Kuna faida gani za kuitwa mtanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna faida gani za kuitwa mtanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nalonga, Dec 29, 2010.

 1. N

  Nalonga JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Naandika ili wanajamii nikiwa na maswali tele kichwani ya nini cha kujivunia kwa mimi kuitwa mtanzania?nimeona nitumie jamvi hili ili ndugu muweze kunisaidia kujibu baadhi ya maswali yanayonitatiza.matatizo mengi yanayotukabili watanzania wengi wa kipato cha chini na chakati ni ya kijamii(social problems),sasa basi naomba mnijuze wajuzi wa hili ni social benefit zipi za kujivunia kwa mimi mtanzania? Au ule msemo wa vijana waliokata tamaa za kuishi tanzania is valid? Yaani..."better born dog in europe than being born in tanzania?"....nisaidieni wajuzi!
   
 2. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,068
  Likes Received: 786
  Trophy Points: 280
  Craaaap!!!!greet thinkaz!!!!
   
 3. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mkuu, nashauri take a deep breath, and drink a cold beer, halafu punguza jazba. Najua hali ya mambo mengi ta bongo inakatisha tamaa sana lakini ndio hivyo ni nchi yetu. There's an old saying "Mama yako ni mama yako tu hata ufanyaje, hata uhamie ulaya ama uoe/kuolewa na mzungu, wote sisi ni waafrika/watz. Cha msingi ni kuelimisha jamii na kuondoa huu mgando wa akili unaotukabili wabongo. Tukishauana na hali ya hewa kuchafuka then ndio politicians wataona watu tuko serious otherwise upole na amani ndio uliotufikisha hapa wadanganyika.
  Naomba uende paleeee Maryland Pub ukapate bia mbili then utapunguza jazba. pole mkuu:whoo:
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Basi subiri uraia popo uruhusiwe ili uwe nazo mbili, kama huwezi you can just deny it!
   
 5. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Elimu ya uraia inahitajika hapa..ni utelezi wa Fikra kutamani kuzaliwa ulaya ukiwa mbwa kuliko Tanzania(nyumbani)...sina hakika na umri wako ila nashawishika kudhani kua si enzi za ndumaro.
  Dhana yangu ni kwamba ili nchi iweze kusimama kiuchumi,kimaamuzi na nyanja nyingine muhimu inapita ktk vipindi vigumu na vya kuogofya ikiwa ni pamoja na kukatisha tamaa kwa wenye mioyo dhaifu,lakini tutakaovumilia mpaka mwisho ndio tutakua wana wema wa nchi,na tutakumbukwa na vizazi vitakavyokuja baadae...NAJIVUNIA KUWA MTANZANIA!
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Utanzania == Mineno mengi
   
 7. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Aisee hili ni swali la ukweli kabisa umeuliza...!

  Nimekua nikijiuliza hili swali pia kwa sababu kwa hali ilivo sasa sijui ni lini tutaweza kuwa na social benefit ambazo ni za uhakika. Kutokuwepo kwa social benefits za uhakika (elimu, Afya, maji, ulinzi, pamoja na elimu ya uraia) ndio chanzo kikubwa sana cha kuzaliwa kwa ufisadi.

  Ufisaidi unatokana na ubinafsi, ubinafsi unasababishwa na kukosekana kwa social benefits za uhakika so kinachotokea ni kwamba mtu anadiriki kuiba mali ya umma ili aweze kumudu maisha au kuweza kupata social benefits zinazokidhi matakwa yake.

  Hebu angalia chanzo cha rushwa, moja ya sababu kubwa ni kipato kidogo ambacho kinafanya mtu asiweze kulipia gharama kubwa za maisha. Kwa kweli, mpka sasa naona inakua ngumu sana kuona faida ya kuwa mtanzania haswa kuwa mtanzania wa kawaida kutokana na kuendelea kwa vitendo vya rushwa, ufisadi, wizi na unyang'anyi (kuvamiwa usiku majumbani na majambazi), kukosekana kwa huduma bora (elimu, afya, umeme, maji, barabara, n.k) kwa sehemu kubwa ya jamii.

  Hivi leo hii tuko karne ya 21 bado upatikanaji wa umeme ni issue? Watu wanaishije bila maji? Usafiri bado ni wa kupigania na kuingilia kwenye mabasi madirishani?

