#COVID19 Kuna dalili kubwa sana za wagonjwa wengi wa Corona hapa Ifakara kata ya viwanja sitini kitongoji cha Minarani

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
6,725
2,000
Hatua za haraka zichukuliwe na viongozi na mamlaka zinazohusika na afya. Kuna idadi kubwa ya watu wenye mafua makali na vikohozi vikali. Wengine wakidai kusikia maumivu maeneo ya koo.

Hiyo hali mimi nilikutana nayo. Kichwa kuuma, maumivu kwenye koo ukimeza mate au chakula, mafua makali na kupiga chafya sana. Kwa sasa hiyo hali imeisha, nilidumu nayo kwa siku kama 10 hivi.

Nauhakika kabisa hii itakuwa ni korona. Mamlaka tembeleeni Ifakara viwanja Sitini Minarani.
 

Dr Mabuga 30

JF-Expert Member
May 8, 2021
300
500
Mjin
Hatua za haraka zichukuliwe na viongozi na mamlaka zinazohusika na afya. Kuna idadi kubwa ya watu wenye mafua makali na vikohozi vikali. Wengine wakidai kusikia maumivu maeneo ya koo...
Mjinga kweli wewe mafua Hayo bhana mimi nipo hapa kibaoni mbona ni hali ya kawaida Unaijua Corona wewe
 

Townchild

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
7,578
2,000
Hatua za haraka zichukuliwe na viongozi na mamlaka zinazohusika na afya. Kuna idadi kubwa ya watu wenye mafua makali na vikohozi vikali. Wengine wakidai kusikia maumivu maeneo ya koo...
Chukueni tahadhari za kujikinga zaidi,nawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni,epuka misongamano,au vaa barakoa kwenye misongamano ,na jitokeze kuchanjwa kituo cha karibu na ulipo.
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
18,986
2,000
Hali ya hewa imechafuka sana duniani mpaka tunashangaa
Kweli mafuriko na summer hii Ulaya?

Huko China kadhalika na Uturuki moto wa ajabu
Kwa sasa hali ya hewa ni sababu ya magonjwa mengi
 

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
6,725
2,000
Jamaa anataka atujengee hofu huyu!! Mimi niko huku Lipangalala, hakuna chochote!!
Kama upo serious kweli na upo hayo maeneo tembelea hiyo mitaa nayosema. Fika mpaka shule ya secondary Shungu. Uje umevaa barakoa. Usije pua juu kama mbwa wa polisi. Fanya mazungumzo na watu wa hayo maeneo.

Sio kila jambo ni mzaha mzaha.
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
25,575
2,000
Kwamba toka wakiwa watoto mpaka wanakomaa viungo hawajawahi kuugua makoo na mafua!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom