Kuna baadhi ya kazi hazitafutwi wakati upo desperate

miamiatz

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
504
927
Kukekuwa na wimbi kubwa la utafutaji wa kazi huku mtu akiwa desperate. Yaani unakuta ameshajikatia tamaa, ameshajichokea, ameshajiambia acha nitafute yoyote.

Hii ni hatua mbaya kufikia na ukifikia hatua hii basi baadhi ya kazi haifai kuziomba. Mfano mmoja wa kazi hizi ni kazi za kwenye makampuni ya consultancy.

Hizo kampuni za consultancy zinatoa huduma za ushauri kwa wateja wao. Hebu jiulize mtu tayari mood ya maisha ishabadilika na ameshajikatia tamaa unampa kazi ya kwenda kupembua jambo kwa mteja kisha awashauri cha kufanya.

Ukishakuwa desperate hata kushauri huwezi. Kichwa kinakuwa mzigo. Hakuna hatua mbaya kama hatua ya kujikatia tamaa. Bora utafute kitu cha kufanya cha kukukeep busy hata kama hakiingizi pesa.

Courtesy of miamiatz
 
Hizo kazi za Consultancy companies huwa ni za watu wazoefu na hiyo career na akiwepo junior/fresh graduate huwa ana assist tu hatoi ushauri na hao wenye uzoefu ushauri wanatoa tu vizuri maana ana uzoefu wa zaidi ya 5 years so hakosei
 
Hazitafutwi ukiwa desperate kupata kazi au desperate kufanya kazi?
 
Back
Top Bottom