  Hii ndio inaishia na conclusion yako kwamba
  "better born dog in Europe than being born in Tanzania?" Walau hata mbwa wanahaki za wanyama huko ulaya
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Nalonga,

  Pole sana kwa kutumia muda mwingi kujiuliza masuali hayo.
  Unataka kujuwa utanzania una faida gani.

  Well, m-PM member Buchanan atakuelezea faida at least 5 za utanzania.

  Mimi sijui kama utanzania una faida au hasara, ila nililo na uhakika nalo ni kuwa utanzania unaendana na sifa ya ukondoo. Tokea enzi za Mwalimu, lakini sasa ndio yamezidi tu,kuna ukondoo, rushwa ya kutisha na ufisadi. Hata Hosea anahofia maisha yake!

  Pili, kwa uzoefu wangu ninaposafiria pasi ya Tanzania basi huwa napata tabu sana katika viwanja vya ndege, huonekana kama jambazi hivi.

  Tatu, nakubaliana na Abdulhalim kuwa utanzania ni mineno mingi.

  Hata askari wakenya wakikukamata wakijua kuwe wewe ni mtanzania basi hawakupi nafasi ya kujitetea, ni kisago tu,wanajua wakikupa nafasi ya kujitetea utawashinda.
  Huwa wanasema “Iii mtu ya Tanzania iko maneno mingi”
  Kwa hiyo, kwa mtu wa kawaida ni tabu sana kusema utanzania una faida.

  Kwa watu wachache utanzania kwao ni lulu, ni kitambulisho cha kuwawezesha kuvuna shamba la bibi. Hawa watakuorodheshea faida elfu na moja za utanzania.
  Hata hivyo uelewe kuwa kuanzia tarehe 29 oktoba 1964, Nchi yetu ilibadili jina na kuitwa Tanzania na kila raia wa Tanganyika automatically akajipatia utaifa mpya wa Utanzania.

  Kwa hiyo utanzania ni utambulisho tu kuwa wewe ni raia wa hii nchi iitwayo Tanzania. Fiada ya utanzania kama unaishi hapa nchini ( kama wewe si katika wale wachache) basi ni kakumuliwa maziwa, yaani kulipishwa kodi ili watu wanunue VX.

  Kama uko nje, basi faida ni kujisifia kwa wenyeji wako huko uliko kuwa Mlima Kilimanjaro uko Tanzania na wewe ni mtanzania.

  Natumai nimekusaidia japo kidogo, japo kwa kukufanya ufikiri zaidi.
   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Tesha,

  Sawa mkuu unajivunia utanzania, nafikiri wengi wetu tuko hivyo. Lakini hujamsaidia sana ndugu Nalonga, yeye anataka kujua faida ya utanzania kwa mtu wa kawaida.
  Au hujamfahamu??

  Hilo la kuwa mbwa ulaya ni katika masuali ambayo pengine kwa kukatishwa tama a na utendaji wa serikali ndio hukumbuka huo msema na kujiuliza jee ni kweli bora hilo la kuwa mbwa ulaya??.

  Nalonga yuko na mawazo mengi na anahitaji msaada kabla hajaanza kupiga makelele na kuokota makopo mitaani.
  Watanzania wengi tuko kama Nalonga. Tusaidiane mawazo.

  Hata ukiangalia michango ya watu humu JF hilo linajidhihirisha wazi. Yeye amepata ujasiri anatafuta msaada.
   
 10. shanature

  shanature JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 718
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  3-0 mjinga,,,,,,,,,,,,,maskini,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,unachekelea ufisadi --------------0
   
 11. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Actually binafsi ubongo una stack kila nikiwaza nchi yangu jinsi mambo yanavyojiendea tu as if hakuna wenye dhamana wanaoliona hili..kwa aina hii ya utendaji wengi tutakua na maswali mengi kuzidi majibu...ndo km haya ya kujivunjia tu sheria,tena kwa kugharimu uhai wa wanadamu wenzio halafu marafiki wanajisachi wanachanga 700,00/= kesho unakua huru kuvunja tena sheria na kejeli kem kem! ....mkuu Nalonga bora kua na hangover muda wote ili usiwaze yanayotendeka wazi wazi! Lakini najua Tanzania yetu tutaikomboa wenyewe na tazama utajivunia heshima uliyokwisha jikatia tamaa!
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu it may sounds crap. But for sure it is not, because it came out of deep sense of love to Tanzania, deep connection to the land and deep thoughts. Moyo wa kuipenda Tanzania unawafanya watanzania waoneshe hasira nchi yao inapokwenda ovyo. Bongo iko ovyo na inazidi kuwa ovyo no doubt, na wa kumlaumu si JK, ni sisi watanzania wenyewe tunaitelekeza Tanzania kwa kutake things for granted, au kwa kuhope kuwa itakuja badilika yenyewe.

