Kuna haja gani ya kuwa na GPSA wakati kuna PPRA?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
WAKALA wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya mwaka 1997, kupitia katika agizo la uanzishwaji wa Wakala.
Agizo la uanzishwaji lilifanyiwa mabadiliko kupitia tangazo Na. 133 la Aprili 13, 2012 na kuzinduliwa Juni 16, 2008.
Jukumu la wakala huu ambao uko chini ya Wizara ya Fedha ni kununua, kuhifadhi na kusambaza vifaa vinavyohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya serikali.
Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya 2011 sura 410 na kanuni zake tangazo la Serikali Na. 446 la tarehe 20/12/2013.

Jukumu hilo linatekelezwa katika mifumo miwili, kununua vifaa kwa ajili ya kutunza na kuuza, kuandaa utaratibu wa ununuzi wa pamoja wa vifaa na huduma mtambuka kwa kutumia mikataba maalumu.

Serikali ilianza kufanya mabadiliko ya kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwa lengo la kuhakikisha umma unapata huduma bora.
“Sekta ya ununuzi kama zilivyo sekta nyingine ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi yoyote ile. Sekta hii ndiyo inayowezesha upatikanaji wa vifaa, mitambo, kazi za ujenzi, huduma za ushauri na zisizo za ushauri kutoka kwa wauzaji, watengenezaji, makandarasi, wataalamu wa ushauri na watoa huduma,” anasema Mwambega.
Sekta hiyo ni kiungo muhimu kati ya muhitaji na muuzaji wa vifaa, kazi au huduma na ni mhimili mkubwa wa ukuzaji wa biashara ndani ya nchi na kati ya nchi moja na nyingine.
“Ununuzi huchangia katika upatikanaji wa ajira na uwezeshaji katika kutoa huduma za kijamii kama elimu, afya na maji.
“Takwimu zinaonesha kuwa ununuzi wa umma katika Tanzania unakadiriwa kutumia asilimia 70 hadi 80 ya bajeti ya serikali,”

Serikali ilianzisha Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini kwa malengo matatu ambayo ni kupunguza gharama za ununuzi katika sekta ya umma, kuongeza ufanisi wa Serikali kwa kuziwezesha taasisi kupata mahitaji yake ya vifaa na huduma zenye ubora na katika ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

UKWELI KUHUSU GPSA
1.Hana akiba ya bidhaa yoyote
2.Wakati bei ya mafuta ikiwa imepungua 1890 petrol kwa lita,GPSA anauza kwa 2500 lita moja ya petrol
3.Photocopy ni 100 hadi 200 GPSA ni 500 ukurasa mmoja
4.Wakati serikali imeagiza bei ya sukari iwe 1800Kg yeye GPSA anaelekeza bei iwe 2500Kg
GPSA kushindwa kufanya kazi kwa mujibu wa malengo yake ni matokeo ya serikali kuwa na taasisi nyingi zinazofanya kazi moja,kuna haja gani ya kuwa na GPSA wakati kuna PPRA?
By Nanyaro Ephata
 
PPRA inajihusisha na kuangali procurement regulation kwa gvt entities, GPSA anahusika na kuuza baadhi ya vitu kwa govt entities na kusajili makapuni yanayotaka kufanya kazi na serikali(kuuzia serikali huduma au bidhaa na kutoa bei elekezi ya huduma hizo, mimi naona wanafanya kazi tofauti ( GPSA na PPRA)
 
Taasisi nyingi nchini ni sekta za kupigia dili tu, kama SSRA ingekuwa inafanya kazi kama majukumu yake yalivyo ainishwa ule ufisadi wa NSSF ungetoka wapi? Mashirika ya pensheni kushindwa kuwalipa wastaafu na SSRA ipo ina maanisha nini? RITA na NIDA zote mbili za nini kama si huo ufisadi kwa nini RITA wasingepewa jukumu la kutoa vitambulisho vya taifa? Nchi hii kila mara mashirika yanaanzishwa ili kujipa ulaji hayana tija kwa taifa kabisa.
 
Itakuchukua muda mrefu na msuli mkubwa sana kutetea uwepo wa GPSA. Kwa ujumla ni sehemu mojawapo ya kuongeza urasimu katika manunuzi ya umma.
 
Mh!! kazi ipo tena sana tuu; hebu ngoja kwanza nimalizie maziwa yangu ndo nirudi.
 
WAKALA wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya mwaka 1997, kupitia katika agizo la uanzishwaji wa Wakala.
Agizo la uanzishwaji lilifanyiwa mabadiliko kupitia tangazo Na. 133 la Aprili 13, 2012 na kuzinduliwa Juni 16, 2008.
Jukumu la wakala huu ambao uko chini ya Wizara ya Fedha ni kununua, kuhifadhi na kusambaza vifaa vinavyohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya serikali.
Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya 2011 sura 410 na kanuni zake tangazo la Serikali Na. 446 la tarehe 20/12/2013.

Jukumu hilo linatekelezwa katika mifumo miwili, kununua vifaa kwa ajili ya kutunza na kuuza, kuandaa utaratibu wa ununuzi wa pamoja wa vifaa na huduma mtambuka kwa kutumia mikataba maalumu.

Serikali ilianza kufanya mabadiliko ya kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwa lengo la kuhakikisha umma unapata huduma bora.
“Sekta ya ununuzi kama zilivyo sekta nyingine ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi yoyote ile. Sekta hii ndiyo inayowezesha upatikanaji wa vifaa, mitambo, kazi za ujenzi, huduma za ushauri na zisizo za ushauri kutoka kwa wauzaji, watengenezaji, makandarasi, wataalamu wa ushauri na watoa huduma,” anasema Mwambega.
Sekta hiyo ni kiungo muhimu kati ya muhitaji na muuzaji wa vifaa, kazi au huduma na ni mhimili mkubwa wa ukuzaji wa biashara ndani ya nchi na kati ya nchi moja na nyingine.
“Ununuzi huchangia katika upatikanaji wa ajira na uwezeshaji katika kutoa huduma za kijamii kama elimu, afya na maji.
“Takwimu zinaonesha kuwa ununuzi wa umma katika Tanzania unakadiriwa kutumia asilimia 70 hadi 80 ya bajeti ya serikali,”

Serikali ilianzisha Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini kwa malengo matatu ambayo ni kupunguza gharama za ununuzi katika sekta ya umma, kuongeza ufanisi wa Serikali kwa kuziwezesha taasisi kupata mahitaji yake ya vifaa na huduma zenye ubora na katika ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

UKWELI KUHUSU GPSA
1.Hana akiba ya bidhaa yoyote
2.Wakati bei ya mafuta ikiwa imepungua 1890 petrol kwa lita,GPSA anauza kwa 2500 lita moja ya petrol
3.Photocopy ni 100 hadi 200 GPSA ni 500 ukurasa mmoja
4.Wakati serikali imeagiza bei ya sukari iwe 1800Kg yeye GPSA anaelekeza bei iwe 2500Kg
GPSA kushindwa kufanya kazi kwa mujibu wa malengo yake ni matokeo ya serikali kuwa na taasisi nyingi zinazofanya kazi moja,kuna haja gani ya kuwa na GPSA wakati kuna PPRA?
By Nanyaro Ephata
TBS na TFDA, EWURA n.k
 
Back
Top Bottom