Kuna faida nyingi zaidi kwenye muungano

cheusimangala_

Senior Member
Dec 1, 2018
114
174
ob_37006e_muungano.jpg

WATANZANIA tunaadhimisha muungano ikiwa ni hatua madhubuti ya kuenzi jitihada zilizotekelezwa na waasisi wa taifa hili, marehemu mzee Abeid Amani Karume na hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Siku ya muungano inaadhimishwa kutafakari mafanikio kutokana na tendo la muungano na changamoto tulizokabiliana nazo hadi hatua hii na hatimae kujipanga vizuri zaidi katika kuenzi na kuendeleza dhana ya muungano katika kipindi kingine cha miaka 50 ijayo na kuendelea, sote tukiwa na nia njema.

Sote ni mashahidi kwamba kitendo cha muungano umekua chachu kubwa ya maendeleo, amani, utulivu na mshikamano, ingawa bado kuna changamoto ambazo zimeshindikana kupatiwa ufumbuzi katika kipindi cha miaka 50 ya muungano huo.

Nitumie fursa hii kuwatanabahisha wananchi kwamba katika karne hii ambayo uchumi unaongozwa na ushindani kutokana na mfumo wa utandawazi unaoigeuza dunia kuwa sawa na kijiji, ushirikiano hauepukiki.

Na taifa lolote litakalopuuza ushirikiano linajiandalia mazingira ya kushindwa katika mfumo wa utandawazi unaoongozwa na ushindani wa kimataifa na hatimae kuparaganyika kabisa.

Muungano ni hatua muhimu ya kuelekea katika ushirikiano wa dhati katika kuimarisha uchumi na maendeleo ya wananchi wa pande mbili.

Aidha muungano unatoa fursa za kiuchumi kwa Tanganyika na Zanzibar kupanua masoko za bidhaa zake na huduma, kuimarisha sekta za uzalishaji, kuongeza ajira, kuimarisha miundombinu na hivyo kujijenga kiushindani.

Pia muungano huu unalenga kuendeleza ujirani mwema uliopo baina ya Watanganyika na Wazanzibari.

Hivyo, watanzania wanapoadhimisha miaka 54 ya muungano, lazima watafakari kwa kina mafanikio yote yaliyopatikana ili yaendelezwe katika kipindi cha miaka mingine, lakini pia waanishe kero zote zinazolalamikiwa na wananchi hasa kwa Zanzibar zinatatuliwa.

Katika kipindi cha miaka 54 iliyopita, watanzania wameshuhudia mengi mazuri yaliyolenga kuimarisha umoja wa wananchi na uchumi wa kila upande, lakini pia malalamiko mengi tayari yamepatiwa ufumbuzi.

Naamini siku ya muungano watanzania wataitumia kutafakari zaidi namna kuuimarisha muungano wetu ambao umekuwa mfano wa kipekee sio barani Afrika bali hata duniani.

Kwa sababu tumeungana changamoto hazitokosekana na kila tunavyoendelea kuwa kwenye muungano changamoto hizo zinaweza kujitokeza zaidi.

Hata hivyo, faifa za muungano huu ni nyingi kuliko kero ambazo zipo, nadhani tufikie kwenda mbele zaidi ili malengo yaliyowekwa na waasisi wetu yaweze kufikiwa.

Nadhani pia serikali zichukue juhudi kuhakikisha zinaifikishia jamii elimu ya muungano sio kwa wananchi pekee kwani hata baadhi ya viongozi wakiwemo wabunge hawautambui huo muungano.
 
Tunataka urais wa kupokezana.Wanzazibari kwisha habari yao- bonge la raw deal.
 
Hivi kwanini tanganyika haijatafuta mshirika mwengine wa muungano huu zaid ya miaka hamsini sasa mnailazimisha zanzibar tu kwenye huu mnaoita muungano?ipo kenya,uganda,burundi lakin huko kote hamuendi kutafuta muungano.Acheni hizo bhana mambo ukoloni yamepitwa na wakati.
 
View attachment 1245176

WATANZANIA tunaadhimisha muungano ikiwa ni hatua madhubuti ya kuenzi jitihada zilizotekelezwa na waasisi wa taifa hili, marehemu mzee Abeid Amani Karume na hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Siku ya muungano inaadhimishwa kutafakari mafanikio kutokana na tendo la muungano na changamoto tulizokabiliana nazo hadi hatua hii na hatimae kujipanga vizuri zaidi katika kuenzi na kuendeleza dhana ya muungano katika kipindi kingine cha miaka 50 ijayo na kuendelea, sote tukiwa na nia njema.

Sote ni mashahidi kwamba kitendo cha muungano umekua chachu kubwa ya maendeleo, amani, utulivu na mshikamano, ingawa bado kuna changamoto ambazo zimeshindikana kupatiwa ufumbuzi katika kipindi cha miaka 50 ya muungano huo.

Nitumie fursa hii kuwatanabahisha wananchi kwamba katika karne hii ambayo uchumi unaongozwa na ushindani kutokana na mfumo wa utandawazi unaoigeuza dunia kuwa sawa na kijiji, ushirikiano hauepukiki.

Na taifa lolote litakalopuuza ushirikiano linajiandalia mazingira ya kushindwa katika mfumo wa utandawazi unaoongozwa na ushindani wa kimataifa na hatimae kuparaganyika kabisa.

Muungano ni hatua muhimu ya kuelekea katika ushirikiano wa dhati katika kuimarisha uchumi na maendeleo ya wananchi wa pande mbili.

Aidha muungano unatoa fursa za kiuchumi kwa Tanganyika na Zanzibar kupanua masoko za bidhaa zake na huduma, kuimarisha sekta za uzalishaji, kuongeza ajira, kuimarisha miundombinu na hivyo kujijenga kiushindani.

Pia muungano huu unalenga kuendeleza ujirani mwema uliopo baina ya Watanganyika na Wazanzibari.

Hivyo, watanzania wanapoadhimisha miaka 54 ya muungano, lazima watafakari kwa kina mafanikio yote yaliyopatikana ili yaendelezwe katika kipindi cha miaka mingine, lakini pia waanishe kero zote zinazolalamikiwa na wananchi hasa kwa Zanzibar zinatatuliwa.

Katika kipindi cha miaka 54 iliyopita, watanzania wameshuhudia mengi mazuri yaliyolenga kuimarisha umoja wa wananchi na uchumi wa kila upande, lakini pia malalamiko mengi tayari yamepatiwa ufumbuzi.

Naamini siku ya muungano watanzania wataitumia kutafakari zaidi namna kuuimarisha muungano wetu ambao umekuwa mfano wa kipekee sio barani Afrika bali hata duniani.

Kwa sababu tumeungana changamoto hazitokosekana na kila tunavyoendelea kuwa kwenye muungano changamoto hizo zinaweza kujitokeza zaidi.

Hata hivyo, faifa za muungano huu ni nyingi kuliko kero ambazo zipo, nadhani tufikie kwenda mbele zaidi ili malengo yaliyowekwa na waasisi wetu yaweze kufikiwa.

Nadhani pia serikali zichukue juhudi kuhakikisha zinaifikishia jamii elimu ya muungano sio kwa wananchi pekee kwani hata baadhi ya viongozi wakiwemo wabunge hawautambui huo muungano.
tujifunze kwa viongozi waasisi, kwa nini utengue maamyzi ya wazazi wako unatafuta laana
 
Back
Top Bottom