tanzania, lakini akasema Watanzania hawana sababu ya kukata tamaa kufuatia uamuzi huo.
  Dk. Mvungi alisema mahakama kwa kusema kuwa haina uwezo wa kutafsiri Katiba na kuruhusu mgombea binafsi imejitumbukiza kaburini kwa hiyari yake yenyewe.
  “Katika hili hatuangalii suala la mgombea binafsi pekee tunaangalia uwezo wa mahakama wa kutafsiri Katiba ambayo inalinda haki za binadamu…Mahakama inapaswa kujua kuwa haki za binadamu zilitangulia kabla ya mahakama na dola na haki hizo za binadamu haziundwi na Katiba bali Katiba yenyewe inazitambua tu,” alisema.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema ameshtushwa na uamuzi huo na kusema kuwa inaonyesha kuwa kuna haja ya kuandika Katiba mpya itakayojali demokrasia zaidi.
  Alisema ameshangazwa kusikia mahakama hiyo ikijivua wajibu wake wakati ndiyo inawajibika kutafsiri Katiba na sheria mbalimbali za nchi.
  Lipumba alisema Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu kunakatisha tamaa na kunashusha hadhi ya mahakama hizo za juu.
  Mkurugenzi wa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Erasto Tumbo, alisema hakutarajia uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Rufaa kwani kufanya hivyo ni kuinyonga demokrasia kwa makusudi. Alisema kama mahakama hiyo ya juu kuliko zote inasema kuwa haina uwezo wa kutafsiri Katiba basi kuna tatizo kubwa ambalo lazima lishughulikiwe.
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema mgombea binafsi ni haki ya kila Mtanzania iliyomo ndani ya Katiba hivyo haoni sababu ya serikali kuwa na kigugumizi.
  Alisema kila Mtanzania ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa hivyo suala la mgombea binafsi halihitaji mjadala mrefu kama inavyoendelea sasa.
  “Lazima tufikiri upya namna ya kuwatendea haki wananchi tuangalie haki zao za kushiriki chaguzi wakiwa wagombea ama wapiga kura bila kuwa katika chama chochote,” alisema Dk. Bana.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...