maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,344
Siku zote sikuwahi kujua wala kufikiri kwamba idadi ya viti maalum vya wanawake bungeni inaweza kufikia hii, yaani viti 110, kwa ujinga wangu nilidhani ni chini ya viti 50.
Lakini viti maalum 110, yaani karibu nusu ya wabunge wa kuchaguliwa ambayo namo bado kuna wanawake, kuingia akina mama wengine 110 kinamna ktk chombo nyeti cha kutunga sheria kama bunge naona kuna mushkeli mkubwa tena sana.
Kwa hatua tuliyofikia ya kutoa haki na vigezo vilivyo sawa kwa jinsia zote katika hatua zote za kugombania nafasi za udiwani, ubunge na urais, sioni kama tuna haja tena ya kuwa na viti vingi vya upendeleo kiasi hiki.
Nimejaribu kupekua na kupitia katiba za nchi wenzetu walio katika jumuiya ya madola ambayo na sisi ni mjumbe wa mabunge yake nimegundua kuwa Tanzania ndiyo nchi pekee yenye kuwa na idadi kubwa ya viti vya upendeleo kwa wanawake ndani ya bunge.
Fikiria mlolongo wa shida, matatizo na mdororo wa kiuchumi walionao watanzania lakini bado kuna wabunge 110 wanawake wamewekwa bungeni, wengine wakiwa wameingia tu kishikaji au kimahusiano binafsi kwa malipo ya kodi ya watanzania.
Fikiria pia madeni ya waalimu, ukosefu wa dawa hospitalini, madeni ya wakandarasi, ukosefu wa maji na mengine mengi lakini bado kuna wabunge wanalipwa bila ya kuwa na jimbo wanaloliwakilisha, wanabaki ni wa kudandia dandia tu hoja za wenzao bungeni na kutetea vyama vyao ndani ya bunge.
Nadhani wakati umefika sasa wa kuvipruni viti hivi na kubakiza viti 40 tu au kuvifuta kabisa na wanawake wanaotaka ubunge warudi kugombea kwenye majimbo yao badala ya kuvizia kutafuna kodi yetu huko bungeni bila kazi maalum. Binafsi sioni kama umuhimu wa wabunge hawa unalingana na mabilioni ya kodi yetu wanayotafuna.
Kama Tanzania tumefikia hatua ya mwanamke kugombea urais akashika nafasi ya tatu mbele ya wagombea wanaume watano, na hata kumpata makamo wa Rais mwana mama bado tunadhaniaje wanawake ni wa kupewa upendeleo?