Kuna baadhi ya wamabongi flava wanajitahidi hebu check hizi lyrics | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna baadhi ya wamabongi flava wanajitahidi hebu check hizi lyrics

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by RayB, May 18, 2010.

 1. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  SONG MR-PRESIDENT
  ARTIST R.O.M.A
  PRODUCER J-RIDER + YUDDI
  STUDIO TONGWE RECORDS
  CONTACTS R.O.M.A- 0717-72007_?
  romabraq@yahoo.com
  INTRO
  By…..Mwl. Julius Kambarage Nyerere
  Ikulu ni mahali patakatifu, ikulu ni mahala patakatifu,
  Mimi sikucha guliwa na wananchi wa Tanzania
  Kuja kupageuza kuwa pango la walanguzi
  Claps claps claps
  By…Roma
  Drop drop drop drop drop yop
  Haaa haaa… yes Surprise …Tongwe records
  We are here for revolution wooord
  Mr. president ..welcome to white house
  Thank you….aaaah …thank you ….yeaaah

  VERSE….1
  Mi ndo’ roma mkatoliki mwenye asili ya kiyahudi
  Mpare wa milimani sa lamu ya kikwetu urewedi
  We ni mkwere wa chalinze ambaye hutamsahau mnyakyusa...(Mwakyembeee)
  Aliye wafundisha monduli siasa
  Aliyekula kiapo kwa agano jipya la wakorintho
  Siyo msabato mwenye siasa za kubattle kama Zitto
  Mwenye wito wa Appocalypto husssle za Kambikatoto
  Msaka ndoto kama kristo shujaa kama Mrisho Mpoto
  Jasiri kama Mandela busara kama Nyerere
  Niliyejificha mapangoni mithili ya Otango Osale
  So usinidanganye kwa uchawi waaa kutumia ndulele
  Au vita vya majimaji nife kama Kinjekitile
  Hatutaki siasa za kale, siku hizi tunawahi kubalehe
  Nawapa pole wakazi wote wa Tandale kwa Mtogole
  Akhsante Sheikh umeniita ikulu sio kisa nina nyota ya mshale
  Najua mvi sio busara ila naomba amani itawale
  Ikulu yako ina thamani zaidi ya falme za kiarabu
  Cha ajabu hawaithamini na inapoteza thawabu
  Taifa lilikutabri tangu enzi ukiwa waziri
  J.K wa 2 utakuja ongoza hii serikali
  Yenye vilio kote kama kina mama wa Galilaya
  Wanaoutafuta ukombozi wasimamishe Pobilahaya
  Viongozi wetu ni mafia na mabeautifull lier
  Nilikuwa na ndoto hizo ila bado hawaja niinspire

  CHORUS
  Pagani si mlituahidi mtamwaga na lami vipiii?...Badoooo
  Wanafuzi mlituahidi walimu mtawaleta!!...woooh
  Morogoro na Tanga vipiii?Badooo
  Dodoma…?Badooo…
  Kigoma…?Badooo..
  Maisha bora kwa watanzania nyie wenyewe mlituambia
  Manurse…?Badooo
  Mapolice…?Badooo
  Ajira kwa vijana na maendeleo kwa kina mama
  Watotoo…?Badooo
  Kina mamaaa…?Badoooo

