Kuna athari zozote kama tukivunja uhusiano na WB,IMF au Marekani?

Ungejua Marekani ameajiri waTanzania wangapi kupitia miradi mbalimbali kwenye Afya, Elimu na Kilimo usingeongea upupu huu
 
Kipimo cha "kuleta mabadiliko" kukoje mkuu sblandes'?
Unajuaje kuwa hakukuleta mabadiliko, au ulitaka siku hiyo hiyo ya "kuvunja uhusiano na Marekani" Uhuru wa Zimbabwe upatikane?
Mkuu alitaka USA isitambue utawala wa mlowezi mzungu Ian Smith na iwawekee vikwazo vya uchumi.
Ian Smith alikuwa ametangaza na kunyinyakulia madaraka ya kutawala South Rhodesia ambayo sasa ni Zimbabwe baada ya wakoloni Waingereza kucheza rafu nyingi tu.Mwl Nyerere alibadirisha strategy akatafuta njia ya mazungumzo kimataifa na huku akiunga vita vya ukombozi.
USA haikubadirisha sera yake hadi 1980 ilipopatikana majority rule.
 
Kumbe kama ni kwa 40% basi tuachane nao tu. Maana bila ya kuachana nao nchi yetu itaendelea kugawanyika kati ya Vibaraka wa mabeberu na wazalendo. Nadhani tukiachana nao Tanzania itabaki na wazalendo tu wanaopambana kwa manufaa ya nchi yao!!
Wewe jamaa unatetea kitu ambacho hakiwezekani.
Ktk Africa, nchi ambayo haikufungamana na IMF au World bank ilikuwa ni Botswana. Lakini institutions hizo zilihakikisha Botswana lazima iwe tied kwao ili kuweza kudhibiti uchumi wa kila nchi Africa na kwingineko.
IMF na world bank ni taasisi zenye kudhibiti chumi za dunia. Ndiyo maana hata Mwlm Nyerere (pia Rais jiwe) alishindwa kutunishiana vifua na wao.
 
Amini usiamini tanzania tuko vizuri midomo kwa maneno mengi tu.. hatujambo! ila kwa hilo haliwezi kutokea milele ni waoga kupindukia mikia katikati ya miguu.
 
Hivi Bavicha mnamatatizo gani kwani sasa tuvunje mahusiano ili iweje?

Au umetumwa Mkuu

Hardworking pays!!!

Sidhani unaelewa vizuri mada ya jamaa. Amezingatia kuwa ni hawa ndio mabeberu, wanatupa misaada na mikopo yenye masharti magumu na huwa wanawatuma watu wetu ndani ya nchi kufanya jambo fulani.

Ili kuwakwepa mabeberu, anauliza hatuwezi kuwaacha tu??? Sidhani ni swala la Bavicha.
 
Hamtachukua hata miezi 3 hali itakuwa tete dollar haitapatika, mafuta yatapanda kwa vikwazo kiufupi watu wenye mitaji watakimbia nchi faster.
 
Hivi kuna jambo lolote baya litatokea kama Tanzania tukiamua kuvunja uhusiano na Shirika la fedha Ulimwenguni (IMF), Benki ya Dunia (WB), au nchi ya Marekani? Badala ya mjadala wa kuendelea ama kutokuendelea kuwa na uhusiano na taasisi hizo ama nchi ya Marekani kwa nini kama taifa tusiamue uhusiano ufe?

Maana ni kama kila wakati inakuwa ni mjadala wa nani kibaraka ama mzalendo kuelekea taasisi hizo na nchi ya Marekani. Hivi kuna ulazima wa kuwa na Mahusiano nao?

