Kuna faida gani ya nchi kuweka vituo vya kijeshi (base) nchi nyingine?

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Wana jf
salaam

Mara nyingine nimekua nikisikia nchi kadhaa kuanzisha vituo vya kijeshi katika nchi nyingine (Military Bases) mfano Marekani wana vituo vingi sana vya kijeshi katika nchi kadhaa duniani kuanzia Ufilipino, Kuwait, Afghanstan na nyingine, je kuna faida gani au hasara gani kuanzisha hivyo vituo je sheria za kimataifa zinatoa nafasi hiyo?
 
Hata mm nataka kujua pia hapa nchin kwetu kuna military bases za nchi zipi, na sisi nchi yetu imeweka military base nchi gani?
 
Maswali mengine ni ujinga!! Hauna bundle ugoogle? Acha kuonyesha ujinga!!! Mzungu kakurahisishia kila kitu kiko kiganjani kwako au mbele yako kwenye laptop hapo bado unaendekeza ujinga!! Waafrica tuna kazi sana!!! Au lugha ya malkia ni shida! Ila kuna translator so hata kama lugha ni shida itumie hiyo!

Basi sawa
 
unaonaje ungesoma tu na kupita kimya bila kutukana?
 
Ukiwa na military base nyingi,maana yake ni kuwa una uwezo mkubwa wa kuproject power,kwamaana ni kuwa majeshi yako yanaweza kuwa au kufika mahali pa tukio kwa mda mfupi sana na carry out operation kwa maslahi ya nchi husika,
=Power projection =force projection.

Disdvantage ni gharama sana kumaintain military base nje ya mipaka ya nchi yako,inahitaji hela nyingi na logistic kubwa
 
Wana jf
salaam

Mara nyingine nimekua nikisikia nchi kadhaa kuanzisha vituo vya kijeshi katika nchi nyingine (Military Bases) mfano Marekani wana vituo vingi sana vya kijeshi katika nchi kadhaa duniani kuanzia Ufilipino, Kuwait, Afghanstan na nyingine, je kuna faida gani au hasara gani kuanzisha hivyo vituo je sheria za kimataifa zinatoa nafasi hiyo?

Kwa ajili ya ulinzi wa vitega uchumi vyao.Mfano kuwaiti kuna makampuni kibao ya marekani.ULinzi wa kuwaiti hautoshi dhidi ya matishio ya magaidi nk ndio maana na wao wameweka.Hata Tanzania ilikuwa na vituo vya kijeshi msumbiji kwa ajili ya kuwashambulia wareno na makaburu waliokuwa wakitishia usalama wa mikoa ya kusini.Nchi inaweza weka kituo cja kijeshi popote karibu na adui yako.Mfano Tanzania ikiwa na uadui na Afrika ya kusini uadui mkali yaweza amua kuweka vituo vya kijeshi zimbabwe au namibia au nchi yoyote inayopakana na Afrika ya kusini ili kuwa na military advantage kukitokea chochote.Urusi pia walikuwa na vikosi vya kijeshi Cuba Ambapo ni karibu na aliyekuwa adui wao mkuu nchi ya marekani lengo likiwa kuwa marekani akianzisha vita na urusi wanambomoa kupitia CUBA.
 
Kiukweli baada ya vita vya pili vya dunia kuna nchi ziliomba majeshi ya USA kuendelea kubaki kwa kuwalinda na maadui wa nchi jirani,
Kwa mfano uwepo wa marekani hiko Japan na Ujerumani.
Pia ukiangalia Djibouti kuna military bases za wanajeshi kama 4000 wa Marekani na pia wapo Wafaransa wakilinda hapo.

Na sasa Wachina nao kwa mara ya kwanza wanaweka base Djibouti kwa kulinda maslahi yao kwa kuwa ndio njia kuu ya manowari kupita.
Saudi Arabia pia wanataka kuweka base hapo.
Inafika mahali nchi inakuwa haijitaji jeshi lake kuwa kubwa kwani wanalindwa kwa mfano German wamepunguza sana jeshi lao.

Ukiangalia upande USA kuweka majeshi kila kona ni kuweza kuwa karibu na tukio la vita. Kwa mfano wakati wa Saddam ndege za America zilikiwa zinatokea Ujerumani
 
Back
Top Bottom