Kuna chama mpaka kampeni zinaisha hawatatamka neno haki kwenye mikutano yao

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,870
2,000
Habari iwe kwenu wakuu!

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya watanzania kufanya maamuzi kwenye sanduku la kura , nimefuatilia kwa ukaribu sana kamapeni za wagombea mbali mbali na kilichonishangaza ni kushindwa wa wanachama, wapambe, viongozi na wagombea wa CCM kutamka neno haki kwenye kampeni zao. Cha kushangaza zaidi ni kwamba hata viongozi wa dini wanaombatana nao huwezi kuwakuta wanahubiri neno haki badala yake wamekuwa wakisisitiza juu ya amani wakisahau kuwa amani ni tunda la haki.

Mgombea na viongozi wa ccm ni wanufaika wakubwa sana wa uwepo wa amani hii iliyopo tanzania na bila shaka wananufaika pia na watanzania wengi kutokujua haki zao. Wanaweza kuamua kutengeneza vitambulisho wakavipa jina lolote na wakakusanya hela bila kuwaeleza watanzania kuwa hizo hela wanazifanyia kazi gani. Wanaweza wakakataa kupeleka maendelea kwenye majimbo ya upinzani kama wanavyodai wenyewe huku wakikusanya kodi kwenye majimbo hayo. Wanaweza kujisifia viongozi wao kutumia mavieite (V8) huku wananchi wakiwa hawana maji safi ya kunywa. Wanaweza kuamua kutokuongeza wafanyakazi mishahara kwa miaka 5 na wasione kwamba ni ajabu hata kidogo, wako tayari kuwalea watu wanaokalia haki za watu na kuwafariji watu hao kuwa wakae kwa amani maana bila amani hakuna amani.

Inakuwaje kamapeni nzima mtu anaweza asitamke neno haki hata kwa bahati mbaya? kwahiyo tukubaliane kwamba kwenye misamiati ya wana ccm neno haki haipo kabisa?. Mtu anawezaje kusema yeye ni mpenzi wa Mungu huku kweli na haki havimo ndani yake. Mungu ni Mungu wa haki tena anahukumu kwa haki tena yeye huwatenda kwa haki waovu na wema ila watu wanaojisifu kuwa ni wapenzi wa Mungu hawawezi kuhubiri juu ya haki. Viongozi wa dini nao wengi wao wameacha kweli na haki ya Kristo wanahuburi tu amani pasipo kuzungumzia haki. Wanasau kuwa haki huinua taifa na dhambi ni aibu kwa watu wote na kwamba mwenye haki akitawala wtu hufurahi. Kwangu mimi na familia yangu HAKI KWANZA AMANI BAADAYE, HAKI NDIYO SHINA NA AMANI NI TUNDA haki amani haipo. Kama unapenda haki tumtafutie kura mpenda haki mwenzetu , anza na familia yako, majirani, wetu kwenye contact zako, watu wa kazini kwako , wakwe zako, wajomba etc wahubirie umuhimu wa haki , uhuru na maendeleo ya watu.

Kindikwili
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom