Kuna chanzo kizuri cha mapato, kwanini Serikali imelala? Manispaa na Majiji mifumo ya majitaka inawahusu hii

Kiume3000

Senior Member
May 17, 2021
180
218
Nilisoma nyuzi JF na nikapost juu ya mradi huu. Ni kitu cha kawaida Sana nchi za wenzetu kujenga mifumo ya maji taka kama ilivyo maji safi yanavyosambazwa huu mradi ni bomba sana.

Si lazima maeneo yote. Uswazi kuachwe kama kulivyo lakini maeneo ambayo yana ramani zinazoeleweka au hata squata ambako kuna njia za mtaani hii inawezekana kabisa.

Please please kama hamuwezi itengenegezeeni ✍️ muwape wanaoweza kuifanya.

ova
 
Huo mradi uko chini ya ya DAWASCO/DAWASA na wanaopata huduma wanailipia.

Bili ziko mbili ya maji safi na majitaka. Hii ya majitaka ni kwa wale waliounganishwa kwenye mtandao wa mamlaka ya maji ambao ni wazalishaji wakubwa wa majitaka.
 
Huo mradi uko chini ya ya DAWASCO/DAWASA na wanaopata huduma wanailipia.

Bili ziko mbili ya maji safi na majitaka. Hii ya majitaka ni kwa wale waliounganishwa kwenye mtandao wa mamlaka ya maji ambao ni wazalishaji wakubwa wa majitaka.
Ipo tayari kumbe...ookay
 
Hii mambo inahusu Sana mji kunuka

 
Hii mambo inahusu Sana mji kunuka

Taka ngumu ndio chanzo kikuu cha uvundo dar
 
Hata wale wanaofyonza majumbani ambako hamana muunganisho wa maji taka, zile gari husika hulipa kiasi cha fedha kule wanakoenda mwaga

Wanaoishi mashambani wallaaaa hawawazi hili, wanachimba kikijaa wanahamisha, kisha wanaotesha mgombaa ama mti wa mparachichi pembeni ya shimo lililojaa, baada ya miezi kadhaa wanakula matunda - ndizi/parachichi etc
 
Serikali yako sikivu imekusikia, tutarajie ongezeko la tozo ya maji taka kwenye bili ya maji....kazi iendelee 🐒
 
Yeah kwa mfano carwash, mahotel, mabar, magereji na biashara zote zinazozalisha majitaka kwa wingi na zimeunganishwa kwenye mtandao wa majitaka wanalipia
Labda kwenye hayo malipo serikali itake kuongeza tozo
Mkuu, huduma hii ipo katika maeneo machache sana. Ile miundo mbinu ya maji taka iliyojengwa enzi za ukoloni au wakati wa utawala wa awamu ya kwanza haijawahi kuongezwa.

Kwa Dar ni maeneo ya Kariakoo, Posta, Upanga, Oysterbay, Masaki na sehemu chache za Ilala ndio kuna sewage system inayokwenda baharini

Tanga kwa mfano mfumo huo uliwekwa na Wakoloni na upo maeneo ya mjini. New locations nyingi hakuna mifumo ya maji taka.

Hata kwa Dar maeneo kama Kinyerezi, Mbweni, Mikocheni, Sinza nk kumepangiliwa vizuri sana lakini kwa mshangao mkibwa hawakuweka mfumo huo ambao sio tu unasaidia ku manage usafi kwenye miji bali pia kua chanzo kizuri na kikubwa cha mapato kwa mamlaka husika na Serikali kwa ujumla
 
Back
Top Bottom