Ni wakati wa kusimama na kutembea kwa miguu yetu wenyewe!!
Inawezekana mkuu kuvunja uhusiano na Marekani na watukome kabisa.
Ila vitu vifuatavyo kwanza tuvikomeshe au tuvirekebishe;
1.Makubaliano ya mkutano wa wizi wa Berlin kuhusu Tanganyika tuuvunje.
2. Soko kuu LA dhahabu ni marekani ivyo tuchimbe na kutumia wenyewe.
3. Mwekezaji mkuu Barick. Ggm nk. Ni mmarekani ivyo tujue jinsi ya kufanya.
4. ARV
5.watalii wengi na wenye makampuni mengi ni marekani.
6.Wasomi wengi wanapenda marekani na vyuo konki marekani.
7.tujichapishie ela yetu tusiwategemee wao.
8.Lions club, Word vision yaani taasisi izi zote tustopishe kazi zake kwetu.
9.. Na mengine lukuki.
Apo tutakuwa free kuvunja uhusiano na wao.
NB: Marekani ndo (WB na IMF ).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni rahisi kuwafurusha Wasukuma kuliko kuvunja uhusiano na hao
Lakini mara kadhaa tumeonesha kwamba maisha yetu yanaweza kusonga mbele bila ya wao. Nakumbuka kwenye hotuba yake moja Mwalimu alisema kwamba haiwezekani kuwa - Defy hawa wakubwa. Lakini siku hizi tupo wazalendo tunaoamini ni wao wanaofaidika na sisi na si sisi tunaofaidika nao. KWA NINI TUSIACHANE NAO TU??
 
Huwezi kuwa kisiwa utakufa.
Ukishirikiana nao positive huwezi kuwa masikini
 
Lakini mara kadhaa tumeonesha kwamba maisha yetu yanaweza kusonga mbele bila ya wao. Nakumbuka kwenye hotuba yake moja Mwalimu alisema kwamba haiwezekani kuwa - Defy hawa wakubwa. Lakini siku hizi tupo wazalendo tunaoamini ni wao wanaofaidika na sisi na si sisi tunaofaidika nao. KWA NINI TUSIACHANE NAO TU??
Serikali imeshindwa kuondokana na mabenki ya ndani kama CRDB, NMB, Standard Chartered, n.k haya yanaidai serikali matrilioni ya shilling. Sasa utaondokanaje na hawa mabwana wa dunia akina World Bank, IFM, na hata African Development Bank imekuwa bwana mkubwa pia.
 
Mkuu alitaka USA isitambue utawala wa mlowezi mzungu Ian Smith na iwawekee vikwazo vya uchumi.
Ian Smith alikuwa ametangaza na kunyinyakulia madaraka ya kutawala South Rhodesia ambayo sasa ni Zimbabwe baada ya wakoloni Waingereza kucheza rafu nyingi tu.Mwl Nyerere alibadirisha strategy akatafuta njia ya mazungumzo kimataifa na huku akiunga vita vya ukombozi.
USA haikubadirisha sera yake hadi 1980 ilipopatikana majority rule.
Aaaha, umeeleza kirefu mkuu 'sblandes'.
Hakuna tofauti kimtazamo kati yetu juu ya hili, isipokuwa:
Elewa kwamba ukimkumbusha mzee (baba) mahali alipokosea na yeye akaona mantiki ya unayomweleza, usitegemee mpaka akueleze kwamba anakili makosa yake.
Anaweza akakaa kimya kwa muda mwingi, lakini utaona mwenyewe mabadiliko yake katika matendo ya mambo hayo hayo taratibu.
 
Inawezekana ila ni vema kupunguza nao mazoea taratibu kwanza tukijiandaa kujijenga.... Lakini hilo litawezekana zaidi kama tutaimarisha benki yetu ya Africa na kuwa na common fund plus kujenga uchumi wa afrika usio na mashiko na mataifa ya nje ya afrika kwa maana kujitegemea kwa mikopo ya masharti nafuu.

Lakini pia, ni vema kujijenga upya kitaasisi kwa kuanza na taasisi namba moja ambayo ni familia ili kujenga ustawi wa jamii ngazi ya kata hadi taifa.

Viongozi wanaopiga madili hawa ni wakuwadhibiti kwa kila namna na kuwacontain na pia turekebishe mifumo ya kisheria ya biashara, kiuchumi, na haki za kiraia.
 
Back
Top Bottom