Katavi
Platinum Member
- Aug 31, 2009
- 41,983
- 12,701
Heshima wakuu...
Nauliza kama kuna chuo chochote hapa nchini kinachotoa mafunzo ya namna ya kuongea mbele ya kadamnasi. Hii inatokana na namna watu mbalimbali tulivyo waoga kuongea mbele ya watu hasa katika sherehe au msibani.
Kuna kisa kilinitokea msibani baada ya kumaliza kutoa heshima kwa mwili wa marehemu na kuwa tayari kusafirishwa, niliombwa nitoe neno la shukrani. Lakini niliweza kukwepa na kumtupia jamaa mmoja aliyekuwa jirani yangu, lakini kumbe yeye ndiye alikuwa mbovu kuliko mimi. Alianza kwa kusema "MSIBA OYEEE"......shukrani kwa mzee mmoja aliyeokoa jahazi.
Naombeni elimu ya namna ya kujiamini nisije kupatwa na aibu kama hiyo........