Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
Nitatoa mfano, Kiwanda kinajengwa Tanzania, mwenye kiwanda anataka apewe tax holliday yaani aendeshe kiwanda bila ya kulipa kodi anapewa, anataka apunguziwe gharama ya umeme anapunguziwa, anaajiri vibarua, kibarua maana yake ni mfanyakazi ambaye analipwa kwa siku na asipokuja kesho labda kwa ugonjwa au hata ajali ajira kwisha anachukuwa mtu mwingine, hapo hapo mwenye Kiwanda anataka asilipe export tax kama akiuza bidhaa nje ya nchi na vile vile akiingiza bidha kwa matuminzi ya kiwanda chake pia anataka Serikali imuondolee import tax, sasa Nauliza kuna faida ya kuwa na hiki Kiwanda?