  VERSE….2

  Inafahamika ulipewa nchi angali imeshachafuka
  Uongoze hii familia kubwa ya kizazi cha nyoka
  Na ukakubali kubeba huu msalaba wa ukombozi
  Hizi kashfa ndo’ changamoto zisikutoe machozi
  Sitosahau campaign zako za mwaka 2005
  Nilichomwa na jua nikingoja upite nipunge mkono
  Traffic aliyepangwa saa moja kisha ukapita saa saba
  Akiwa na stress za mwanae shuleni kafukuzwa ada
  Leo mna nyumba mna mashamba mna viwanja mna viwanda
  Mi nasaga na rhumba na mshahara wangu haujapanda
  Yule traffic maisha magumu aaah muogopeni Mungu
  Nikisema it is not fair mnataka mnifunge pingu
  Gerezani kesi za wanyonge cheki zinapigwa tarehe
  Jamhuri itafata mkondo ee mola wangu wasamehe
  Wasaliti kama Eskarioti mbele ya Yesu Mnazarethi
  Wa sakramenti ya ekaristi bado hawaitaki torati!!
  Harakati ndo’ jadi siogopi hadi wanichape mjeledi
  Hadi yuddi alikuwa shahidi kwa vinanda na vinubi
  Elimu yetu bahati nasibu kama mikopo ya desi
  Kimbilio la waliofeli ni ualimu na upolisi
  Wamefisadi tenda ya rada, ndege ya raisi, magari ya jeshi
  Wote matraitor sasa skrepa kama Lubumbashi
  Wanapata alama za juu kwa kumuhonga penzi professor
  Mtunza pesa wa benki kuu kumbe pepa zote alidesa
  Au unataka 2010 mapinduzi yawe ya Liberia
  Eti utajiri ni mbuga, milima na ziwa Vicktoria
  Piga vita ujinga, umasikini na H.I.V carriers
  Askofu kutawala nchi hatutaki hizo elimu dunia
  Migomo ya chuo kikuu naitupia jicho la 3
  Sitetei mpaka Rutashoborwa akiwa wakili kisutu
  Kul - nafs - dhal - kal - maut inasema torati
  Rest in peace shusha bendera ipepee nusu mlingoti
  Bungeni hawaijadili bajeti ya mlala hoi
  Mtu hataishi kwa mkate bali neno siyo divai
  Tazama timu yako iliyoko madarakani
  Na mchunguze kwa makini anayelia sana msibani.

  CHORUS

  Walimu si mlituahidi mtatupa hela zetu vipiii…?Badooo
  Mitihani si mliahidi haitavuja tena….woooooh
  Nachingwea na Mbeya vipiii…?Badooo
  Tabora…?Badooo
  Mtwara…?Badooo
  Maisha bora kwa watanzania nyie wenyewe mlituambia
  Wamachinga…?Badoooo
  Wakulima…?Badooo
  Ajira kwa vijana na maendeleo kwa kina mama
  Wazee…?Badooo
  Vyuo vikuu…?Badooo

  VERSE….3

  Huu sio wakati wa kuwaua maalbino
  Angalau mapinduzi kama Macio Maximo
  Usihangaike kumtafuta Roma…mi!! Hakimu wa getho
  Mwenye sauti ya mamlaka!!! iliyomfikisha Mrombo Keko
  Baada ya kukemea ufisadi na sera za Karamagi
  Na waliokula jasho letu kwenye migodi ya Buzwagi
  Utazuia vipi ongezeko la wimbi la ukeketaji…
  Wakati Ngariba ndo’ diwani wa kata kwenye kijiji!!
  Neither do I…!! hongera ulipima ukimwi
  Watanzania nasi tuamke tusimpige kibao tu Mwinyi
  Hapa nagundua aya-tul - munafik - thalatha
  Inawezekana aliishia alifu wakati anasoma madrasa
  Huu sio muda wa kujadili kesi za Manji na Mengi
  Hayo ya Mungu we Kaisari jadili mambo ya msingi
  Teacher alipojiita mtabiri Tanganyika wote vipofu
  Padre wa kwanza pentekoste ubatizo wa maji marefu
  Machozi yalinitoka Segera watoto hawapati haki
  Wengi wamekimbia shule basi lije wauze visheti
  Wanaosomeshwa kwa mtaji wa chapati na uvuvi wa samaki
  Wabunge wao wamekaa na wanajiita wanaharakati!!
  Rudi kwenu kahamasishe nduguzo hawana taaluma
  Wazaramo wamegoma soma still mwali wanamcheza ngoma
  Wanalia Kilwa Kivinje huku wanaocheka ni wabunge
  Walionunua kura ya bibi kwa kumuhonga doti ya kitenge
  Hata wamasai walikuchagua kwa kura nyingi za upendo
  Wakiamini mtetezi yuaja wa jimbo la Oldoyo Sambo
  Waambie what is going on ndani ya himaya ya bwawa la Mtera
  Waonyeshe na mikataba ya utawala wa mgodi wa Kiwira
  Jeshi lote kwenda Tarime hawakuwa na njia mbadala
  Na walioteketea Mbagala!!
  Mr.pres …. Haya masikharaaaa!!!
  Sina maana utoke wewe hicho kiti umuachie professor
  Nisamehe kama nakosea maana mimi sio mwanasiasa
  Claps claps claps