  Ni vizuri kujiuliza what is the difference between being a foreigner and a Tanzanian? ni kutohitaji residence permit tu? au kuna tunayobenefit zaidi ya hapo. How is Kenyan in Tanzania different from a Tanzanian in Tanzania. How will i feel sad to be out of Tanzania? just missing my friends???
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Bongo ukiwa 'mgeni' na kingereza cha uongo na kweli hata totozz utapiga za kumwaga tu..(joke).

  IMO ukiwa bongo wewe kama mtz, unakuwa raia wa daraja la 2..ka-syndrome ka kubabaikia wageni kanakua kwa kasi sana. Na mbaya zaidi kataathiri vibaya sana mustakabali wa vizazi vijavyo achilia mbali msoto wa hivi sasa.

  Kwa kuongezea ukitaka kwenda nje ya nchi utapigwa danadana za viza na still utailipia. Uraia wa dunia ya kwanza ungekuwa unanunuliwa tusingepata hizi shurba..

  Nchi nyingine ukiwa raia unapata favors za hapa na pale, kama kupata punguzo kwene National Airlines, etc sisi hivi vitu kwetu ni sawa na ku-travel through time machine.
   
 14. n

  nyantella JF-Expert Member

  #14
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Nafikiri una mtindio wa ubongo. Si uhame tu uende ukawe "umbwa" huko Europe? kwea pipa and go useless brain!
   
 15. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #15
  Dec 30, 2010
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  Nchi hii inauma wajameni hakuna faida yoyote ya kuwa mtanzania zaidi ya kuongea kiswahili fasaha na kuishi katika dunia ambayo ni informal yaani kuanzia TRA, Immigration, housing system, shops/viosks, wizarani, mikataba feki (Dowans) ni vitu unique kwa nchi hii hakuna viongozi kusimamishwa kwa rushwa, kazi zinatolewa kwa kujuana, hakuna malengo hata ya maika 10, kila leo noti zinabadilishwa watu wapate mwanya wa kuchukua fedha zao, kila kiongozi anakuja na lake kwa kifupi ni nchi ya kijinga afrika....Madini ndio kabisa tumewapa wachimbe alafu sisi tunawalipa wao (VAT)....Mimi kama mtanzania naona ni bora nikaishi nchi nyingine yenye dira na lengo na kuthamini raia wake angalau hata kwa barabra na social services nyingine kuliko kuishi katika nchi ambayo inaongozwa na genge la watu ambao wanadhani wataishi milele hivyo wanachuma tu hawafikirii vitukuu vyao vitaishi wapi vitakula nini???? inauma lakini ndio hivyo wakenya, waruanda wako mbali mno wanatuona punguani kumrudisha mtalii madarakani....I hate being Tanzanian!
   
 16. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #16
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndugu,

  Hili swali la faida ya kuwa mtanzania ni swali muhimu mno kwa jamii na kizazi cha leo. Mimi mwenyewe nimekua nikijiuliza kila kukicha ni faida gani napata kwa kuwa mtanzania lakini sioni. Haya ndio maswali muhimu kuhusu utaifa ambayo inabidi yaanze kujibiwa na vionhozi wetu.

  Kwa kweli, naomba ajitokeze mtu walau anisaidie japo kujibu hoja hii...! Anafaidikaje kuwa mtanzania wakati hakuna maji kwenye bomba, elimu wanafunzi wanakaa chini, hospitali hakuna na kama zipo ni mbovu, mahakamani haki ni ya kununua, ufisadi ulio kidhiri Serikalini, wizi wa mali za umma, umeme wa gharama, gesi vile vile gharama, wizi na uhalifu uliokidhiri mitaani, barabara mbovu etc...! Bora mbwa ulaya, anapata nafasi ya kulala kwa raha, anaogeshwa, anaenda hospitali kwa docta (veterinary)...!
   
Loading...