Nyankuru Wankuru
JF-Expert Member
- Apr 22, 2018
- 1,199
- 1,346
Utakuta mkuu wa idara kwenye hizi halmashauri zetu analipwa mshahara wa 'leaders scale' pamoja na house allowance, electricity allowance, communication allowance, usafiri pia anapewa na kazi anayofanya ni kukaa tuu ofisini na kusaini mafile pamoja na kupitia mihutasari iliyoandaliwa na wasaidizi wake.
Mara nyingine hawa wakuu wa idara wanakuwa hawana hata aibu , unakuta anakwambia hebu wapigie fulani na fulani simu walete taarifa fulani tuinganishe na kujisahaulisha kuwa yeye anapewa communication allowance kila mwezi.
Lakini pia utakuta watumishi hawa wa chini muda wote wako bize na kazi, mara waende field, warudi waandike taarifa, mara wafuatilie utekelezaji wa maagizo ya viongozi sasa ukiona mshahara anaopata unaweza kutoa machozi.
Sasa mtu anapewa mshahara mkubwa na allowance nyingi sasa ni kwanini mtu huyo huyo awe na wasaidizi wake?.
Ni bora mtu kama huyo akaachiwa idara nzima afanye kazi mwenyewe kuliko kuwa na wasaidizi wake. Maana mshahara anaoupata ni mkubwa sana kuliko kazi anazofanya kwa siku.
Na wengine ukienda kwenye sehemu za kunywa chai na chakula (mama lishe) utawakuta wanapiga story tu huku wakitumia muda mwingi huko.
Serikali kwenye hili mlifanyie kazi, pesa nyingi za walipa kodi zinapotea kwa kuwalipa watu wasio kuwa na majukumu mazito huku maofisini. Hasa kwenye Halmashauri na Ofisi za wakuu wa mikoa.
Na pia siku hizi wakuu wa idara nyingi wamekuwa wajanja sanaa, utakuta wamerundika mifaili juu ya meza kwa muda mrefu kuzuga ili waonekane kuwa wameelemewa na kazi kumbe ni geresha tu.
Vile vile, kwa kuongeza ufanisi kwenye hizi halmashauri zetu na ofisi za wakuu wa mikoa ni vyema sasa serikali ikaja na mfumo wa electronic wa mafaili ( e- file management information system) mfumo wa namna hii itasaidia kujua file linachukua muda mwingi kwa Mkuu wa idara gani na kwa afisa gani.
Asante
Sent using Jamii Forums mobile app