  OUTRO
  By…Mwl...Julius Kambarage Nyerere
  Kwa hiyo kitu kimoja tunataka kuelewa…
  ni hali ya matatizo ya nchi yetu yalivyo sasa hivi....Eee!!
  Kwasababu...sera ya...ay..…awamu ya kwanza…. awamu yangu mimi…
  imefanya mema…. imefanya ya kijinga….
  ya kijinga yanaachwa…!! lazima yaachwe….
  Ubaya wenu ni kwamba…. mnaacha mema...mnachukua ya kijinga.


  NB: NIMEIPENDA SANA HII KITU NA HIVI NDIVYO WASANII WANAVYOTAKIWA KUFANYA ATI
   
 2. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #2
  May 19, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa na mkubali sana kwa kazi zake ni nzuri na zina zungumzia maisha halisi tuliyo nayo Watanzania.....Kuna watu walijitokeza na kumwambia hapunguze ukali wa mashairi yake kwa (Mkulu).

  Niusikiapo huu wimbo huwa napata matumaini kuwa kama msanii tu anaweza kuimba hivi basi ipo siku hii nchi itakombolewa na vjn toka kwa hawa mafisadi wanaoendelea kuturudisha kwenye umaskini kila siku.....

  Mungu ibariki kazi ya mikono yangu ili familia yangu ipate mkate wa kila siku maana nimekata tamaa na hali ya nchi yangu Amen!!!
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  wakati wasanii wengine wanatoa beti za namna hii wengine wanahamasisha kuchangia ccm!

  hebu tuwekeee na video au audio yake tafanyali
   
 4. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #4
  May 19, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  View attachment 10352
  [video]http://www.eastafricantube.com/media/23997/Re:_ROMA_-_MR_PRESIDENT/[/video]
   
 5. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Daaah huu wimbo nimeshausikia ila kweli huu utunzi sikua makini kuusikiliza kwa kina, Huyu msanii anafaa kupata tuzo ya Msanii Bora Mzalendo wa Tanzania 2009/10, sio wale kina mbagala na kamuambie full kuimba mapenzi mapenzi ambayo hayana faida kwa mlala hoi amabe hana hela kwa hiyo hajala chakula na hayo mapenzi atafanyaje kama hajamfia mtu kifuani. Wasinii wetu wabadilike waimbe vitu vianvyoikosoa serikali na kelimisha jamii bila kuogopa kwani kila binadamu ana haki ya kueleza hisia zake bila kumtukana mtu.Kazi kuimba ANANIPENDA ANANIPENDA NAMPENDA NAMPENDA......., Je hatuna la kusikia la maana zaidi ya hayo..............? #@#%$^$&$ zenu.
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hiyo link sio ya wimbo huo mbona!
   
 7. G

  Gabby Member

  #7
  May 19, 2010
  Joined: May 18, 2010
  Messages: 32
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Huyu ni mzalendo wa kweli. Mwacheni aseme yaliyo moyoni. Si mmesikia wameanza kung'atuana huko Iringa?
  Bado tunasubiri ile nchi ya ahadi ya maishabora kwa kila MTZ. Lakini caution ni kuwa lazima tuwe na akili za MBAYUWAYU kwa vile 315k hatuna uwezo nazo.
   
