Kuna athari zozote kama tukivunja uhusiano na WB,IMF au Marekani?

Hiyo AfDB biggest investors ndio nchi zilezile zinazotoa pesa kupitia WB na IMF.

Suppose waafrika wote tujitoe kwa pamoja halafu tuanzishe taasisi yetu. There comes a conundrum maana nchi za kiafrica ndio wakopaji wakubwa kupitia banks na wengi wana makusanyo pungufu ya kukidhi budget zao who is to fund that new institution?

Kuachana na WB inabidi kwanza tuwe na uchumi unaoweza walau kukusanya mapato ya kukidhi budget yetu vinginevyo ni day dreaming.
 
Inawezekana ila ni vema kupunguza nao mazoea taratibu kwanza tukijiandaa kujijenga.... Lakini hilo litawezekana zaidi kama tutaimarisha benki yetu ya Africa na kuwa na common fund plus kujenga uchumi wa afrika usio na mashiko na mataifa ya nje ya afrika kwa maana kujitegemea kwa mikopo ya masharti nafuu.

Lakini pia, ni vema kujijenga upya kitaasisi kwa kuanza na taasisi namba moja ambayo ni familia ili kujenga ustawi wa jamii ngazi ya kata hadi taifa.

Viongozi wanaopiga madili hawa ni wakuwadhibiti kwa kila namna na kuwacontain na pia turekebishe mifumo ya kisheria ya biashara, kiuchumi, na haki za kiraia.
Bila kubadili mfumo wa uongozi ni ngumu kutokuwa tegemezi
 
Kwa Tanzania bado hata kuthubutu hatuwezi kuvunja uhusiano na USA
hakuna nchi imewahi kuvunja uhusiano na WB na IMF, kuhusu Marekani athari yake ni tutakosa misaada lakini kuvunja uhusiano nao inawezekana mfano Zaire ilivunja uhusiano na Marekani kwa sababu Marekani ilishiriki jaribio la kumpindua Rais na ikavunja uhusiano na Belgium kwa sababu kuna mwandishi wa ki belgiji aliandika kitabu cha kumkashifu rais
 
Huo ndio ukweli ambao baadhi ya mataga hawapendi kuukubali kisa itikadi
Mkuu be serious. Hapa Tanzania, hakuna kiongozi mwenye utashi, nia wala jeuri ya kuvunja uhusiano na taasisi hizo. Kinachoendelea ni politiki uchwara kuwafunga kamba “wanyonge” - period.

Hata Nyerere alijua hana jeuri hiyo. Angalau alisimamia mwiko wake binafsi wa yeye kutokuwa na mkono katika makubaliano ya kushinikizwa na “mabeberu” hao; akampasia mzee ruksa urais na zigo lake la kumwaga wino kwenye makubaliano na IMF.

Tusimame na kutembea kwa miguu yetu wenyewe? Won’t happen kwenye jamii iliyojaa watu wanaoshindana kuwa wajanja, kula bata kwa sana kwa utajiri wa harakaharaka wa kufisidi dola, kuchezesha kamari, kuchuuza upako, miujiza, ulozi n.k.

Tumeachwa mbali kabisa na nchi za Asia ya mbali (China, Japan, Malaysia, Singapore, n.k.) zenye utamaduni wa kufanya kazi kwa juhudi kubwa na maarifa ambazo, pamoja na yote, hazina mpango wa kilevi wa kukorofishana na Marekani, WB, IMF.
 
Hilo swali unhemuuliza marehemu Mugabe. Mzee wale no nyuki ikiwagusa mkate Tanzania utaununua shs elf 20. Mugabe walimulisha njaa mpk wajida wakampa kifo ca mende kapinduka. Usichezee Mmarekani sharubu zake utajuta kuzaliwa
 
Back
Top Bottom