Kuna binti nilimuahidi nitamuoa mwaka huu ila bado mambo magumu, nifanyeje?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Huyu binti nina mwaka nipo nae katika mahusiano na moja kati ya promise niliyomuahidi nitamuoa mwaka huu mambo yangu yatakapokaa sawa Ila mpka sasa mambo magumu.

Na binti naye kwao wameanza kumsumbua kwani alishawaeleza ana mchumba anataka kumuoa sasa home kwao mpaka sasa hivi wananisikilizia Mimi nitaenda lini kujitambulisha, kutoa Mahari tufunge harusi na mimi kila nijiangalia financially sipo vizuri.

Je, nifanye nini kuepuka hiki kikombe mpaka mambo yangu yatakapokaa sawa maana mpka sasa sina ajira na biashara haziendi kabisa?

1627976904346.png

 
We jamaa unataka kumuua mleta mada. Mtu anakuambia hana ajira na biashara haziendi we unamshauri akakope mke kweli? Halafu atakuja kuishi vipi na huyo mke sasa?
Man ee we unadhani kama mambo hayamwendei sawia atafanyaje... bora aende akawambie kuwa hana ila ataleta akipata, alafu wao ndo wataamua.
 
Kamati ya wanaume Taifa ilipitisha sheria kwamba Hakuna kutoa ahadi wakati unafinyiwa kwa ndani, ulipuuza sasa unaona yanayokupata.
Wewe mueleze halihalisi na Kama unampenda kweli nenda kwao ongea na mzee wake mueleze. Yeye mwenyewe anaelewa.
👉Kama humpendi na uko tayari kumpoteza huyo mwanamke hili jambo utaon jepesi ila kma humpendi utaona ni mzigo
 
Unataka kuingia jela ya mateso?
1. Ndoa NGUMU
2. Ndoa SHIDA
3. Ndoa NDOANO
4. Ndoa MAJANGA
5. Ndoa MATESO
6. ..........
7. .........
8. ....
|
100.

We nyandua SEPA.

Ole wako uoe halafu kesho utuletee nyuzi za malalamiko.

SHAURI YAKO.

#YNWA
 
Je nifanye nini kuepuka hiki kikombe mpaka mambo yangu yatakapokaa sawa maana mpka sasa sina ajira na biashara haziendi kabisa.

Tuachie mzigo huo sisi wenye ajira na biashara zetu zinaenda vizuri kabisa...

Hivi hujui kuwa nyama huliwa na mwenye kisu kikali!!
 
Kuoa ni jambo la wakati tu Mkuu wala sio swala la maisha kuwa mazuri. Wazee walikuwa wanaoa hawana misingi imara ila wamedumu sana na ndoa sisi tunaoa tukiwa na misingi imara na hatudumu na ndoa.

Mkuu kama unaona kabisa huu ni wakati wa mimi kuoa oa, unaweza kusubiri upate maisha mazuri ukayapata kweli ukaoa then ukafilisika vipi mke utamrudisha kwao?

Fanya maamuzi tu Mkuu, akikataa au wakikataa kisa hujasimama vizuri achana naye fanya mambo mengine, uje kuoa mwanamke mwengine pia, usijesema utamrudia.
 
Binti kama haelewi sasa mtafanyaje maana maisha ni yenu mwambie hali mbaya kama anawezs kuku finance uje kumlipa badae sawa kwa sababu swala la ndoa ni swala sensitive na linakuja na majukumu mazito!
 
Je, huyo binti ana shughuli ya kumuingizia kipato? Kama vipi oa ivo ivo iwapo anakubali kuishi nawe kwenye shida na raha!
 
Katika kila jambo lazima upimwe ba kujaribiwa. Nakushauri uoe. Iakini kabla kuwa muwazi kwa mwanamke. 1. Mweleze nini unafanya. 2. Unaingiza kiasi gani. 3. Unategemea kuishi vipi naye. Ni ili kama ameweka matazamio makubwa ayashushe ikiwa atakubali muweze kuishi kwa amani. Pia anaweza kukushauri na kuwashirikisha wazazi wake wakajua hali yako, hii itakusaidia baadae.

Ukiona aibu usipokuwa muwazi atakuwa na mategemeo makubwa na baadae atakusumbua sana na kama ni mlalamikaji ndoa itakuwa chungu sana hasa utakapoanza kupata watoto.
 
Back
Top Bottom