 8. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Well done ROMA, I salute u
   
 9. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huyu dodo yuko safi ile mbaya ila nimesikia akilalamika nyimbo zake zimepigwa marufuku kupigwa redioni hasa vedeo zake kwenye luninga na serikali. source clouds fm
   
 10. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kama hiyo ni kweli basi kaka hii ni hatari kabisa na huu uhuru wa kujieleza uko wapi? Dogo kama huyu huwezi kumkuta katika matangazo ya CHANGIA CCM kama wengine
   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  dah umenikuna ku mtima wangu nimemkubari kijana, tunataka
  vijana wenye mitazamo kama hiyo,
  huyo dogo hata akiambiwa maisha bora kwa kila mtanzania, lazima atahoji
  badala ya kupiga makofi ka' b'wege, big up sana kijana
   
 12. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,714
  Likes Received: 8,269
  Trophy Points: 280
  Ya kweli haya!??
  Basi tumeisha..
   
 13. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,714
  Likes Received: 8,269
  Trophy Points: 280
  Nasikia ana nyingine kali kuliko hii yaitwa Tanzania..una lyrics zake mkuu!???
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Garbido populism geared at capturing the Nyerere revering Borgs in Tanzania.

  Wewe mtu mweusi tii utajiitaje Myahudi?

  Ndio hawa wale wale wanajipimp kuwa agents wa change halafu kesho keshokukutwa mkiwakuta kwenye matangazo ya CCM complete with Green and Yellow T-Shirts mnakuwa disappointed.

  This does not impress me at all.
   
 15. M

  Mutu JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huyu anaimba nyimbo za ukombozi , maana utawala wa sasa ni wakinyonyaji kushinda wakikoloni
   
 16. M

  Mutu JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama ulisoma bongo hukusoma kiswahili kiasi cha kujua SANAA ni nini na vitu kama tungo,fanani,maudhui ,hadhila..............na jukumu la kutafsiri tungo ni la nani!
  The same in english ART.............

  Ukitaka ibaki kama ilivyo ni kwamba kuna Wayahudi weusi kama mkaa kama una exposure utalijua hili.So do your homework .
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Huu utumbo wa ku ride the populist wave, complete with formulaic Nyerere clips ndiyo unaona art?

  Huyu self loathing black african Jew wannabee ndiye unamuona artist?

  No wonder kesho keshokutwa vichwapanzi hawa hawa wakipanda jukwaani na bendera ya CCM kuna watu kama JMushi wanataka ku commit suicide kama wamepigwa kibuti na demu siku ya harusi.

  I can see clearly through all this BS, nothing new or impressing here. As a matter of fact I see a vile and juvenile attempt at greatness, and I can go at it line by line, toe by toe, buck by buck.

  Just dare me.
   
 18. M

  Mutu JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapo pekundu kheri mimi sijaona ahaaaaaaaaaaa the guy 'll come swinging
   
 19. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wewe mtu mweusi tii utajiitaje Myahudi?
  If this is the case then umepotoka wapo wayahudi weusi tii just for your information (Tazama picha hapo chini)!!!!!!! Halafu mkuu pamoja na kwamba ni haki yako kupinga au kuwa na maoni tofauti juu ya wimbo wa msanii huyu, U have taken it too personal na kusahau kwamba hii ni fasihi!

  [​IMG]


  Ndio hawa wale wale wanajipimp kuwa agents wa change halafu kesho keshokukutwa mkiwakuta kwenye matangazo ya CCM complete with Green and Yellow T-Shirts mnakuwa disappointed. - Hii ni mojawapo ya maana na gharama za demokrasia.
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Hao ndio wale wale self loathing blacks wanaotaka kujitoa kwenye blackness.

  The only black Jews I know are the Falashas, and they are not "weusi tii" wametyoka Ethiopia huko.

  The Jewish religion -if you are talking about this in religious context- wants nothing to do with blacks, just try to go to a Jewish Synagogue and see.

  Kijana at best anaweza kuwa anahitaji maelekezo kuhusu lines gani aondoe, na lines gani aongeze.

  He is not the next bets thing he is trouted out to be.First of all he invests too much in religiosity and the scriptures while religiosity and the scriptures are nothing buit the oppressors tool.How can you fight the oppressor by using his very own tools of oppression?
  '
  '
   
Loading...