Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 653
- 1,058
Ninavyojua mimi kuna nchi ambazo hazitaki kuhamia huko kwa sababu ukishakuwa huko unajiondoa kwenye kundi la nchi zinazotakiwa kusaidiwa na kupata misamaha baadhi na unahamia haraka kwenye kundi la nchi zinazokopesheka. Kwa maana hiyo Tanzania imepata sifa ya kuwa nchi ya kupata mikopo zaidi kuliko misaada.
Ukiangalia kwa undani nchi inayokopesheka ina maana ni nchi yenyewe inakopa na sio wananchi wanakopa. Tayari Tanzania ina deni kubwa sana ukilinganisha na awamu ya JK ilivyokuwa. Ukiangalia fedha zote ambazo Tanzania imekopa hazina athari chanya yeyote kwa wananchi wake wa kawaida.
Inasemekana huko nyuma Tanzania ilikuwa inasita kuingia kundi la nchi hizo kwa sababu ya kukwepa kuwa nchi inayokosa misaada. Nchi nyingine kama India pia nao waliwahi kujichelewesha kwenda kundi la nchi zinazoendelea ili wasikose misaada. Kwani kadri unavyokuwa ndivyo unavyoonesha huhitaji kusaidiwa. Kwa Tanzania wananchi bado wanahitaji kusaidiwa. Benki ya Dunia inafurahi tu kwa Tanzania kuhamia kundi hilo kwa sababu kwao wanapata mteja ambaye anajiamini kuwa ana uwezo wakati kiuhalisia ni hamna kitu kabisa hapo!