Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,216
- 113,519
Tetemeko lililotokea jana huko Chile ni moja ya matetemeko makubwa sana kutokea duniani. Vipimo vyake vilikuwa 8.8 kwenye mzani wa Richter. Hakika hili lilikuwa kubwa zaidi kuliko lile la Haiti lililotokea mwezi uliopita ambalo vipimo vyake vilikuwa 7.0
Cha kushangaza hili la Chile inaonekana maafa yake hayatakuwa makubwa sana ukilinganisha na lile la Haiti. Hii pengine ni kwa sababu Chile ilikuwa imejiandaa vya kutosha na janga kama hili kwa sababu ya uwepo wake kwenye ule ukanda wa ring of fire kwenye bahari ya Pacific ambako matetemeko mengi ya ardhi hutokea. Maandalizi hayo yanaelekea yameweza kuepusha maafa makubwa zaidi ya yaliyotokea.
Mpaka sasa Chile hawajaomba msaada kutoka kwa yeyote yule, si Marekani wala majirani zao Argentina. Bila shaka wana uwezo na ujuzi wa kutosha kukabiliana na kilichotokea.
Sasa nimekaa hapa nikakumbuka Mzee Mwanakijiji hupenda kusema taifa lisilojiandaa kwa majanga hujiandaa kwa maafa. Binafsi kwa kweli nimevutiwa na jinsi Chile walivyokabiliana na wanavyoendelea kukabiliana na janga hili. Inavyoelekea hata majengo yao yamejengwa imara kuweza kuhimili matetemeko makubwa kama hili la jana. Sasa sijui sisi kama taifa tumejifunza nini kutoka Chile jinsi ya kujiandaa na majanga haya ya asili.